Tahadhari: Lifts(Elevators) zinaweza kuua!

Hahaaa hii hali Mimi ilinikuta lakini sijawai fikiria kuacha tumia elevator

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka fulani nikiwa nasoma Law School pale Mawasiliano nikiwa na rafiki yangu na mtu mwingine, jumla watatu..tukapanda lift ya jengo mojawapo..

Sisi tulikuwa tunaenda ghorofa ya 3 ambako ndiyo mwisho wa lift...sasa ikafika floor ya pili ikasimama, akashuka jamaa mmoja tukabaki mimi na rafiki yangu.

Hapo ndipo kizazaa kikaanza. Ikaenda mpaka floor ya 3, ila ikagoma kufungua mlango. Ikaanza mchezo wa kupanda na kushuka ground floor.
Ikafika wakati, zile taa za kuonesha umefika floor ipi zikazima...inapanda juu, ikifika haifunguki, inashuka chini, inapanda tena.
Tukajaribu kupiga simu, hazitoki, jaribu ku shout sauti haitoki.

Nikawa naona kabisa kuwa tunafia mle ndani. Tulikaa almost 6 to 7 minutes. Kijasho chembamba cha panick kimeshaanza kutoka.

Baadaye ikapanda tena hadi floor ya tatu, milango ikaanza kufunguka very slowly, upenyo ulipopatikana tu, tukatoka.

From that day, ile experience imebaki kichwani mpaka leo. Na sikupanda tena zile lift za pale chuoni. Na kila nikienda mahala pengine kabla ya kutumia lift, ile kumbukumbu hunijia.
 
Cajojo hiyo experience uisikie tu kwa mwingine ni hatari sana
Hyo experience ninayo mkuu ilinikuta nikiwa na husband na mtt wetu mdogo wa miezi 7. Lilikua tukio la dkk chache but lilinipa hofu ambayo sitakaa nisahau nawaza mtt wangu atakavyoanza kukosa hewa jamani Mungu mkubwa tulipojaribu kubonya kitufe ilifunguka. Ndo maaana nasema nimesisimkwa maana nikikumbuka najisikia vibaya
 
Halafu sehemu nyingine lift zinajaa balaa! Kama lile jengo la RITA pale karibu na Bilicanas. Unaomba Mungu lisitokee jambo baya maana inabidi hiyo rescue action isichelewe hata kwa dakika moja amasivyo itakua balaa kwa watu wanavyojazana
Kuna jaa plus joto ushuzi basi tafrani. Hapo round hawachukui wenye mioyo midogo kama mie tunaanza safr ya kwenda kwa baba kwa kuzimia kwanza
 
Imagine unaenda gorofa ya 10 si mlima huo [emoji26][emoji26][emoji26]
Hapo napo maamuzi yake magumu maana huna jinsi
Halafu taa ikizima ikawaka tena unaanza kukumbuka Sala zote
Kwa kweli ni hatari maana hata likitokea la kutokea unakuta mhudumu anapiga soga nje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo ndio standards tunataka ziwekwe na serikali kwa wenye majengo yote wanaopaswa kuweka lift
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…