malisoka
JF-Expert Member
- Jul 8, 2012
- 1,860
- 2,639
Toka wiki iliyopita mpaka sasa hakuna habari yeyote iliyotolewa na Polisi kuhusu kutekwa kwa MO. yupo wapi? watekaji ni nani? na Watekaji wanataka nini au kwa sababu gani?
Nimejifunza mambo mengi sana hasa uwezo wa wana usalama wetu kushughurikia mambo kama haya.
1. Nchi ipo salama. Lakini usalama unapokuwa haupo basi haipo salama kabisaaaaaa!
Kama uharifu unatendwa asubuhi kweupee na mpaka sasa hakuna matokeo. ni dhahiri kwamba vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinahitaji mafunzo zaidi au kubadirisha kabisa mfumo wa utendaji wao. Badala ya kuwa wanasiasa, wawe huru kwa kila mtu . Nina mashaka kwamba labda mambo haya yamekuwa mazoea masikioni mwao, kutekwa na kutekwa kwa watu.
2. Kama hii ingetokea kwa Rais ingekuwaje? au Ikatokea kwa mwananchi wa kawaida mimi ingekuwaje(labda ningeambiwa nimejiteka).
3. Polisi wajenge mahusiano mazuri na wananchi na sio vitisho.
Unajua kwa nchi za wenzetu walioendelea. Mtoa taarifa wa kwanza kabisa au wanayesaidia polisi au wana usalama kupata habari ni raia wa kawaida na hatimaye wanapata matokeo mazuri. Tofauti na sisi hapa bongo watu wanaweza kuwa wanajua ILA wanaogopa kuoozea jela kwa kuwa tunakuwa suspect number 1. Hasa polisi jengeni urafiki na raia mnaowatumikia msiwafunge ovyo, msiwasingizie makosa, Boresheni mfumo wa polisi jamii. haya yatawasaidia sana.
4. Wanasiasa na matamko yao.
Ninaona ni vizuri waziri wa mabo ya ndani na wanasiasa wengine wangepunguza vitisho na matamko mengi ambayo ni ya kisiasa zaidi kuliko utendaji. wawe watendaji zaidi kuliko kila dakika, kila siku kutoa matamko yasiyokuwa na tija. kwa mfano tunamtaka MO tujue habari zake yupo wapi nk Longo longo na vitisho havisaidii. Kwa mfano wakati wa mlipuko wa mabomu Ubalozi wa Marekani, Waliotoa masaada walikuwa Raia wa kawaida ukiacha mambo ya kitaalamu. Polisi tuambieni gari aina flani au namba flani rangi flani mmeliona wapi?
5. Mafunzo maalumu kwa askali wetu kudeal na matukio kama haya.
Tunaomba muwape askali wetu mafunzo ya hali ya juu kushughulikia matukio kama haya. Inatia aibu na inatutia huruma kwamba mtu anaweza kupotea zaidi ya siku 3 bila habari zake kujulikana mpaka leo(tulidhani kimya kingi kinamshindo). wekeni camera za kisasa kila mtaa. Msisubiri camera za kisiasa za Mkuu wa Jiji Mtachelewa , Tegeni camera zenu binafsi mtazijua ninyi tu na zitawasaidia sana.
Ninawatakia mafanikio mema katika kumtafuta na kumpata ndugu yetu Mo. tutawashukuru sana.
Tunajisikia aibu, tunajisikia hasira, tunajisikia wanyonge sana.