Tahadhari: Usajili wa line za simu kwa alama za vidole

Kama unahisi kuna ujanja umetumika na kitambulisho chako kimetumika kusajili laini ambazo hizifahamu

Nenda kituo cha huduma kwa wateja uangalie namba zilizo sajiliwa kwa kitambulisho chako bila ya wewe kujua utaziona zote hata kama zipo 10 kisha zifunge ambazo huzihitaji au ziswap uzichukue maana hizo zote ni mali yako
Nitapita katika brunches zao kukagua waliosajiliwa kwa kutumia kitambulisho changu nikizikuta zina mpunga wa maana watajuta kuzaliwa
Naenda polisi nachukua RB kuwa nimeibiwa simu kisha naenda kuziswap kweli bongo fursa zipo nyingi ila hatujui kuzitumia
 
Uzushi tu

Namba ya NIDA ipo connected na Fingerprint ya muhusika

Ingekuwa hivo watu wengi wangejisajiri kwa namba za Watu wengine
Mkuu kila jambo linawezekana. Nadhani kinachofanyika

1).unasajili SIM card yako then unaambiwa system imekataa

2).unasajili SIM card nyengine unaambiwa tayari

3).unaondoka na moja unaacha moja

4). MTU akija anainunua ikiwa imesajiliwa anaenda kutumia.

5).ulimwengu wa sayansi na Technologia kilichoshindikana ni kuumba nafsi ya BINADAMU.
Mamtu yanatengeneza karatasi zinasoma kwenye account.

Note; Anayefanya usajili ndiye mjazaji wa Taarifa, wewe unatoa no. Ya kitambulisho na finger print kusajili namba nyengine.

Inabidi tukubaliane na msemo kuwa tushatumia 10% ya Brain zetu.
 
Mtoa mada acha nikusahihishe kidogo.
Iko hivi wakala akiwa ana namba yako ya nida hawezi kusajiri laini nyingine kwa sababu itahitajika iwe connected na fingerprnt..
Utapeli na ujanja wa mawaka uko hivi.
Unapotoa namba ya NIDA au kitambulisho chako utakapomtajia namba yako ya simu utaweka dole gumba lako na kukamilisha kisha atakwambia tena rudia tena, kwahiyo pale unaporudia kuweka fingerprnt tambua kuwa anakamilisha usajiri wa laini nyingine tena kwahyo kitambulisho chako kimoja kinaweza kukamilisha laini hata tatu kwa mpigo bila wewe kujua...

Tatizo liko kwa mitandao ya simu kuruhusu kitambulisho kimoja kukamilisha laini zaidi ya moja ya mtandao mmoja.
Wao wataka pesa ukinunua lain unatumia kuwasiliana. Na unapowasiliana ndo wanaingiza pesa.
 
Hahaaa !! In a darkest circumstance there is a bright side if you have a courage to look into it.
Nitapita katika brunches zao kukagua waliosajiliwa kwa kutumia kitambulisho changu nikizikuta zina mpunga wa maana watajuta kuzaliwa
Naenda polisi nachukua RB kuwa nimeibiwa simu kisha naenda kuziswap kweli bongo fursa zipo nyingi ila hatujui kuzitumia
 
Nipe namba yako ya Nida uone kama siwezi kusajilia simu.

Unaamini finger print hii hii ambayo mwingine anaweka dole gumba, mwingine chanda, mwingine kidole cha kati na mwingine kidole cha mwisho?
Mkuu chutama tu, umeingia chaka.

Unachosema hakiwezekani hata akirudi Masihi.
 
Hii haya inajibu swali lako either umeiruka au umesoma lakini hujaelewa. Nimekusogezea karibu uisome tena

"Sasa ikitokea hivyo na ametumia namba ya kitambulisho chako wakitrack namba za hiyo laini taarifa zitakazo onekana ni za kwako japo finger prints zitakuwa za mtu mwingine mpaka hapo wewe utakuwa mtuhumiwa wa kwanza kwa hiyo hata upepelezi/uchunguzi ukiwa unaendelea wewe utakuwa tayari unasota rumande kwa kosa ambalo si la kwako"
Rudi shule mkuu.
 
Mtoa mada acha nikusahihishe kidogo.
Iko hivi wakala akiwa ana namba yako ya nida hawezi kusajiri laini nyingine kwa sababu itahitajika iwe connected na fingerprnt..
Utapeli na ujanja wa mawaka uko hivi.
Unapotoa namba ya NIDA au kitambulisho chako utakapomtajia namba yako ya simu utaweka dole gumba lako na kukamilisha kisha atakwambia tena rudia tena, kwahiyo pale unaporudia kuweka fingerprnt tambua kuwa anakamilisha usajiri wa laini nyingine tena kwahyo kitambulisho chako kimoja kinaweza kukamilisha laini hata tatu kwa mpigo bila wewe kujua...

Tatizo liko kwa mitandao ya simu kuruhusu kitambulisho kimoja kukamilisha laini zaidi ya moja ya mtandao mmoja.
Asipokuelewa hii basi tena
 
Nipe namba yako ya Nida uone kama siwezi kusajilia simu.

Unaamini finger print hii hii ambayo mwingine anaweka dole gumba, mwingine chanda, mwingine kidole cha kati na mwingine kidole cha mwisho?
ACHA UONGO .Ukiweka dole inatokea hadi picha yako uliyosajili nida dole likiwa tofauti haikubali.Uongo wenu wa kudanganyana vijiwe vya kunywa gongo baki nao mwenyewe
 
Ni mara ya pili kulisikia hii tahadhari wahusika tunaomba mfuatilie kama kuna hoyo loophole kwenye system. Ingawa kama system inaaweza kuruhusu namba moja kusajiliwa kwa alama za vidole zaidi ya mara moja itakuwa system ya kipuuzi kabisa. TCRA wa synchronize system zao na NIDA ili sisi tupeleke namba na majina tu alama za vidole wazikute hukohuko kwenye system za NIDA.
 
Mtoa mada acha nikusahihishe kidogo.
Iko hivi wakala akiwa ana namba yako ya nida hawezi kusajiri laini nyingine kwa sababu itahitajika iwe connected na fingerprnt..
Utapeli na ujanja wa mawaka uko hivi.
Unapotoa namba ya NIDA au kitambulisho chako utakapomtajia namba yako ya simu utaweka dole gumba lako na kukamilisha kisha atakwambia tena rudia tena, kwahiyo pale unaporudia kuweka fingerprnt tambua kuwa anakamilisha usajiri wa laini nyingine tena kwahyo kitambulisho chako kimoja kinaweza kukamilisha laini hata tatu kwa mpigo bila wewe kujua...

Tatizo liko kwa mitandao ya simu kuruhusu kitambulisho kimoja kukamilisha laini zaidi ya moja ya mtandao mmoja.
Hii inaingia akilini .
 
Kama ndio hivyo zoezi la kusajiri laini kwa alama za vidole linakuwa limefeli kabisa na linakuwa halina maana zaidi wanakuwa wamesumbua tu wananchi.

........Kabla walisema mtu mmoja hawezi sajiri laini zaidi ya mbili kwa mtandao mmoja isipokuwa kwasababu maalumu, Leo inakuwaje mitandao inaruhusu uhuni kama huo ufanyike?
acha kumsikiliza huyo mjinga mleta mada.System ya NIDA ni kama ya passport ukigonga dole zinatokea details zako zote na picha.Huyo mleta maada mpumbavu mjinga na bwege .Dole la mtu mwingine haliwezi kubali kusajili laini kwa kutumia kitambulisho cha mtu mwingine.MLETA mada ni wale wajinga wa vijiweni wasioelewa kinachoendelea duniani
 
Back
Top Bottom