Tahadhari: Kondomu Bandia Zauzwa Nchini

popiexo

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
742
195
KONDOMU zinazodaiwa kuwa ni bandia ambazo zilipigwa marufuku nchini Uingereza kutokana na kubainika kuwa hazina ubora unaotakiwa, zimetapakaa katika maduka mbalimbali ya dawa nchini, Mwananchi limebaini. Kondomu hizo ni Durex na Trojan ambazo zina vipele na uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa zinauzwa katika maduka mbalimbali ya dawa kwa bei ya Sh5,000.

Mwishoni mwa mwaka jana, Serikali ya Uingereza ilifanya msako mkali kwa lengo la kukamata mamilioni ya kondomu hizo, wakati ambao ilikuwa imepita takriban miezi 18 tangu zilipokuwa zimeingizwa nchini humo. Mdhibiti wa Dawa na Bidhaa za Afya wa Uingereza alinukuliwa akisema kuwa mamilioni ya kondomu hizo feki ziliingizwa kutokea Mashariki ya Mbali na kwamba tayari zilikuwa zimetumiwa na idadi kubwa ya watu.

kondom+pic.jpg

Kondomu hizo zinadaiwa kutokuwa na ubora hali inayoweza kuongeza hatari kwa watumiaji kwa kusambaza kwa kasi magonjwa ya zinaa, virusi vya Ukimwi au kusababisha mimba zisizohitajika, hivyo kuharibu mikakati ya uzazi wa mpango.

Ofisa Habari wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Gaudensia Simwanza akizungumza na gazeti hili jana, alithibitisha kuwapo kwa taarifa za kondomu hizo za Durex na Trojan na kuongeza kuwa mamlaka hiyo imewaagiza wakaguzi wake kuzichunguza ili kubaini kama zina ubora ama la. “Wakaguzi walichukua sampuli ya kondomu hizo kwa lengo la kuzichunguza, nipe muda kidogo ili nizungumze na mkurugenzi ili kujua uchunguzi ule umefikia wapi,” alisema Simwanza.

Alipotafutwa baadaye alibainisha kwamba uchunguzi wa sampuli hiyo bado upo maabara na kwamba majibu yake hayajatoka. Hata hivyo hakusema ni lini yatatolewa.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Leandri Kinabo aliomba apewe muda ili afuatilie kujua ni kondomu za aina gani zilizowahi kukamatwa na kupigwa marufuku zisitumike.

“Nipe muda kidogo nifuatilie ili kujua zilizopigwa marufuku na ambazo tulizizuia kuingizwa nchini, nitafute mchana,” alisema Kinabo ambaye alipotafutwa baadaye alisema yuko kwenye kikao na kwamba alikuwa hajaweza kuwasiliana na watu wa maabara.

Hii siyo mara ya kwanza kuibuliwa kwa taarifa za kuwapo kwa kondomu feki nchini, kwani Desemba 20, mwaka jana kontena lililosheheni kondomu za kiume aina ya Melt Me kutoka nchini India lilikamatwa na kuzuiwa katika Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kubainika kuwa hazifai kwa matumizi.

Maofisa wa TBS walilazimika kufanya msako katika baadhi ya maduka ya dawa jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kuziondoa kondomu hizo katika soko.

Source: Mwananchi
 
fazaa

JF-Expert Member
May 20, 2009
2,985
0
Kama una mke wako sidhani utababaika kutafuta condom.

Wanao tafuta condom ni wale vichaa wasio tulizana na wake zao au hawataki kuoa.

Wapumbafu watabaki kuwa wapumbafu tu, kwani condom nani amezipa mtaji kama sio vichaa wasio tulizana na wake zao, au wasio tafuta mke wakaoa :biggrin:
 
silver25

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
744
0
Tulia na mkeo ambaye mulisha pima na kufanana majibu, ili usitumie kabisa, muwe Waaminifu kwasababu hii hali tuliyonayo si mzuri kabisaaaaaaa
 
Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,605
2,000
Kama una mke wako sidhani utababaika kutafuta condom.

Wanao tafuta condom ni wale vichaa wasio tulizana na wake zao au hawataki kuoa.

Wapumbafu watabaki kuwa wapumbafu tu, kwani condom nani amezipa mtaji kama sio vichaa wasio tulizana na wake zao, au wasio tafuta mke wakaoa :biggrin:

Mkubwa na wanawake wasioolewa na wasiotulizana na wanaume wao ni wendawazimu......?
 
HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,613
2,000
Kwa wale wasiotulia au wenye urafiki kabla ya ndoa, ni vyema kuchukua tahadhari ....
 
LINCOLINMTZA

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
1,640
0
Nani kakwambia kwamba kondomu inazui ukimwi?
Ukimwi hauzuiliki hata kwa kondomu za bati

By profesa Jay.
 
popiexo

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
742
195
Kama una mke wako sidhani utababaika kutafuta condom.

Wanao tafuta condom ni wale vichaa wasio tulizana na wake zao au hawataki kuoa.

Wapumbafu watabaki kuwa wapumbafu tu, kwani condom nani amezipa mtaji kama sio vichaa wasio tulizana na wake zao, au wasio tafuta mke wakaoa :biggrin:

Wengine hutumia kwa ajili ya uzazi wa mpango.
 
fazaa

JF-Expert Member
May 20, 2009
2,985
0
Wengine hutumia kwa ajili ya uzazi wa mpango.
Siwezi kufanya ujinga huo condom zote zina chemical, lazima ni uthamini mwili wa wife wangu, nitacheza mchezo wa kawaida withdraw methord-pulling out:high5:
 
Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,605
2,000
Kama ulivyo sema na wao ni wendawazimu tu vipi wazini kabla ya kuolewa:biggrin:

Mkubwa wabembelezaji ni siye wenyewe unanyenyekea mpaka basi kisa upate kile kipenyo dah..............!
Basi dunia nzima vichaa na wendawazimu...............!:A S shade:
 
sarikoki

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
1,195
0
KONDOMU zinazodaiwa kuwa ni bandia ambazo zilipigwa marufuku nchini Uingereza kutokana na kubainika kuwa hazina ubora unaotakiwa, zimetapakaa katika maduka mbalimbali ya dawa nchini, Mwananchi limebaini. Kondomu hizo ni Durex na Trojan ambazo zina vipele na uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa zinauzwa katika maduka mbalimbali ya dawa kwa bei ya Sh5,000.

Mwishoni mwa mwaka jana, Serikali ya Uingereza ilifanya msako mkali kwa lengo la kukamata mamilioni ya kondomu hizo, wakati ambao ilikuwa imepita takriban miezi 18 tangu zilipokuwa zimeingizwa nchini humo. Mdhibiti wa Dawa na Bidhaa za Afya wa Uingereza alinukuliwa akisema kuwa mamilioni ya kondomu hizo feki ziliingizwa kutokea Mashariki ya Mbali na kwamba tayari zilikuwa zimetumiwa na idadi kubwa ya watu.

View attachment 84578

Kondomu hizo zinadaiwa kutokuwa na ubora hali inayoweza kuongeza hatari kwa watumiaji kwa kusambaza kwa kasi magonjwa ya zinaa, virusi vya Ukimwi au kusababisha mimba zisizohitajika, hivyo kuharibu mikakati ya uzazi wa mpango.

Ofisa Habari wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Gaudensia Simwanza akizungumza na gazeti hili jana, alithibitisha kuwapo kwa taarifa za kondomu hizo za Durex na Trojan na kuongeza kuwa mamlaka hiyo imewaagiza wakaguzi wake kuzichunguza ili kubaini kama zina ubora ama la. "Wakaguzi walichukua sampuli ya kondomu hizo kwa lengo la kuzichunguza, nipe muda kidogo ili nizungumze na mkurugenzi ili kujua uchunguzi ule umefikia wapi," alisema Simwanza.

Alipotafutwa baadaye alibainisha kwamba uchunguzi wa sampuli hiyo bado upo maabara na kwamba majibu yake hayajatoka. Hata hivyo hakusema ni lini yatatolewa.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Leandri Kinabo aliomba apewe muda ili afuatilie kujua ni kondomu za aina gani zilizowahi kukamatwa na kupigwa marufuku zisitumike.

"Nipe muda kidogo nifuatilie ili kujua zilizopigwa marufuku na ambazo tulizizuia kuingizwa nchini, nitafute mchana," alisema Kinabo ambaye alipotafutwa baadaye alisema yuko kwenye kikao na kwamba alikuwa hajaweza kuwasiliana na watu wa maabara.

Hii siyo mara ya kwanza kuibuliwa kwa taarifa za kuwapo kwa kondomu feki nchini, kwani Desemba 20, mwaka jana kontena lililosheheni kondomu za kiume aina ya Melt Me kutoka nchini India lilikamatwa na kuzuiwa katika Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kubainika kuwa hazifai kwa matumizi.

Maofisa wa TBS walilazimika kufanya msako katika baadhi ya maduka ya dawa jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kuziondoa kondomu hizo katika soko.

Source: Mwananchi

Du.! hii kitu siwezi kutumia kabisa, hapa lazima niwe mkweli. Na ndio maana mimi sio muasherati maana hata kama nikisema niibe ruti nitapiga kavu tu.
 
mkonowapaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
1,494
1,225
kondom ninazoziamini siku zote ni SALAMA tu!! haya ma-imported huwa siyakubali,,,pamoja na garama zake kuwa kubwa........pia kondom kama Dume nna kesi nao soon!!zinapasuka sijawahi ona....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom