Tahadhari: Usajili wa line za simu kwa alama za vidole

Kama ndio hivyo zoezi la kusajiri laini kwa alama za vidole linakuwa limefeli kabisa na linakuwa halina maana zaidi wanakuwa wamesumbua tu wananchi.

........Kabla walisema mtu mmoja hawezi sajiri laini zaidi ya mbili kwa mtandao mmoja isipokuwa kwasababu maalumu, Leo inakuwaje mitandao inaruhusu uhuni kama huo ufanyike?
 
Kwanza kabisa naungana na wewe kiasi lakini:

Je wajua tabu na shida wanazopata mawakala?
Je wajua malipo wanayolipwa mawakala?
Je wajua vijana wengi wamejiajiri kwa hii kazi?

Kabla hujawahukumu jaribu kuwatetea mawakala wa mitandao, wanafanya kazi ngumu na kubwa malipo madogo, kiujumla mitandao inawanyonya, serikali, Tra na tcra wanawakandamiza mawakala..
Kila lawama anapewa wakala, wakati huo hamjawahi kuuliza au kuwasemea.
Wanaonekana ni wezi, vibaka na wazululaji.
Lakini hawa ndiyo mitandao inawategemea kukuza na kuua soko la mwingine, lakini hawathaminiwi...

Waache watafute Ridhiki kwa njia yoyote hile, ni haki yao.

Mawakala Hawathaminiwi
 
Hicho kitu akiwezekani mkuu, uwezi kusajili kwa kutumia kitambulisho cha MTU kama auna hata kidole kimoja cha muhusika, alama ya kidole utacho sajilia laini lazima iwiane na zile zilizowekwa NIDA kwa kitambulisho husika
 
Hicho kitu akiwezekani mkuu, uwezi kusajili kwa kutumia kitambulisho cha MTU kama auna hata kidole kimoja cha muhusika, alama ya kidole utacho sajilia laini lazima iwiane na zile zilizowekwa NIDA kwa kitambulisho husika
Vipi kwa mtu ambaye hakuweka finger prints wakati anajisajili nida?????
 
Wewe Ni mpumbavuuuu, tena ungekuwa jirani ningekukata vibao namba ya NIDA hata ukiwanayo haina faida Kama huna fingerprint za muhusika sasa hapo unaweka matak** yako ama nini... Acha upumbavu wew kudanganya watu
 
Kama unahisi kuna ujanja umetumika na kitambulisho chako kimetumika kusajili laini ambazo hizifahamu

Nenda kituo cha huduma kwa wateja uangalie namba zilizo sajiliwa kwa kitambulisho chako bila ya wewe kujua utaziona zote hata kama zipo 10 kisha zifunge ambazo huzihitaji au ziswap uzichukue maana hizo zote ni mali yako
 
Mtoa post mbumbumbu kwel kwel nataka niseme kinachowezekana apo ni kusajiliwa laini ya jina la mtu mwingine, isiyo verified kwa NiDA pekee ndo mawakala wanaweza ila lain iliyoverified kabisa na NiDa haiwezekan labda awe ameverfy mwenyewe kwa fingerprnt,.
 
Jensen salamone,
Utakuwa ni uzembe mkubwa endapo mawakala waliopewa kazi hiyo kuachwa bila utambulisho wa laini watakazozisajili. Kuwekwe kumbukumbu za msajili na laini zote alizozisajili ili itakapotokea kuna tukio la kiarifu wakala ahusishwe moja kwa moja.
 
Kinga ni bora kuliko tiba, iwe kweli au sio kweli mtoa uzi maneno yako sio ya kupuuzwa hata kidogo
 
Mimi najua kuwa fingerprint zinaenda sambamba na namba za NIDA, zikioana basi mfumo utakukubalia kusajili line.
Kama hawajaseti hivyo basi wamekosea sana
 
Back
Top Bottom