Tahadhari, Internet Inaua Nguvu za Kiu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahadhari, Internet Inaua Nguvu za Kiu

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, May 4, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,618
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"][/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD][​IMG][/TD]
  [TD]
  Habari si nzuri kwa wanaume wanaopenda kutumia wireless internet kwenye laptop zao wakiwa wameziweka laptop zao mapajani au karibu na viungo vyao muhimu vya kiume, utafiti wa wanasayansi wa Marekani na Argentina umeonyesha kuwa wireless internet inaua mbegu za kiume.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Utafiti uliofanywa na wanasayansi toka Marekani na Argentina umeonyesha kuwa wireless internet kwenye laptop ina madhara kwa viungo vya uzazi vya mwanaume kwa kuharibu ubora wa mbegu za kiume au kuziua kabisa.

  Utafiti uliofanywa kwa kuweka mbegu za kiume chini ya laptop inayotumia wireless internet ulionyesha kuwa mbegu za kiume zilipungua ubora wake na hivyo kupunguza chansi ya mwanaume kupata mtoto.

  Utafiti huo ulifanywa na timu ya wanasayansi toka taasisi ya Nascentis Centre for Reproductive Medicine iliyopo Cordoba, Argentina kwa kushirikiana na wanasayansi wa Marekani wa taasisi ya Eastern Virginia Medical School.

  Mbegu za kiume za wanaume 29 wenye afya njema wenye umri kati ya miaka 26 na 45 zilikusanywa na kugawanywa makundi mawili. Kundi moja la mbegu za kiume liliwekwa chini ya laptop inayotumia wireless internet na jingine liliwekwa mbali na laptop zinazotumia wireless internet.

  Matokeo ni kwamba robo ya mbegu za kiume zilizowekwa chini ya laptop yenye wireless internet ziliuliwa ndani ya masaa machache. Vinasaba au DNA ya mbegu za kiume nazo ziliharibiwa.

  Kwa upande wa pili, mbegu za kiume zilizowekwa mbali na laptop hazikuonyesha kupatwa na madhara yoyote zaidi ya kupungua kidogo sana kwa spidi ya kuogelea ya mbegu za kiume.

  Wakati huo huo, mbegu za kiume zilizowekwa chini ya laptop ambayo haikuwa imeunganishwa kwenye internet hazikuonyesha kukumbwa na uharibifu mkubwa kama uliotokea pale zilipowekwa chini ya laptop iliyounganishwa kwenye wireless internet.

  "Utafiti wetu unaonyesha kuwa kutumia wireless internet huku ukiwa umeiweka laptop karibu na viungo vya uzazi hupelekea kuharibika kwa ubora wa mbegu za kiume", alisema Dr Conrado Avendano, ambaye ndiye aliyeongoza utafiti huo.

  "Kwa sasa hatujui kama madhara haya yapo kwenye laptop zote ziliounganishwa kwenye wireless internet au la".

  Sababu ya kuharibika kwa mbegu za kiume huenda ikawa inasababishwa na miale ya electromagnetic inayotolewa na wireless internet.

  Matokeo ya utafiti huu yamewekwa kwenye jarida la mwezi huu la Fertility and Sterility journal, ingawa dokta Avendano amewataka wanaume wasipaniki kwani tafiti zaidi zinaendelea kuhusiana na suala hili.
  Tahadhari, Internet Inaua Nguvu za Kiume
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 429
  Trophy Points: 180
  hata mimi nilishawai kuhisi kitu kama hichi mkuu ! asante kwa angalizo
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu asante sana kwa tahadhari hii maana inatupa angalizo zuri sana kuhusu hizi laptop tunazotumia na kuziweka mapajani
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  kuna ukweli huko.............ninaamini hata simu za mkononi ambazo huwa tunaziweka kifuanio upanda wa kushoto ambako moyo uko na simu kwenye mifuko ya mbele karibu na kokwa za kiume zinaweza kuleta madhara ya kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume..............au magonjwa ya moyo
   
 5. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mzizimkavu hii ni habari njema ndio maana kila wakati nasema hizi new technology zina mambo mengi sana ila kikubwa tutafute njia ya kuli cover hii situation nje ya hapo ni janga kwa nchi za dunia ya tatu
   
 6. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,748
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  ni kwali! Niliwahi kusikia habari kama hii BBC Swahili. Swali; je hata internet ya simu za mkononi ina madhara kama haya?
   
Loading...