Tahadhari: Epuka wizi huu

Tahadhari: Epuka wizi huu

sir j

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2016
Posts
319
Reaction score
214
Kuna baadhi ya wazazi, marafiki na ndugu wengi wamekuwa wakiibiwa sana pesa hasa kwa mfumo wa mtandao, kwa mfano, kuna mzazi mmoja ambaye yupo Mbeya, lakini anakijana wake yupo mikoa ya Kanda ya ziwa kimasomo. Mzazi huyu alipokea ujumbe kwa simu ukimtaka kutuma pesa kwa ajili ya mwanae aliyepo masomoni, na kwamba asipotuma pesa hiyo, hatua kali zitachukuliwa dhidi ya mwanae huyo.

Bila ya uchunguzi wowote, mzazi huyu alituma jumla ya Shilingi 314,000/- ndo akawa ametapeliwa namna hiyo.

Halafu, msambazaji wa meseji hizo hujitambulisha kuwa yeye ni mkurugenzi wa shule husika anayosoma mwanao, rafiki au ndugu yako.

Kuwa makini sana na jumbe zisizoeleweka zinazotumwa kwenye simu yako.

Hapa chini ni moja kati ya meseji hizo zinazotumwa na huyo tapeli.

" Baba, mjiandae siku ya ijumatatu kuna mchango wa kwenda savei masai-mara ya Serengeti Kenya, na tunakaa huko siku 5. Jana wakurugenzi ndio wametoa uamuzi hasa wenye masomo yetu na tunaenda kufanya mtihani yaani majaribio, maksi nitakazopata wataunganisha kwenye matokeo yangu ya kuhitimu. Tunaondoka tarehe 4 hadi tarehe 9. Mchango ni sh. 100,000/=.
Usafiri na chakula na malazi, wenzangu wameshaanza kutoa. Tuma kwa mwalimu namba hii. Msalimie mama.
by mwanao Kan
by paroko."

NB:-
Habari hii ni kweli na nitukio ambalo limetokea kwa jamaa yangu wa karibu. and I am a third part victim on the issue.


Please be aware
 
Inakuwaje mtoto anasoma shule ya mbali mzazi unakuwa huna hata namba ya simu ya uongozi wa shule? Yaani unambwaga mtoto shuleni hata hufuatilii mambo yake?
 
ila kuna wizi mwingine tunaingia kichwa kichwa cc wenyewe mmh
 
Back
Top Bottom