Shimilimana
Member
- Mar 12, 2013
- 52
- 15
Salute wana Jf wote: Baada ya kuwa nimefuatilia kwa muda mrefu namna ya hii mitandao ya kuuza bidhaa za tiba lishe/food supplements/food dietary, nimegundua kuwa tiba lishe kama ilivyo haina tatizo bali wasambazaji wake ndiyo wenye tatizo. Mojawapo ya tatizo kubwa nililoliona ni kwa wale wasambazaji wanaomcha Mungu, nimegundua ni wengi sana kama siyo robo tatu ya wote ambao ndiyo hasa nimesukumwa kuwapa tahadhari kwa hiki wanachokifanya. Baada ya kuahidiwa utajiri kwa kushawishi watu kujiunga na mitandao hii, wanatumia nguvu nyingi ikiwemo uwongo ili kuwavuta watu kujiunga na mitadao hii badala ya kutumia nguvu hiyo na ukweli kuwafanya watu wamche Mungu ili wapate utajiri usiyo na mwisho wala majuto. Mwenye kuelewa na aelewe, tubadilike ili tuepuke hasira ya Mungu baada kuwa tumeondoka hapa dudiani na kuuacha utajiri huu wenye hila. Thanks, be blessed
sijui umeandika nini mkuu jiange tena iliueleweke..
:coffee:
kama umesoma vizuri kuna mahali nimesema mwenye kuelewa na aelewe nikitambua kuwepo kwa watu kama wewe watakaoshindwa kunielewa. Asante, barikiwa
Kumbe sio mie pekeyangu ambaye sijaelewa.... 😕 😕
Ni kwepi hujaeleweka ndugu..Fafanua vizuri hii mitandao ni ipi na wanashawishi kivipi..Je una maanisha akina Dk Ndodi?
Wote hao lao moja, waweza danganyika ukafikiri wanasaidia kumbe ni pupa za kutaka mapesa tu, matapeli/wezi hao wotesina shida na watu kama kina Ndodi kwani wao wanatoa tiba na kufundisha watu kufuata kanuni bora za afya ili wawe mbali na magonjwa tofauti na mitandao kama GNLD, wao wana kauli mbiu isemayo 'KULA SEMA' ambayo inatumika kuwapatia utajiri, pia mtandao huu haufundishi watu jinsi ya kuwa na afya njema pale wanapofanya semina zao bali huwataka watu kujiunga nao ili kusambaza(kuuza) supplements, mimi ni shahidi wa hayo kwani nimewahi huhudhuria semina zao. Mitandao mingine ni forever living na mingineyo, tukumbuke Mungu pekee ndiye FOREVER LIVING, thanks
Ni kweli MadamG unayosema, ni budi tufahamu kuwa shortcut yoyote kwa jambo lolote ktk maisha itatuletea madhara na majuto makubwa, pengine ktk maisha yetu yote.....Tuhesabu gharama kabla ya kujenga MNARA.... ThanksUnategemea kwa matokeo ya O-level vikundi hivyo si ndio vitapata wafuasi wengi coz wengi wao wameshajikatia tamaa na matokeo wanaangalia shortcut ya maisha.
sina shida na watu kama kina Ndodi kwani wao wanatoa tiba na kufundisha watu kufuata kanuni bora za afya ili wawe mbali na magonjwa tofauti na mitandao kama GNLD, wao wana kauli mbiu isemayo 'KULA SEMA' ambayo inatumika kuwapatia utajiri, pia mtandao huu haufundishi watu jinsi ya kuwa na afya njema pale wanapofanya semina zao bali huwataka watu kujiunga nao ili kusambaza(kuuza) supplements, mimi ni shahidi wa hayo kwani nimewahi huhudhuria semina zao. Mitandao mingine ni forever living na mingineyo, tukumbuke Mungu pekee ndiye FOREVER LIVING, thanks
Pyramid schemes....yaani ni utapeli mtupuIwapo unakula chakula bora utapata viini vyote ambavyo vinahitajika na mwili. Hutahitaji hizo supplement zinazokazaniwa na hao wanapyramid schemes mbalimbali.