Tahadhari: Wahuni wanaojiita "panya road" wameanza kusumbua watu tena

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
892
1,226
Kwa wakazi wa Mwananyamala na maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam kuweni na tahadhari na mda na njia mnazopita.

Siku ya jana wamesumbua watu maeneo ya Mwananyamala kwa Kopa kwa kuwapora pikipiki na mabegi ya wanafunzi waliokuwa wanatokea Kairuki wanaoishi Mwananyamala.

Nakushauri usitembee na mabegi wanayoita 'ya pc' watakung'oa mgongo.

Unaposikia hili waambie na mwenzio
 
Mbona huku mikoani hakuna ndugu? Huku hata ukiiba karanga tunachoma moto.
Watu wanaiba mchana mchana halafu people zinawaangalia tu.
Wanaume wa dar tabu tupu. Huku mkoani makundi ya ovyo ovyo hayapo
Itakuwa mkoani hakuna kitu cha kuiba ndo maana hawapo. Alafu mikoani napo ushirikina unawabeba sana nyie.
 
Kwa iyo wanaume wa dar ni tatizo au mbona wana sema asilimia kubwa ya watu wa dar wametokea mikoani ndio maana wazaramo wamekimbia mji
 
Heshima Comrade..

Tatizo la hili suala Ni kufeli kwa Taasisi za Kifamilia, Jamii na Taifa kwa ujumla wake. Hivi watoto wadogo Kama hao (Panya road) wanaisumbua vipi Jamii?..

Hao Panya road si wanajulikana na wahusika?. Mtoto wa Mzee X, Y na Z?. Sasa kwanini Mamlaka husika isishughulikie root causes na siyo effects pekee?.

Hivi makundi ya kigaidi yakijitokeza na kuwapa hao watoto silaha si watakuwa Al Shabab, M 23 na kadhalika?.

Serikali/Mamlaka husika imekuwa iki-react too slow and un-professional katika hili. Tatizo huwa ni nini?.

Serikali i-deal na latent consequences, intended and un intended consequences katika hili la Panya road. La sivyo watakuwa wengi na kuja kuwazidi wana usalama wetu ambao kimsingi ni wachache sana.

Kwa waliosoma Physics wana concept fulani katika Hooke's Law. Elastic material ikishavuka elasticity, basi inaingia katika second stage iitwayo deformation ambako huwa haiwezi kurudi tena katika original shape.

Panya road watavuka Elastic limit. Wakiingia kwenye Deformation point hakuna atakayebaki salama.

Samaki mkunje angali mbichi. Tuwakunje Panya road still mapema.

Hekima Ni Uhuru.
 
Mbona huku mikoani hakuna ndugu? Huku hata ukiiba karanga tunachoma moto.
Watu wanaiba mchana mchana halafu people zinawaangalia tu.
Wanaume wa dar tabu tupu. Huku mkoani makundi ya ovyo ovyo hayapo
Huku mikoani tunafundishana kufanya kazi huko dar wanafundisha uvivu na umbeya sasa njaa ikiwakolea wanawatuma watoto wao wakapole watu
 
kwa mitaa ile watashugulikiwa fasta kwasababu wako kalibu na mitaa ya kitengo na wadau wa kitengo huwa wanakunywa mitaa iyo iyo
 
Nielekezeni waliko nikawafundishe adabu maana nina mbinu zote za mgambo, jeshi na kipolis
Vibaka wadogo kama hao hawanibabaishi.
 
Mzee wa jiji hili Makonda si yupo? Ninaamini atawamudu.
Haya mambo wananchi wanapaswa kuyamaliza wenyew na wasingoje jeshi la polisi.
Huku mwanza tunawashugulikiwa wenyew. Polisi wakija wanakuta majivu tu. Kuna dogo mtaani kwetu alikuwa na hiyo tabia ya wizi. Wakamuwekea mtego yy na wenzake. Mtego ukanasa bahati nzuri mtaani ulikuwa unamjua lkn alichezea kichapo na wenzake. Hicho kipigo zaid ya mbwa mwizi. Na jera akaenda.
Sasa hivi ni kijana mzuri tu anashika na jembe. Anatafuta pesa kwa jasho lake
 
Nielekezeni waliko nikawafundishe adabu maana nina mbinu zote za mgambo, jeshi na kipolis
Vibaka wadogo kama hao hawanibabaishi.
Kwa wanaume wa dar hawakupi support yyte. Utapambana pekee yako. Na cha ajabu usishangae wakaanza kukupiga picha warushe kwenye account zao za facebook, jamii forum, whatsapp na insta
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom