Tahadhari namba hii ya simu 0746 435 352

Tahadhari namba hii ya simu 0746 435 352

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,896
Reaction score
15,124
Namba 0746435352 baada ya kuchunguza inamilikiwa na SIKUJUA NDEMEZI.

Kuna sauti ya mwanaume mnamo saa 10.45 mchana ilipigwa kwa mke wangu, ati

"hapa ni Voda simu namba yako imeshinda ya zawadi Tshs 200,000 na simu ya Techno."

Nimerudi nyumbani mamsap mwenye furaha tele!
Mara moja nikamwambia utapeli huo.
Sasa hivi simu hii haipatikani hewani.

Inaweza kuwa simu imeibiwa na inatumika kutapeli.
Ni vema huyu Sikujua akawahi kutoa taarifa mahali salama.
 
Aisee..watu noma, voda tangu lini wameanza hiyo ishu
 
Wako wengi sana mchezo wa kawaida huo...

Kuna mwenzao mmoja alinipigia simu juzi akaniuliza wewe ni fulani nikamjibu ndio

Akajitambulisha, mimi fulani bin fulani napiga simu toka Vodacom makao makuu.

Nikajibu, ehee..!

Akaniuliza namba yako ndio hii....nikajibu ndio.

Akaniambia umeshinda bahati nasibu toka Vodacom...

Nikajibu....eheee!

Akaniuliza....hivi upo mkoa gani.?

Nikamwambia ....acha uzuzu yaani wewe upo makao makuu Vodacom halafu hajui mimi niko mkoa wala....

Kabla sijamaliza nikasikia simu ti!titi! ....sikumpata tena hewani.
 
Mie kuna hii no. 0787 730 300 walinikurupua asubuhi asubuhi najua simu ya maana eti nimeshinda nikamshushua akatkata simu iweje nitumie voda halafu nipigiwe kutumia airtel hapa naziorodhesha , vyuma vinabana kila mbinu wanatumia
 
Hali imekuwa ngumu ndio maana kila mtu anapambana na hali yake kwa namna yake
 
Kuna jamaa alinipigia ananiambia ule mzigo wa nguvu za kiume umewasili! Nikamshushua Nikamwambia mimi sio mtamba,
 
Back
Top Bottom