Heshima Comrade..
Tatizo la hili suala Ni kufeli kwa Taasisi za Kifamilia, Jamii na Taifa kwa ujumla wake. Hivi watoto wadogo Kama hao (Panya road) wanaisumbua vipi Jamii?..
Hao Panya road si wanajulikana na wahusika?. Mtoto wa Mzee X, Y na Z?. Sasa kwanini Mamlaka husika isishughulikie root causes na siyo effects pekee?.
Hivi makundi ya kigaidi yakijitokeza na kuwapa hao watoto silaha si watakuwa Al Shabab, M 23 na kadhalika?.
Serikali/Mamlaka husika imekuwa iki-react too slow and un-professional katika hili. Tatizo huwa ni nini?.
Serikali i-deal na latent consequences, intended and un intended consequences katika hili la Panya road. La sivyo watakuwa wengi na kuja kuwazidi wana usalama wetu ambao kimsingi ni wachache sana.
Kwa waliosoma Physics wana concept fulani katika Hooke's Law. Elastic material ikishavuka elasticity, basi inaingia katika second stage iitwayo deformation ambako huwa haiwezi kurudi tena katika original shape.
Panya road watavuka Elastic limit. Wakiingia kwenye Deformation point hakuna atakayebaki salama.
Samaki mkunje angali mbichi. Tuwakunje Panya road still mapema.
Hekima Ni Uhuru.