Tahadhari kwa wauza simu wenzangu

Tahadhari kwa wauza simu wenzangu

Vieloon

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2012
Posts
1,520
Reaction score
695
Kama wewe ni Muuzaji wa simu au Tablets. Ukaweka tangazo lako humu JF au Kupatana, au kokote kule...Harafu akatokea mteja akakuomba umtumie IMEI namba ya simu yako ili aweze kuangalia km haitafungiwa na TCRA au km ni original kweli. Mwogope, Kimbia...

Au mueleweshe kwamba km anahitaji kweli mkutane then kabla ya kufanya biashara au kukukabidhi hela atakagua na kuangalia IMEI number mbele yako ajiridhishe kwanza km simu ni Original ndio mfanye biashara.

Kumpa mtu usiyemjua IMEi # ya simu yako kabla hamjafanya biashara ni sawa na kufanya mtu ajue namba za hela zako zilizo kwenye wallet yako.

Kuna "matapeli" huwa ukiwapa IMEI namba, wanadai Simu ni yao/zao...wengine wanashirikiana hadi na Police kudai cm hiyo/ hizo ziliibiwa na uthibisho wao unakuwa ni hiyo IMEI namba uliyompa. Utaitwa mwizi, Utachukuliwa simu na hela utatoa.

Na inaweza isikukute wewe ila wakasubili kwa kipind flani yakaja kumkuta hata mteja uliyemuuzia hiyo cm baadae.

# BIASHARA NJEMA...Maisha yaendelee

Msisahau kunicheki for the best original smartphones # 0654776976
 
Back
Top Bottom