SoC01 Tahadhari: Biashara za mtandaoni ni chanzo cha umaskini

Stories of Change - 2021 Competition

Jurudyiza

Member
Jul 15, 2021
70
96
Mtoa mada ##JURUDYIZA##

Wapendwa hakuna jipya chini ya jua asilimia kubwa ni ubatili mtupu.

Kwa sasa watu wengi wanajikita kutafuta utajiri wa haraka bila kujua harakaharaka haina baraka Na ujue tu kwamba Sayansi na teknolojia kwetu Afrika bado inanufaisha wachache tena nao wananufaika kwa kuhadaa wengi wasiojua au wale wanaokurupuka kufanya maamuzi.

Biashara za mtandao kwa sasa zimewaliza wengi wanaotamani kufanikiwa zaidi kwa kutumia njia za mkato na biashara hizo ni hadaa sana na wao wanao zihubiri asilimia kubwa hawajanufaika bali nao ni walaibu tu wakiamini ipo siku watatoka tu mwishowe huwa hawasimulii tena hasara wanazozipata.

Ndugu zangu mimi ni mhanga mkubwa, nimefanya biashara mbalimbali japo si zote ila nakupa mfano wa chache nilizo na uzoefu.

Kwa ukweli wangu naamini mtaunga mkono kama kweli ninyi ni wakweli na uhalisia ni kwamba kwenye biashara za mtandao mifumo yake ni migumu kukutajilisha na huwezi kupata utajiri kiurahisi. Mfano wa biashara hizo ni kama zifuatazo:-

Forex na mfano wa hizo, hapa najua wapo wengi wanatamani kufanya biashara hizo na baadhi yao wanajigamba wana mafanikio makubwa, Du hapana nasema hapana! Naamini kabisa kati ya watu 100 wanaofanikiwa ni watu 3 hadi 5 na huo ni mtazamo wangu tu ila najua hata watu hao ni wengi sana na hii inaniuma sana.

Kwenye mfumo huo wa FX wanaofanikiwa naamini kabisa ni wale walioutengeneza mfumo huo wa biashara ukianzia na mifumo yao ya kufanyia biashara iwe MT4 au MT5 kute huko ni sehemu ya kuteketezea fedha.

Kwa mfano mtu anaweza kuweka USD 200 lakini ndani ya dakika 20 akawa amepata hasara ya hela yote sasa hiyo ni biashara kweli! Hapana mtamaliza hela zenu bure ni bora hiyo USD 200 zaidi ya TSH 400,000/= ukafanyia biashara nyingine au huu ni uongo? Hata biashara ya nyanya huwezi kupata hasara hiyo yote kwa mpigo ni biashara kweli hiyo au balaa!

Mimi naamini kabisa hakuna biashara ya kukupatia faida kwa mkato na ukawa tajiri zaidi ya kujituma na kuwa mbunifu katika biashara ndogo unayoanza nayo wewe mwenyewe kuliko hizi zinazohamasishwa na vijana.

Wengine wamegeukia kubashiri michezo mbalimbali kwa kuangalia dau linalowekwa, ndugu yangu nako huko usithubutu utamaliza pesa zako tu, kupatia timu zote hasa kwenye JACKPOT sio mchezo ndio maana wanaobashiri wanaweza kuwa 100000 lakini asipatikane hata mmoja, kwenye hii michezo hakuna cha odd ndogo wala kubwa wengi wanalia na faida inaend kwa yule aliyetengeneza mfumo huo ila nyie mnaliwa tu.

Ukija kwenye biashara zenye sura ya upatu kama forever na nyinginezo nazo hamna jipya chini ya jua, ninauzoefu nayo na nimeifanya simaanishi ni biashara mbaya bali uwezo wa kufanikiwa ni mdogo sana wala hatipaswi kudanganyana. Ni vema mtu unapomhamasisha ajue kwamba biashara hiyo ni nzuri ila pia ni ngumu sana kwa mfano unapewa bidhaa/virutubisho uuzie watu ili wanunue na kwa sababu utawaaminisha kwamba zitawasaidia halafu wao wananunua na haziwasaidii au unamuunganisha mtu kuingia kwenye biashara hiyo kwa zaidi ya Tsh210, 000/= Za kianzio ambapo akishaingia anawaza tu kuwa tajiri bila kujua kwamba wakati mwingine hata bidhaa alizopewa kwa kuanza nazo wakati mwingine hata hazipati wateja! Mwishowe unavunja urafiki naye na kuwa maadui,.

Ni heri sisi tubadilike na tujue biashara zinazoendelea mitandaoni zinamaliza na kukausha fedha tunazozitafuta kwa nguvu na jasho letu na hizo fedha zikiteketea huko tunabakia hatuna wa kumlaumu zaidi ya kuumia mioyoni mwetu tu.

Nawaomba ndugu zangu tufanye kazi kwa bidii na tuwe wabunifu kwa kutengeneza vyanzo sahihi vya fedha na usihadaike na kudanganywa kuingia kwenye biashara ya mtandaoni bila kuwa na elimu ya kutosha kwani huko unaweza kuishia kulia tu.

ASANTENI SANA.
 
Wabongo bhana,ukiangalia Wateja wa betting apps ni zaidi ya 10M+now na hao wanachukua uncalculated risk,kwa sababu kubet hakuhitaji sana ujuz na elimu lakn kwenye swala la forex maneno shazi.WATU zinawauwa tamaaa zao kenye Fx ,watu wanaingia na over expectations sina maneno mengi bhana ila Forex is real legit profitable and business like other businesses ,DO YOUR OWN RESEARCH AND COME WITH YOUR OWN CONCLUSION,Never believe preached utajiri
 
Target ya maskini ni kuvuna papo hapo, wenzetu wanawekeza kwa 5 good years ndipo anaanza kula matunda.

Forex nimeanza 2017, nimepoteza sana but now ni gwiji wa fx na binary natumia uzoefu utokanao na fx.
Elimu
Elimu
Eli

Napata hasira sana nikiona vijana mnatapeliwa kirahisi namna hii.
Fuga hata bata achana na mambo ya forex.

We endelea kulipia bills za wanaume wenzako huko Bahamas.
Unavyosema ni Kama vile labda sijawahi weka hela Nika tredi nikapata faida na nikaituma kwa benki akaunti.
Ishu ni ngumu na retailer traders Yuko kwenye worst scenario,Mana anaandamwa Sana maadui mengi like commissions.
Ni Nani anayetapeliwa mkuu.
 
Forex will never make you rich. Go find a job. Toka hapo kwa shemeji yako acha dada yako akazwe kwa uhuru.

Find a job dude. Huu ndio ukweli mchungu kwako na washamba wenzako.

Tena wewe utakuwa umesoma education maana mnakuwaga wajinga sana.

Find a job man. Forex Is scam.
Duu unaonekana wewe una miliki Dola bilioni kadhaa sana,afu uko arrogant Sana.
You don't know me.
Kwani education sio kozi mkuu.
Ila unaonekana bado uko around mid twenties.

Sina haja ya majigambo Mana hayasaidii kitu.
Namie siwezi kuiga Tabia yako Nina ethics zako.

Inaonekana umepoteza Sana hela pole Sana mkuu.

Yani nisingekuwa mwenyewe shahidi basi ningefuatana na wewe.

Ishu Iko taiti around 100 wanapita 5 pekee.
I know why no need to prove to you.

Naona umeseomea Latvia umekuwa Kama wewe ndiye mbongo wa kwanza kusomea nje.

Yani blacks huwa wanajiona ufahari Sana kuishi ama kwenda nchi za wanaume wengine ambao Babu zao walimwaga damu wakazijenga. Yeye anakuwa Kama mwanamke anaenda kuishi kwa kuolewa.
Hujaulizwa Kama kwenu hakuna shule mpaka ukaenda.

Unaongea lugha fulani Ivi hata mjukuu wa Trump hawezi iongea na anakuwa yupo loyal to people.

Yaani unajiona Kama unaweza nunua watu na huku hata hujajenga darasa moja ukasaidia community yako.

Ama pesa zako unazipima kwa starehe unazofanya mkuu.

Ngoja nikuache.
I won't argue with anymore
 
Unavyosema ni Kama vile labda sijawahi weka hela Nika tredi nikapata faida na nikaituma kwa benki akaunti.
Ishu ni ngumu na retailer traders Yuko kwenye worst scenario,Mana anaandamwa Sana maadui mengi like commissions.
Ni Nani anayetapeliwa mkuu.
Sio kwamba watu hawapati hata kidogo, shida ni kwamba kwenye biashara hii watu wanaifanya wakiwa wameaminishwa kufanikiwa zaidi na wengi huaminishwa fx ni biashara ya wasomi tatizo mafanikio ya nayopatikana kwa traders ndio hayaonekani kiasi kwamba mtu wa kawaida kumthibitishia uwepo wa mafanikio katika biashara hii ni ngumu.
 
It needs knowledge, experience and capital. So unadhani ni rahisi kuvipata vyote ivyo lakini ama unaona ni kazi rahisi.
Mana ili uifurahie uwe na angalau na $10k,uzoefu above 5yrs,uwe umetredi na ku triple angalau akaunti ya demo.

Ishu ni ngumu namie nalijua ilo sio rahisi.
Hii ni zaidi ya wito ama kazi mkuu.

Yaani ni ngumu kweli ni lazima mtu aishie njiani asipopata right education.
Education na vitabu na mentors wamejaa na wao walipigwa wakakimbilia kuifundisha.
Sasa kupata right books,mentor,n.k pia ni kazi Sana Tena Sana.
Ref wayne mwenyewe anapiga demo na kuuza signals.

Pia watu wanakuja wanajua hakuna kazi.
Yani ni ngumu Bora hata ukalime

Na iyo nimeshiona siwezi nikamwambia mtu aingie Kama sio ambitious,
Yaani sijui nisemeje.

You've to sacrifice your life kwa muda mchache like 7yrs.
Ni Nani Yuko tayari kwa iyo ishu na hapa usiku mchana muda wote uko nayo unastadi na kudemo tredi.
Hakuna hela nyepesi.

Kuna sadaka kubwa you've to pay.
Na ndo Mana wanaofanikiwa ni wa kutafuta kwa torch.

How about Jesse Livermore,ama wale waliomo kwa market wizard ama ni story za kutunga kuvuta wajinga.
 
Sio kwamba watu hawapati hata kidogo, shida ni kwamba kwenye biashara hii watu wanaifanya wakiwa wameaminishwa kufanikiwa zaidi na wengi huaminishwa fx ni biashara ya wasomi tatizo mafanikio ya nayopatikana kwa traders ndio hayaonekani kiasi kwamba mtu wa kawaida kumthibitishia uwepo wa mafanikio katika biashara hii ni ngumu.
Kwa sasa watu wengi wanajikita kutafuta utajiri wa haraka bila kujua harakaharaka haina baraka Na ujue tu kwamba Sayansi na teknolojia kwetu Afrika bado inanufaisha wachache tena nao wananufaika kwa kuhadaa wengi wasiojua au wale wanaokurupuka kufanya maamuzi.

Hii nimeikopi kwa jamaa aliyeileta maada mbona inajielezea kabisa hapo
 
In trading you're competing against the sharpest mind in the world.
Muda huo wanawaza kuchukua hela zako na wewe unawaza kuchukua hela zao.
So unaweza game ikoje.
Ukipoteza mwingine ndiye anaipata.
Mana mnakuwa mna bet against value decrease/increase ya financial instruments.
Naweza Nika speculate kuwa value ya gold itapanda mwingine akachukua Oda yangu akadai kuwa itashuka.

Trading ni highly liquid market.
Millions of Dollars can be just be made/lost in a matter of blink an eye.
Ishu sio nyepesi yaani ni ngumu.

Pia mtu Kama hujaweza toka kwa ishu fulani haimaanishi kuwa basi kila mtu atafuata nyayo zako.
Self limiting beliefs.
This game is against human nature na hii najua kabisa ndo Mana tunapigwa za uso.

Yaani it's very counterintuitive to our every DNA stored in our body.
You're swimming against human nature.
Ni ngumu Ila it can be done.

Kama ukiona Ina suit your traits go on ukiona haikufai sepa kabisa.
Sio rafiki Sana na our human nature
 
Mkuu nakuunga mkono kwa asilimia kubwaa mkamaria mwenzangu....hata mimi kati ya kuBet na Foreksi nilichagua,nachagua na NitachG
Aua kubet maishaaa FX amna pesa nshawai kujaribu kusoma na mavideo ya course za udemy ninazo ila roho ikakataa kabsaa mwaisa roho inasema "kama unataka kuona dunia chungu anza kutrade Foreksi" kuna mdau kasema hapo juu kubet ukiweka pesa ikaenda ndo imeenda....hapana haiko ivo ckuiz tumia System bet mfano ukiweka mechi 3 ikalost 1 unarudishiwa stake yako kiasi ila uko kwenye kudownload mapesa hapana aisee

Sijawahi kucheza system bet, niambie ni kampuni gani unabetia?
 
Mbona Kama uko arrogant na ego inakutawala mkuu.
Unajipamabanua Sana hata sijui umefanya Nini dunia tukufahamu. Sasa kusomea Latvia umevumbua Nini ama kisa kuruka na ndege na kula nyeupe huko club unajiona Kama unatembea hewani haukanyagi ardhini Kama sie mkuu.

Kwani mchaga umefanya invention gani basi ndugu. Yaani uko na ego Ile mbaya unajiona uko smart Sana kuliko binadamu wote.
Una ukwasi gani ndugu.
Uko Forbes ama uko jf?
Nina Imani hauna hata kitu kinaitwa Dola Billioni ili angalau uweke kwenye list ya matajiri.
Mbona dangote akatulia mkuu.
Yaani debe huvuma Sana ili lisikike Ila lililojaa limetulia.
NB mie Sina hela,Mana utaanza kuwa mie Nina hela gani.

Ila am sure you don't own $bilioni even a half.
Watanzania Wana nguvu za kuwekeza kwa juice Ila sio kwa gesi. In prof Muhongo voice.
Una hela unafanya Nini huku mkuu.
Remember money can't lenghten your tongue, so be humble kijana Kama umezipata unajiona kuwa unaweza kumtawala kila mtu Kama mkeo ama mwanao sio ivyo.
Usiwe limbukeni wa kushika hela.remember gives you freedom and make you rich.

Haya boss hata huwa unadhamini Nini hapo kijijini kwenu
Hahaha emesomea Latvia anajiona kamaliza kila kitu.

Hawa ndio Elon Musk anawatukana jitu Lina madegree ughaibuni halijavumbua hata Vijiti vya kujichokonolea meno
 
Ujue mtu akishasoma anajiona kuwa yeye pekee anastahili kuishi duniani.
Wasiosoma ama walisomea kozi za ualimu hawana thamani kwake.
Yaani hujui kuwa jk nyerere alikuwa mwalimu akamkomboa toka kwa mkoloni,
Jpm ,majaliwa Samia na wabunge kibao like mwita weitara na ryoba marwa ni walimu Ila saivi wako wapi.
Na yeye akasoma kozi yake iliyo keki Ila hata hasikiki anapiga kelele asikike na ajulikane na hao hapo hawapigi kelele.

Anatakiwa atafute pesa mpaka awe anatambulishwa na sio kujitutumua humu kuwa tumfahamu kuwa akasomea Latvia kanchi ambako hakana hadhi hakajulikani.
Angekuwa ameenda like uk Germany USA n.k asingepata shida kujitambulisha.
Ila achana naye anavyoongea unajua yukoje ama ametokea mazingira gani huko nyuma.
Angekuwa ametokea Kama familia ya mbowe ama mengi ambao wote ni wa machame na Wana hela hata asingehaika ili Koo yake ijulikane.
Angekuwa humble Mana amezaliwa home akaukuta utajiri,hausigeli na shamba boy wote Wana magari Yao.
Ila yeye akabahatisha so anataka aabudiwe Mana huko kwao anaabudiwa.
Nina ukwasi ,ukwasi gani ama kuhonga demu laki afu ukimbeba kwa kibebi woka chake akimuweka hapo samaki samaki akitumia tulaki labda tuwili basi anajiona kuwa yupo juu ya dunia.

Kama mbabe akatalii hata huko space,angeungana na jef Benzos wakaenda huko.

Nina Imani anatembelea gari second hand Ile zero mileage hana hata Jesus Christ.
Ila bana ngoja nimpuuzie
 
Hamna mnalolijua, nyie ni washamba wa kutupwa. Mtauza hadi pichu kisa forex.
Tafuteni kazi vijana, hela za ku-download hazipo.

Najua mnahisi nawabeza or kuwadharau but sio hivyo, huu ni ukweli mchungu nawaambia na Ipo siku mtanikumbuka baada ya kuuza kila kitu hadi pichu zenu.

Tena we keisangora unaandika text ndeeeefu Inaonesha kabisa how ume-panic. Relax boy and find a job.
 
Poa pamoja Sana mangi. Sijapanick Ila maongezi yako ndiyo hayo yanayoudhi.
Relax
 
Hamna mnalolijua, nyie ni washamba wa kutupwa. Mtauza hadi pichu kisa forex.
Tafuteni kazi vijana, hela za ku-download hazipo.

Najua mnahisi nawabeza or kuwadharau but sio hivyo, huu ni ukweli mchungu nawaambia na Ipo siku mtanikumbuka baada ya kuuza kila kitu hadi pichu zenu.

Tena we keisangora unaandika text ndeeeefu Inaonesha kabisa how ume-panic. Relax boy and find a job.
Pia weka hapa wewe unalolijua. Sie hatujui ni washamba tumekubali. Wewe mjanja wa latvia.hujapata demu uko ukaja kuuzia sura bongo
 
Hamna mnalolijua, nyie ni washamba wa kutupwa. Mtauza hadi pichu kisa forex.
Tafuteni kazi vijana, hela za ku-download hazipo.

Najua mnahisi nawabeza or kuwadharau but sio hivyo, huu ni ukweli mchungu nawaambia na Ipo siku mtanikumbuka baada ya kuuza kila kitu hadi pichu zenu.

Tena we keisangora unaandika text ndeeeefu Inaonesha kabisa how ume-panic. Relax boy and find a job.
We lofa unadhani Mimi nategemea forex.

Kwa Ego yako ukute huna lolote. Nina uwezo wa kukuajiri wewe na mama yako mkawa wafanyakazi wangu.

Umeenda kusoma lativia unajiona mjanja sana stupid
 
Mtoa mada ##JURUDYIZA##

Wapendwa hakuna jipya chini ya jua asilimia kubwa ni ubatili mtupu.

Kwa sasa watu wengi wanajikita kutafuta utajiri wa haraka bila kujua harakaharaka haina baraka Na ujue tu kwamba Sayansi na teknolojia kwetu Afrika bado inanufaisha wachache tena nao wananufaika kwa kuhadaa wengi wasiojua au wale wanaokurupuka kufanya maamuzi.

Biashara za mtandao kwa sasa zimewaliza wengi wanaotamani kufanikiwa zaidi kwa kutumia njia za mkato na biashara hizo ni hadaa sana na wao wanao zihubiri asilimia kubwa hawajanufaika bali nao ni walaibu tu wakiamini ipo siku watatoka tu mwishowe huwa hawasimulii tena hasara wanazozipata.

Ndugu zangu mimi ni mhanga mkubwa, nimefanya biashara mbalimbali japo si zote ila nakupa mfano wa chache nilizo na uzoefu.

Kwa ukweli wangu naamini mtaunga mkono kama kweli ninyi ni wakweli na uhalisia ni kwamba kwenye biashara za mtandao mifumo yake ni migumu kukutajilisha na huwezi kupata utajiri kiurahisi. Mfano wa biashara hizo ni kama zifuatazo:-

Forex na mfano wa hizo, hapa najua wapo wengi wanatamani kufanya biashara hizo na baadhi yao wanajigamba wana mafanikio makubwa, Du hapana nasema hapana! Naamini kabisa kati ya watu 100 wanaofanikiwa ni watu 3 hadi 5 na huo ni mtazamo wangu tu ila najua hata watu hao ni wengi sana na hii inaniuma sana.

Kwenye mfumo huo wa FX wanaofanikiwa naamini kabisa ni wale walioutengeneza mfumo huo wa biashara ukianzia na mifumo yao ya kufanyia biashara iwe MT4 au MT5 kute huko ni sehemu ya kuteketezea fedha.

Kwa mfano mtu anaweza kuweka USD 200 lakini ndani ya dakika 20 akawa amepata hasara ya hela yote sasa hiyo ni biashara kweli! Hapana mtamaliza hela zenu bure ni bora hiyo USD 200 zaidi ya TSH 400,000/= ukafanyia biashara nyingine au huu ni uongo? Hata biashara ya nyanya huwezi kupata hasara hiyo yote kwa mpigo ni biashara kweli hiyo au balaa!

Mimi naamini kabisa hakuna biashara ya kukupatia faida kwa mkato na ukawa tajiri zaidi ya kujituma na kuwa mbunifu katika biashara ndogo unayoanza nayo wewe mwenyewe kuliko hizi zinazohamasishwa na vijana.

Wengine wamegeukia kubashiri michezo mbalimbali kwa kuangalia dau linalowekwa, ndugu yangu nako huko usithubutu utamaliza pesa zako tu, kupatia timu zote hasa kwenye JACKPOT sio mchezo ndio maana wanaobashiri wanaweza kuwa 100000 lakini asipatikane hata mmoja, kwenye hii michezo hakuna cha odd ndogo wala kubwa wengi wanalia na faida inaend kwa yule aliyetengeneza mfumo huo ila nyie mnaliwa tu.

Ukija kwenye biashara zenye sura ya upatu kama forever na nyinginezo nazo hamna jipya chini ya jua, ninauzoefu nayo na nimeifanya simaanishi ni biashara mbaya bali uwezo wa kufanikiwa ni mdogo sana wala hatipaswi kudanganyana. Ni vema mtu unapomhamasisha ajue kwamba biashara hiyo ni nzuri ila pia ni ngumu sana kwa mfano unapewa bidhaa/virutubisho uuzie watu ili wanunue na kwa sababu utawaaminisha kwamba zitawasaidia halafu wao wananunua na haziwasaidii au unamuunganisha mtu kuingia kwenye biashara hiyo kwa zaidi ya Tsh210, 000/= Za kianzio ambapo akishaingia anawaza tu kuwa tajiri bila kujua kwamba wakati mwingine hata bidhaa alizopewa kwa kuanza nazo wakati mwingine hata hazipati wateja! Mwishowe unavunja urafiki naye na kuwa maadui,.

Ni heri sisi tubadilike na tujue biashara zinazoendelea mitandaoni zinamaliza na kukausha fedha tunazozitafuta kwa nguvu na jasho letu na hizo fedha zikiteketea huko tunabakia hatuna wa kumlaumu zaidi ya kuumia mioyoni mwetu tu.

Nawaomba ndugu zangu tufanye kazi kwa bidii na tuwe wabunifu kwa kutengeneza vyanzo sahihi vya fedha na usihadaike na kudanganywa kuingia kwenye biashara ya mtandaoni bila kuwa na elimu ya kutosha kwani huko unaweza kuishia kulia tu.

ASANTENI SANA.
Naupenda usemi huu wa kimombo 'If you do not know where you are going any road will take you there'
 
Back
Top Bottom