Tahadhari kwa wale wanaolipwa kuzomea

Tahadhari kwa wale wanaolipwa kuzomea

Mudawote

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2013
Posts
11,569
Reaction score
16,017
Ni vema wanaolipwa na kujipanga barabarani kuzomea au kupiga deki wajiandae maana na vijana wa ccm wakiamua kulipiza kisasi patakuwa hapatoshi. Tufanye siasa za kistaraabu kwani hata ccm siasa za rafu tunazijua.
 
Ni vema wanaolipwa na kujipanga barabarani kuzomea au kuoiga deki wajiandae maana na vijana wa ccm wakiamua kulipiza kisasi patakuwa hapatoshi. Tufanye siasa za kistaraabu kwani hata ccm siasa za rafu tunazijua.

Hakuna anelipwa kuzomea.na sidhani kama ni vijana wa UKAWA tu nadhani hata vijana wa CCM wanaojielewa pia kwa kua wamechoka na uozo wa utawala wa miaka 50...tatizo ninyi mpo wachache sana hamtaweza kufanya hivyo.
 
Kwanza tuweke kumbukumbu sawa' ccm hakuna vijana wote ni wazee. Ukimwona kijana yupo ccm ujue ana matatizo. Alafu wanaowazomea ccm siyo ukawa ni wananchi wa kawaida wenye maisha magumu kutokana na ubovu wa ccm ----- wewe.
 
Ni vema wanaolipwa na kujipanga barabarani kuzomea au kuoiga deki wajiandae maana na vijana wa ccm wakiamua kulipiza kisasi patakuwa hapatoshi. Tufanye siasa za kistaraabu kwani hata ccm siasa za rafu tunazijua.

Daaaahh bro unaongea kwa huruma na unyonge mpaka nimekuhurumia. Pole bro ndio dunia.. Usiuweke moyo wako wote kwenye siasa utakuja kufa kwa presha
 
Nakumbuka hata mwigulu aliisha wahi izungumzia hii ishu,kuwa wako fiti wanaweza kujibu mashambulizi wakiamua:-D:-D

Sjui wanasubiri nini???
 
Ni vema wanaolipwa na kujipanga barabarani kuzomea au kupiga deki wajiandae maana na vijana wa ccm wakiamua kulipiza kisasi patakuwa hapatoshi. Tufanye siasa za kistaraabu kwani hata ccm siasa za rafu tunazijua.

ccm haina vijana, ina mapoyoyo waganga-njaa
 
Hivi CCM ina vijana?

Kina Shigella na Le Mutuz ni vijana?
 
Ni vema wanaolipwa na kujipanga barabarani kuzomea au kupiga deki wajiandae maana na vijana wa ccm wakiamua kulipiza kisasi patakuwa hapatoshi. Tufanye siasa za kistaraabu kwani hata ccm siasa za rafu tunazijua.
Kuzomea au kushangilia kwenye mikutano huwa kunatokea automatically bila kuwapanga watu. Ukiwa kwenye mkutano wa mwanasiasa anayevutIa na kupendeka kama Lowassa halafu ukijifanya hamnazo na kuanza kuzomea unaweza kujikuta kwenye hali mbaya sana! Na CCM wanalijua hili na ndio maana hakuna mtu anayekubali kulipwa fedha ili azomee kwenye mikutano ya UKAWA kwani makubwa yanaweza kumfika.
 
Nakumbuka hata mwigulu aliisha wahi izungumzia hii ishu,kuwa wako fiti wanaweza kujibu mashambulizi wakiamua:-D:-D

Sjui wanasubiri nini???
Hahaaaa! Wanajua tu kuzomea bungeni!
 
Hakuna anelipwa kuzomea.na sidhani kama ni vijana wa UKAWA tu nadhani hata vijana wa CCM wanaojielewa pia kwa kua wamechoka na uozo wa utawala wa miaka 50...tatizo ninyi mpo wachache sana hamtaweza kufanya hivyo.

Umewahesabu lini ukajua vijana wa ccm ni wachache na hawawezi kufanya lolote,? msijaribu kuvuruga amani kwa kisingizio eti mpo wengi.
 
mie nililipwa 20,000= kuvaa t - shirt ya ccm !!!Leo nimetandika mlango wa kuingilia chooni kila mtu anaikanyaga
 
Aliewaambia kuwa ni wapumbavu hakukosea

Kapimwe akiri unaweza kuwa hazimo au mke wa mwenyekiti wewe unaangalia maslahi ya mme wako badala ya maslahi mapana ya Taifa.

swissme
 
Ni vema wanaolipwa na kujipanga barabarani kuzomea au kupiga deki wajiandae maana na vijana wa ccm wakiamua kulipiza kisasi patakuwa hapatoshi. Tufanye siasa za kistaraabu kwani hata ccm siasa za rafu tunazijua.
yaache yanajifanya yanajua.sisi sa hvi tunapiga kura tu kunyamazisha hawa malofa
 
Ni vema wanaolipwa na kujipanga barabarani kuzomea au kupiga deki wajiandae maana na vijana wa ccm wakiamua kulipiza kisasi patakuwa hapatoshi. Tufanye siasa za kistaraabu kwani hata ccm siasa za rafu tunazijua.

Kada wa CCM, Fatuma Isaka anayedaiwa kugongwa na gari kwenye vurugu zilizotokea juzi baada ya wafuasi wa chama hicho kuvamia mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chadema, Juma Duni Haji, amefariki dunia.Tukio hilo lilitokea saa tisa alasiri katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chang'ombe A kabla ya Duni kuwasili kuhutubia mkutano wa kampeni.Inadaiwa Fatuma aligongwa na gari la CCM baada ya kuteleza wakati likiondoka kwenye uwanja huo.Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Jenifa John alisema wakiwa katika viwanja hivyo, walifika makada sita wa CCM na kuwaamuru wanachama wa Chadema kuondoka kwa madai kuwa ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ilionyesha hawakupangiwa kufanya mkutano kwenye eneo hilo kwa siku hiyo."Walituambia Serikali ni yao na shule ni yao, kwa hiyo hakuna chama chochote kinachoweza kuwazuia kufanya kampeni mahali hapo na kututaka tuondoke," alidai Jenifa.Alisema baada ya mabishano hayo, makada hao wa CCM waliokuwa na gari, waliamua kuondoka.Alisema wakati gari linaondoka, kada mmoja wa chama hicho (hakumtaja jina) alikuwa hajapanda, hivyo alivyokuwa akitaka kulirukia kwa bahati mbaya aliteleza, akaanguka na kukanyagwa na magurudumu ya nyuma."Wenzake waliondoka na kumuacha majeruhi huyo akiwa chini. Wakazi wa eneo hili walikodi gari na kumpeleka hospitali," alidai Jenifa.<Akizungumzia tukio hilo, Katibu wa Chadema Mkoa wa Dodoma, Kennedy Kimario alisema CCM ilifanya makusudi kuvamia mkutano huo. "Walifanya fujo bila sababu, walikuwa wanajua kuwa anapokuja mgombea urais au mgombea mwenza kisheria mikutano yote midogo ya kampeni inapaswa kusimama," alisema Kimario.Katibu Msaidizi wa CCM Mkoa wa Dodoma, Othman Dunga alivilaumu vyombo vya dola kwa madai kuwa vilishindwa kuchukua hatua mapema. "Sisi tulikuwa na barua halali kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi ya kufanya mkutano mahali hapo, lakini walipokuja polisi waliwaruhusu Chadema waendelee na mkutano wao wa kampeni," alidai Dunga.Hata hivyo, Dunga alidai kuwa kada huyo aligongwa na gari la Chadema na kuchomwa mwilini na vitu vyenye ncha kali.Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Mnyambuga alithibitisha kutokea kwa mgongano wa ratiba kati ya vyama hivyo na kumalizwa na msimamizi wa uchaguzi wa Manispaa ya Dodoma Mjini."Ratiba ilileta shida baada ya kufanyiwa marekebisho kwa sababu siku hiyo aliyekuwa ahutubie mkutano ule wa kampeni alikuwa mgombea mwenza wa Chadema, kwa mujibu wa utaratibu, ililazimu kupangua ratiba suala hilo lilimalizwa na mkurugenzi ambaye ni msimamizi wa Uchaguzi wa Manispaa ya Dodoma Mjini)," alisema.
 
Back
Top Bottom