Tahadhari ya ugaidi

Tony Laurent

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
2,200
2,000
Ndugu Watanzania wenzangu. Tunapoelekea kwenye sikukuu za mwisho wa mwaka, nachukua nafasi hii kuwaomba tuchukue tahadhari kuhusiana na vitendo vya kigaidi ambavyo vinaweza kufanywa na magaidi ama wa ndani au kutoka nje ya nchi. Tuwe makini tunapokuwa kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu, kama vile sehemu za ibada, fukwe,nk. Magaidi ni watu wanaoishi miongoni mwetu. Tutoe taarifa kwenye vyombo vya dola mara tunapoona nyendo zisizo za kawaida za mtu au kikundi cha watu. Kinga ni bora kuliko tiba. Waswahili wanasema mwenzio akinyolewa wewe tia maji. Wenzetu Kenya yamesha wakuta. Vyombo vya dola navyo vitimize wajibu wao ipasavyo. Kwa pamoja tuilinde nchi yetu.
Mungu ibariki Tanzania.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom