TAHADHARI kwa wana ChitChat wote...

Status
Not open for further replies.

salim2013

Member
Joined
Apr 3, 2013
Messages
27
Points
45

salim2013

Member
Joined Apr 3, 2013
27 45
Kila jukwaa lina watu ambao wanakuwa ni members ‘zaidi ya wengine’ tokana na mapenzi ya kila member. Katika majukwaa yote hili la CC limekithiri tabia za uchochezi na undumilakuwili kwa members husika. Member anakuwa na ID zaidi ya moja kwa malengo ya kuchezea akili za members wenzie wa hili Jukwaa.

TAHADHARI:

Kwa member yeyote mwenye ID zaidi ya moja na zote akataka kuzitumia ChitChat kwa kutaka kuwa nazo active kwa sababu zozote zile, hizo IDs zitaunganishwa mara moja!

Kwa mwanachama yeyote yule atakayehisi kuna member ana ID zaidi ya moja kwa lengo la kuwavuruga, TAFADHALI taarifa itolewe mara moja kwa njia ya kubofya kitufe cha “Report Abuse” ama kwa PM kwenda kwa Invisible ama Moderator ama wote. Epuka kuvunja sheria kwa kufanya name calling kwenye thread husika, utafungiwa pasipo sababu!

ChitChat imekuwa ikitumika kama njia ya kutafuta wachumba, kuunganisha marafiki, na kukuza ujamaa kati ya baadhi ya members. Na hapohapo imekuwa ikitumika vibaya na baadhi ya waharibifu; kubeza, kejeli, sanifu na kuchezea akili za watu. Hili hatutalivumilia, lengo letu kuwaanzishia uwanja huu halikuwa kuwavuruga!

Zoezi la kufuta huo usanii wa kuwa na ID zaidi ya moja kwa ajili ya kujikosha na nyingine kwa ajili ya kuponda na kusababisha ukosefu wa amani limeshaanza kufanywa mara moja na baadhi ya IDs zimekuwa merged.

Wana ChitChat, hili jukwaa linaweza kuonekana ni sehemu ya mzaha na lisilo na tija! Hii sio sahihi. Kila mahala katika jamii panahitaji sehemu ambayo ni ‘Stress free zone’ kama ilivyokuwa awali na kama itakavyokuwa kuanzia sasa ambapo lipo na uangalizi wa karibu. Tutajiepusha na ban lakini itapobidi, tutatembeza ban kwakuwa tutakuwa tumelazimika!

Ni muhimu, mtambue kuwa tunaheshimu privacy zenu na iwapo mkapata threats au PM za kutilia mashaka wasisite ku-report kwetu nasi tutachukua hatua haraka sana. EPUKA ku-paste PM ya mtu katika public forums, itakuzawadia ban kwakuwa ni nje ya sheria za JF!

NOTE: Hakuna moderator hata mmoja anayeweza kujigamba, kupiga mkwara kupitia PM wala kukupigia simu kukutishia kwa namna yoyote ile, mods wetu wamefunzwa uvumilivu na kuheshimu privacy za watu na hivyo yeyote atayekuja kwako akijigamba kuwa moderator wa JF tafadhali tufahamishe mara moja!

Nawatakia Chit Chatting njema…
mwenye user zaid ya moja dawa ni kuban zote mbili
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,380,704
Members 525,857
Posts 33,777,397
Top