Tahadhari kwa kinababa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahadhari kwa kinababa

Discussion in 'JF Doctor' started by Mahesabu, Apr 22, 2011.

 1. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Sigara wavutazo ndizo zinazoua watoto wao
  * Watafiti: Mimba ni mbalimbali na sigara
  NA PETER ORWA
  WATU wengi wanapenda kuvuta sigara. Lakini, si wote wanaojua kwamba athari hizo haziishii kwa mvutaji tu, bali hata wahusika wengine wa karibuni kama watoto, kuanzia maisha yao wakiwa tumboni.
  Inaelezwa kitaalamu kwamba, wanaume wanaovuta sigara wanahatarisha maisha ya watoto wao ambao hawajazaliwa.Tayari nchini Uingereza, imeshabainika kwamba maisha ya kuvuta sigara katika makazi ya ghorofa yameshaua watoto 600,000 na wito umetolewa kwa jamii kuachana na tabia hiyo kwani inahatarisha maisha ya watoto.Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Nottingham wamegundua kwamba uvutaji katika mazingira ya wajawazito walipo iwe kazini au majumbani inaongeza hatari juu ya hatima ya maisha ya watoto walio tumboni kwa asilimia 23 na madhara mengine ya mtoto kwa asimilia 13.
  Utafiti huo ulifanyika kwa mizunguko 19 katika sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Marekani ya Kusini na Kaskazini, Bara Asia na Ulaya.Huko nyuma zilishafanyika utafiti wa namna mbalimbali kwamba wanawake wanaovuta sigara ndio wanaohatarisha zaidi afya ya vijana wao.Mtaalamu bingwa, Profesa Andrew Shennan wa Hospitali ya Mtakatifu Thomas ya London, Uingereza anasema:"Ni muhimu kwamba wanawake wafahamu hatari zinazohusiana na kuhusishwa sigara anazovuta mwingine na kuwapa tahadhari juu ya hatari ya afya kwa watoto watakaozaliwa.”Anasema kemikali iliyoko katika sigara inajulikana katika kuongeza madhara makubwa kwa mimba.
  Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO), ni kwamba theluthi moja ya watoto wanaokufa ni kutokana na sababu zinazoanzia katika uvutaji wa sigara.Uchunguzi uliofanywa katika nchi 192 umegundua kwamba, uvutaji sigara wa mtu mwingine mathalan baba una madhara kwa afya ya mtoto ikiwemo kifo, homa ya mapafu na pumu, athari za moyo, kansa na mfumo wa kupumua.
  WHO inasema kwamba, katika ubashiri wao wa kitaalamu ni kwamba, kuna jumla ya watoto 165,000 wanaokufa kutokana na athari za sigara katika bara Afrika, Asia ya Kusini na Mashariki.Mfumo wa madhara yao kiafya unaendana na kuwepo aina ya matatizo ya yatokanayo na mfumo wa maradhi ya kuambukizwa pamoja na moshi wa sigara kutoka kwa watu wa karibu.Kwa mfano, takwimu za mwaka 2004 zonaonyesha vifo vitokanavyo na madhara hayo, watoto 379,000 ni kwa matatizo ya moyo; watoto 165,000 ni kutokana mfumo wa kupumua; watoto 36,900 ni wa pumu; na kansa ya mapafu ni watoto 21,400.Duniani kote kunakadiriwa wapo wavuta sigara bilioni 1.2 ambao starehe yao imeweka rehani afya ya watu wengine, ambapo mbali na watoto, wanawake wanaelezwa wako katika hatari kubwa ya kudhurika, kulinganisha na wanaume.
  Karen Wilson, Profesa Mshiriki katika Kituo cha Afya cha Chuo Kikuu cha Rochester, anashauri:“Wazazi wanatakiwa wajitume hasa kunausuru watoto wao kutoka katika hatari kama vile matumizi ya tumbaku.
  “Inashangaza sana kuona matokeo haya na kuona kwamba wazazi wanawaacha watoto wao wadhurike na sigara hii inavyovutwa na mtu mwingine majumbani kwao."
  Katika nchi nyingi kuna hatua nyingi zimeshachukuliwa kudhibiti matumizi ya sigara ikiwemo nchi za Afrika Mashariki.
  Nchini Tanzania, uvutaji wa sigara katika sehemu za hadhara ulipingwa tangu mwaka 2003 ikiwemo katika vyombo vya usafiri vya umma, shuleni na hospitalini.
  Hiyo inaendana na kupiga marufu mauzo ya bidhaa za tumbaku watu wote chini ya miaka 18, huku mtangazo yote ya biashara kuhusu bidhaa ya tumbaku yahusishe tahadhari ya madhara yake.
  Nchini Kenya, kuna hatua zilizochukuliwa kudhibiti uvutaji wa sigara katika mji mkuu wa Nairobi na miji ya Mombasa na Nakuru.
  Marufuku hiyo inagusa maeneo ya umma kama vile viwanja vya ndege, viwanja vya michezo. Baa na migahawa kwa mujibu wa sheria hiyo zimeagizwa kuwa na sehemu tofauti za watu kuvuta sigara.
  Sheria inatamka mtu akipatikana na hatia ya kuivunja, atakabiliwa na faini ya sh. 50,000 ya Kenya ambayo ni sawa na zaidi ya sh. 500,000 ya Tanzania au kifungo cha miezi sita au adhabu zote mbili zinaenda kwa pamoja.
  Nchini Kenya, sigara inasababisha vifo vya watu 8,000 kila mwaka na inaelezwa idadi ya wanaokufa kutokana na madhara ya moshi ya mvutaji mwingine ni watu 4,000.
  Kwa maana hiyo, sigara ina madhara makubwa ambayo kuyakabili inahitaji tafsiri pana.
   
Loading...