Tahadhari kuhusu propaganda chafu

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
Posted by John Mnyika | May 13, 2012

WanaJF wenzangu, katika kipindi cha kati ya 2011 mpaka 2012 kuna mwelekeo ambao naona ni vyema kila unapoibuka mkauchukulia kwa tahadhari. Kwa nyakati mbalimbali kila ninaposhughulikia masuala ya kitaifa yenye kuwagusa baadhi ya watu ndani ya serikali au CCM huanza vita vya mtandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhoji kuhusu utendaji kazi wangu jimboni sanjari na utekelezaji wa ahadi za kampeni.

Watu hawa hawahoji ahadi za Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM alizozitoa jimboni Ubungo mwaka 2005 na zingine zaidi akazitoa 2010; natambua kuwa wanao uhuru wa kuacha kuhoji ahadi hizo kwa sababu wanazozijua wao na kuhoji ahadi zangu nilizoahidi za kuwawakilisha wananchi, kuisimamia serikali na kushiriki kikimilifu katika kutunga sheria zote zikiwa na lengo la kuwezesha maendeleo.

Hata hivyo katika kutumia uhuru wao huo wa kikatiba ni vizuri pia wakatimiza wajibu wa kufuatilia utekelezaji tunaousimamia kwa kuzingatia kuwa toka nichaguliwe nimekuwa na kawaida ya kutoa mrejesho wa hatua kwa hatua wa kazi ambazo nazifanya za kuwatumikia wananchi jimboni, hivyo ni vizuri rejea ikafanyika katika taarifa hizo na kama kuna maswali ya ziada nipo tayari kuyajibu kwa kila nitakapopata wasaa.

Kwa ajili ya urahisi wa rejea na kutokana na maswali ambayo hujirudia kwa masuala ambayo tayari yameshatekelezwa na nimeshayatolea ufafanuzi kwa nyakati mbalimbali, nafanya utaratibu ili mwaka wa fedha 2011/2012 utakapoisha niweke utekelezaji wote kwenye ripoti moja ya mwaka iwe rahisi kwa rejea. Kwa sasa mnaweza kutembelea http://mnyika.blogspot.com (JOHN MNYIKA) upo mrejesho wa utekelezaji hatua kwa hatua kuhusu namna nilivyotimiza wajibu wa kuisimamia serikali katika kuwezesha maendeleo jimboni, mafanikio tuliyopata mpaka sasa, changamoto tunazokumbana nazo na namna tunavyoendelea kuzikabili.

Hatahivyo, naomba ieleweke kwamba uwepo wa mikakati ya propaganda kwenye mitandao na wakati mwingine hata kwenye baadhi ya vyombo vya habari hautanirudisha nyuma katika kushughulikia masuala ya kitaifa yenye maslahi ya umma. Izingatiwe pia kwa nafasi ya ubunge mliyonituma kuwawakilisha nina wajibu kwa taifa; hivyo sitaacha kuendelea kushughulikia matatizo ya kimfumo katika nchi yetu kwa hofu tu ya kuhojiwa kuhusu masuala ya jimbo. Izingatiwe pia nina nafasi ya uongozi katika chama ambayo inaniweka katika mstari wa mbele wa mapambano na wakati mwingine kupokea mashambulizi kutoka kwa wapinzani wetu.

Katika kipindi hiki pia cha kuelekea hukumu ya kesi ya uchaguzi tarehe 24 Mei 2012 tayari zimeanza propaganda kwenye mitandao ya kijamii lakini pia napata simu toka kwa wananchi na pia mrejesho toka kwa viongozi mbalimbali kwenye mikutano yetu jimboni kuhusu ujumbe ambao unasambazwa na makada wa CCM vijiweni.

Naendelea kuyatafakari masuala na matukio yote na nitazungumza wakati muafaka na hata ikibidi kuwataja wahusika kwa majina. Ujumbe wangu kwa wote mlioamua kunitangaza kuwa adui yenu rejeeni historia yangu ya harakati kabla ya kujiunga na siasa 1999 mpaka 2004, na kazi zangu za kisiasa 2005 mpaka 2010; mtanielewa vizuri zaidi. Kuvunja ofisi ya mbunge kuchukua vifaa na nyaraka au kutuma watu mliowatuma hakuwezi kunirudisha nyuma, badala yake mnanipa moyo zaidi wa kusonga mbele nikijua kwamba matokeo yameanza kuonekana.

Kwa wote ambao mnaniunga mkono kwa hali na mali; naendelea kuwashukuru, nimefika hapa nilipo kwa sababu yenu; kwa pamoja tumeshinda, kwa pamoja tutaendelea kushinda. Nimewaandikia mchukue tahadhari juu ya propaganda chafu, wakati mkiendelea na mijadala yenye tija kwa taifa. Endeleeni na uhuru wenu wa kutuhoji na kutukosoa, nami nitaendelea na wajibu wa kuwatumikia na pia kuwajibu kama sehemu ya kuwajibika; maslahi ya umma kwanza.
 
Last edited by a moderator:
Safi sana J.J. Mnyika kwa kutoa ufafanuzi. Tunamngojea Mh. Mdee naye aseme kwani propaganda hizo hazikutolewa kwako tu bali pia kwake.
 
bravo kamanda, unakaribia kupumzika katika ukomboz mkubwa utakaofanyika 2015, ata mimi ninameyasikia haya kamanda mhombe mungu akusaidie.
 
Dogo tulia acha kukurupuka,
we ulitoa ahadi kivyako, naamini hukutoa ahadi kwasababu kikwete anatoa. kwahiyo tunapokuhoji utujibu siyo kusema tumuhoji na kikwete hapo umechemka maana waliotoa ahadi ni wengi na kila mtu kwa wakati wake so hata katika kuhoji, tutamuhoji kila mtu kivyake na wakati wake. nakushauri tu mdogo wangu kuwa ukihojiwa sema umechotimiza mpaka sasa, kilicho kwenye mchakato na kitakachokuja baadaye.
usiwe kama kina nanii hawa sijui mahigeee wanaoanza kuropoka ahaaa misitu oho wanyamapori sijui nini baada ya kuondolewa, sasa wangesema changamoto hizo wakiwa mawaziri tungewaelewa.
mi nipo upande wako pia kukusaport so kaza buti mzee twende
viva cdm, m4c
 
Posted by John Mnyika | May 13, 2012

WanaJF wenzangu, katika kipindi cha kati ya 2011 mpaka 2012 kuna mwelekeo ambao naona ni vyema kila unapoibuka mkauchukulia kwa tahadhari. Kwa nyakati mbalimbali kila ninaposhughulikia masuala ya kitaifa yenye kuwagusa baadhi ya watu ndani ya serikali au CCM huanza vita vya mtandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhoji kuhusu utendaji kazi wangu jimboni sanjari na utekelezaji wa ahadi za kampeni.

Watu hawa hawahoji ahadi za Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM alizozitoa jimboni Ubungo mwaka 2005 na zingine zaidi akazitoa 2010; natambua kuwa wanao uhuru wa kuacha kuhoji ahadi hizo kwa sababu wanazozijua wao na kuhoji ahadi zangu nilizoahidi za kuwawakilisha wananchi, kuisimamia serikali na kushiriki kikimilifu katika kutunga sheria zote zikiwa na lengo la kuwezesha maendeleo.

Hata hivyo katika kutumia uhuru wao huo wa kikatiba ni vizuri pia wakatimiza wajibu wa kufuatilia utekelezaji tunaousimamia kwa kuzingatia kuwa toka nichaguliwe nimekuwa na kawaida ya kutoa mrejesho wa hatua kwa hatua wa kazi ambazo nazifanya za kuwatumikia wananchi jimboni, hivyo ni vizuri rejea ikafanyika katika taarifa hizo na kama kuna maswali ya ziada nipo tayari kuyajibu kwa kila nitakapopata wasaa.

Kwa ajili ya urahisi wa rejea na kutokana na maswali ambayo hujirudia kwa masuala ambayo tayari yameshatekelezwa na nimeshayatolea ufafanuzi kwa nyakati mbalimbali, nafanya utaratibu ili mwaka wa fedha 2011/2012 utakapoisha niweke utekelezaji wote kwenye ripoti moja ya mwaka iwe rahisi kwa rejea. Kwa sasa mnaweza kutembelea http://mnyika.blogspot.com (JOHN MNYIKA) upo mrejesho wa utekelezaji hatua kwa hatua kuhusu namna nilivyotimiza wajibu wa kuisimamia serikali katika kuwezesha maendeleo jimboni, mafanikio tuliyopata mpaka sasa, changamoto tunazokumbana nazo na namna tunavyoendelea kuzikabili.

Hatahivyo, naomba ieleweke kwamba uwepo wa mikakati ya propaganda kwenye mitandao na wakati mwingine hata kwenye baadhi ya vyombo vya habari hautanirudisha nyuma katika kushughulikia masuala ya kitaifa yenye maslahi ya umma. Izingatiwe pia kwa nafasi ya ubunge mliyonituma kuwawakilisha nina wajibu kwa taifa; hivyo sitaacha kuendelea kushughulikia matatizo ya kimfumo katika nchi yetu kwa hofu tu ya kuhojiwa kuhusu masuala ya jimbo. Izingatiwe pia nina nafasi ya uongozi katika chama ambayo inaniweka katika mstari wa mbele wa mapambano na wakati mwingine kupokea mashambulizi kutoka kwa wapinzani wetu.

Katika kipindi hiki pia cha kuelekea hukumu ya kesi ya uchaguzi tarehe 24 Mei 2012 tayari zimeanza propaganda kwenye mitandao ya kijamii lakini pia napata simu toka kwa wananchi na pia mrejesho toka kwa viongozi mbalimbali kwenye mikutano yetu jimboni kuhusu ujumbe ambao unasambazwa na makada wa CCM vijiweni.

Naendelea kuyatafakari masuala na matukio yote na nitazungumza wakati muafaka na hata ikibidi kuwataja wahusika kwa majina. Ujumbe wangu kwa wote mlioamua kunitangaza kuwa adui yenu rejeeni historia yangu ya harakati kabla ya kujiunga na siasa 1999 mpaka 2004, na kazi zangu za kisiasa 2005 mpaka 2010; mtanielewa vizuri zaidi. Kuvunja ofisi ya mbunge kuchukua vifaa na nyaraka au kutuma watu mliowatuma hakuwezi kunirudisha nyuma, badala yake mnanipa moyo zaidi wa kusonga mbele nikijua kwamba matokeo yameanza kuonekana.

Kwa wote ambao mnaniunga mkono kwa hali na mali; naendelea kuwashukuru, nimefika hapa nilipo kwa sababu yenu; kwa pamoja tumeshinda, kwa pamoja tutaendelea kushinda. Nimewaandikia mchukue tahadhari juu ya propaganda chafu, wakati mkiendelea na mijadala yenye tija kwa taifa. Endeleeni na uhuru wenu wa kutuhoji na kutukosoa, nami nitaendelea na wajibu wa kuwatumikia na pia kuwajibu kama sehemu ya kuwajibika; maslahi ya umma kwanza.

bravo jembe!
 
Na barabara ya Sinza E ulisema itajengwa umefikia wapi? Pia tungependa kukuona ukituwakilisha kwenye full council japo posho si kama za ubunge ila matatizo mengi ya wananchi yanaweza kupatiwa ufumbuzi hapa. Unasalimiwa na vijana wa pale mahakama ya ndizi big brother wanafurahishwa sana na jitihada zako za kusubiri waandishi wa habari ndipo ufike kusikiliza shida zao. Sikujua muheshimiwa wewe na JK ni mapacha nitawaambia wapiga kura wasihoji utendaji wako maana watakuudhi ila wahoji utendaji wa JK. Nitawaomba viongozi wa CDM wakuongezee madaraka ya kitaifa ili kuhalalisha kukosekana kwako jimboni. Kwa maana upo busy zaidi ya Mbowe mwenyekiti wako ambaye hata ameteua siku za kukutana na wananchi ila wewe unawajibika zaidi JF.
Sincerely.
Mwana Ubungo anayerubiri mwaka 2015 kukumwaga.
 
Mkuu hapo kumchanganya na huyu mzee wa ahadi umechemka.Yule kila mahali kaahidi cha muhimu wewe kutimiza ya upande wako.Basi kamwe hutakaa ukayasikia hayo maneno unayoyasikia sasa hivi.Hata kama yatakuwepo hayatakua makubwa kama ya sasa.Cha muhimu ni kukaza buti nakuendelea na mapambano kwani muda bado unao.Kila la heri na majukumu yako kwani hizo ndo changamoto za siasa za bongo.
 
Na barabara ya Sinza E ulisema itajengwa umefikia wapi? Pia tungependa kukuona ukituwakilisha kwenye full council japo posho si kama za ubunge ila matatizo mengi ya wananchi yanaweza kupatiwa ufumbuzi hapa. Unasalimiwa na vijana wa pale mahakama ya ndizi big brother wanafurahishwa sana na jitihada zako za kusubiri waandishi wa habari ndipo ufike kusikiliza shida zao. Sikujua muheshimiwa wewe na JK ni mapacha nitawaambia wapiga kura wasihoji utendaji wako maana watakuudhi ila wahoji utendaji wa JK. Nitawaomba viongozi wa CDM wakuongezee madaraka ya kitaifa ili kuhalalisha kukosekana kwako jimboni. Kwa maana upo busy zaidi ya Mbowe mwenyekiti wako ambaye hata ameteua siku za kukutana na wananchi ila wewe unawajibika zaidi JF.
Sincerely.
Mwana Ubungo anayerubiri mwaka 2015 kukumwaga.

ili umchague nani?
 
hajazuliwa maneno yeyote anasikia kuwa wananch wamechoka kwa ahadi ambazo hazitekelezeki watu sasahivi hawatak mwbwembwe za kusimama tu bungen wanataka mabadiliko ya maendeleo,kashashindwa na jimbo ndo byebye!ukiona hivo anakuambia hatak kuhojiwa juu ya ahadi zake eti mbona J.K hawamuhoji!
 
Baada ya kushindwa kufanya maendelea majimboni kwenu.....MNYIKA,MDEE na LISSU mnatafuta wachawi...! Hamna tofauti na wabunge tuliowachoka na kuwaweka ninyi tukitumai mabadiliko....kumbe wote ni walewale...!
 
Mti wenye matunda ndio urushiwao mawe! Kamanda, hii ni ishara kwamba kazi yako ni tishio kwa magamba. Kaza buti, tuko pamoja nawe!!
 
Taabu ya watanzania ni kukosa utashi na upevu wa mawazo,wengi wao hawawezi kukaa na kufikiri na ndio maana wengi wanatoa maoni ambayo siyo,mpaka mda huu mh. Mnyika hana miaka 3 bungeni, yeye anatuwakilisha ila kuchaguliwa kwa kiongozi si kwamba utapata mabadiliko mda huo huo,angalieni yeye si serikali hana uwezo wa kutekeleza ahadi zote ndani ya wiki,mwezi mwaka kwani yeye hatoi fedha mfukoni mwake, nilimsikia akivalia njuga suala la maji,je mabomba yanatolewa bure?barabara inatengenezwa bure?je yeye anapokea allowance kiasi gani? Tujaribu kufikiri kwa muda kwani huwezi kuwa doctor kwa siku baada ya kujiunga chuo cha udaktari
 
sio siri umewapa taarifa, hata usingejibu watumwa wa mafisadi wanaona tu kazi yako, unawakilisha wanaubungo lakini hiyo ni njia tu ya kuwaokoa waTZ wote, ndani ya mafisadi wasioona hata kazi nzuri za viongozi wazuri ndani ya serikali na kuanza kuwachafua wataacha kukuchafua wewe??chapa kazi tupo pamoja, hata kwetu wapo hao Mnyika, tunajua na tunaiona kazi kubwa unayoifanya kulinganishwa na wachumia tumbo, wala usirudi nyuma, mbele daima, ngoma zao hazikeshi, vocha walizopewa zikiisha watanyamaza tu.
Big respect Bro
 
Na barabara ya Sinza E ulisema itajengwa umefikia wapi? Pia tungependa kukuona ukituwakilisha kwenye full council japo posho si kama za ubunge ila matatizo mengi ya wananchi yanaweza kupatiwa ufumbuzi hapa. Unasalimiwa na vijana wa pale mahakama ya ndizi big brother wanafurahishwa sana na jitihada zako za kusubiri waandishi wa habari ndipo ufike kusikiliza shida zao. Sikujua muheshimiwa wewe na JK ni mapacha nitawaambia wapiga kura wasihoji utendaji wako maana watakuudhi ila wahoji utendaji wa JK. Nitawaomba viongozi wa CDM wakuongezee madaraka ya kitaifa ili kuhalalisha kukosekana kwako jimboni. Kwa maana upo busy zaidi ya Mbowe mwenyekiti wako ambaye hata ameteua siku za kukutana na wananchi ila wewe unawajibika zaidi JF.
Sincerely.
Mwana Ubungo anayerubiri mwaka 2015 kukumwaga.

ACHA UJINGA WEWE, KWANI YEYE NI MHANDISI WA BARABARA? KAWAULIZE WAHANDISI WA HALAIMASHARi
 
Back
Top Bottom