Tahadhari ya upungufu wa chakula yatolewa kutokana na mvua chache

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa mwezi Oktoba, Novemba na Disemba unaonyesha kwamba maeneo mengi ya nchi yatapata mvua chache na hivyo kusababisha athari ikiwemo upungufu wa chakula.

Mkurugenzi mkuu wa TMA Dkt Agnes Kijazi amesema hayo leo jijini Dar es salaam na kuwashauri wakulima kupanda mbegu za mazao ambazo zinakua hazihitaji maji mengi.

Dkt Kijazi pia ameeleza kuwa athari hizo zitajitokeza si kwa Tanzania pekee bali pia ni kwa nchi zote za Afrika Mashariki huku akieleza athari hizo kwa sekta mbali mbali hapa nchini ikiwemo wafugaji na wakulima.
 
Huwa nawaza jambo moja. Kama nchi huwa tuna mipango ipi endelevu ya kupanda miti na kutengeneza na kuendeleza misitu kwa ajili ya kureplace miti inayochomwa kila siku kutengeneza MKAA na pia kuhifadhi mazingira kwa kizazi hiki na kijacho.
 
Ipo sema mdogo mdogo
 
Tufafanulie kidogo sisi wananchi wa kawaida tuweza kuelewa na hata kushiriki katika utekelezaji inapobidi.
Mfano mlima kilimanjaro kunamradi wa kushiriki kupanda miti kila mwaka na wilayani kuna siku za kuhifadhi uoto wa asili kwa kupanda miti...
 
Huwa nawaza jambo moja. Kama nchi huwa tuna mipango ipi endelevu ya kupanda miti na kutengeneza na kuendeleza misitu kwa ajili ya kureplace miti inayochomwa kila siku kutengeneza MKAA na pia kuhifadhi mazingira kwa kizazi hiki na kijacho.
Ukute apo kwako umepanda nguzo za umeme, fensi na vijiti vyenye kamba za kuanikia nguo halafu unalaumu serikali
 
Pamoja na miti kuchomwa.Bado Tanzania's a INA misitu mikubwa kweli.Tembra katavi,tabora,kigoma,mbeya,Moro nk.misitu bado mingi sana tens iliohifadhiwa na isiohifadhiw.
Mwka Jana nilitaka kuuziwa heka 50 zote ni pori nukaenda uziwa 20 heka sehemu nyingibe Nazo zote ni pori najiandaa kuzifyeka niliweke mazao.
Upungu was wa view a huwa hautokei Tz yote bali janda Fulani, kuna mikoa ukikaa kola mwaka unashuhudia mvua.
 
Hapana. Nyumbani kwangu nina miti zaidi ya 20, miti ya kawaida na ya matunda. Ondoa Hofu. Natekeleza kwa vitendo:D
 
Pamoja na miti kuchomwa.Bado Tanzania's a INA misitu mikubwa kweli.Tembra katavi,tabora,kigoma,mbeya,Moro nk.misitu bado mingi sana tens iliohifadhiwa na isiohifadhiw.
Mwka Jana nilitaka kuuziwa heka 50 zote ni pori nukaenda uziwa 20 heka sehemu nyingibe Nazo zote ni pori najiandaa kuzifyeka niliweke mazao.
Upungu was wa view a huwa hautokei Tz yote bali janda Fulani, kuna mikoa ukikaa kola mwaka unashuhudia mvua.
Sikubaliani sana na wewe. Hali ya mapori na misitu kwa Mkoa wa Morogoro ni tofauti na zamani.... Mapori yanateketea kwa shughuli za kibinadamu.
 
Back
Top Bottom