SoC01 Tahadhari: Biashara za mtandaoni ni chanzo cha umaskini

Stories of Change - 2021 Competition

Jurudyiza

Member
Jul 15, 2021
70
96
Mtoa mada ##JURUDYIZA##

Wapendwa hakuna jipya chini ya jua asilimia kubwa ni ubatili mtupu.

Kwa sasa watu wengi wanajikita kutafuta utajiri wa haraka bila kujua harakaharaka haina baraka Na ujue tu kwamba Sayansi na teknolojia kwetu Afrika bado inanufaisha wachache tena nao wananufaika kwa kuhadaa wengi wasiojua au wale wanaokurupuka kufanya maamuzi.

Biashara za mtandao kwa sasa zimewaliza wengi wanaotamani kufanikiwa zaidi kwa kutumia njia za mkato na biashara hizo ni hadaa sana na wao wanao zihubiri asilimia kubwa hawajanufaika bali nao ni walaibu tu wakiamini ipo siku watatoka tu mwishowe huwa hawasimulii tena hasara wanazozipata.

Ndugu zangu mimi ni mhanga mkubwa, nimefanya biashara mbalimbali japo si zote ila nakupa mfano wa chache nilizo na uzoefu.

Kwa ukweli wangu naamini mtaunga mkono kama kweli ninyi ni wakweli na uhalisia ni kwamba kwenye biashara za mtandao mifumo yake ni migumu kukutajilisha na huwezi kupata utajiri kiurahisi. Mfano wa biashara hizo ni kama zifuatazo:-

Forex na mfano wa hizo, hapa najua wapo wengi wanatamani kufanya biashara hizo na baadhi yao wanajigamba wana mafanikio makubwa, Du hapana nasema hapana! Naamini kabisa kati ya watu 100 wanaofanikiwa ni watu 3 hadi 5 na huo ni mtazamo wangu tu ila najua hata watu hao ni wengi sana na hii inaniuma sana.

Kwenye mfumo huo wa FX wanaofanikiwa naamini kabisa ni wale walioutengeneza mfumo huo wa biashara ukianzia na mifumo yao ya kufanyia biashara iwe MT4 au MT5 kute huko ni sehemu ya kuteketezea fedha.

Kwa mfano mtu anaweza kuweka USD 200 lakini ndani ya dakika 20 akawa amepata hasara ya hela yote sasa hiyo ni biashara kweli! Hapana mtamaliza hela zenu bure ni bora hiyo USD 200 zaidi ya TSH 400,000/= ukafanyia biashara nyingine au huu ni uongo? Hata biashara ya nyanya huwezi kupata hasara hiyo yote kwa mpigo ni biashara kweli hiyo au balaa!

Mimi naamini kabisa hakuna biashara ya kukupatia faida kwa mkato na ukawa tajiri zaidi ya kujituma na kuwa mbunifu katika biashara ndogo unayoanza nayo wewe mwenyewe kuliko hizi zinazohamasishwa na vijana.

Wengine wamegeukia kubashiri michezo mbalimbali kwa kuangalia dau linalowekwa, ndugu yangu nako huko usithubutu utamaliza pesa zako tu, kupatia timu zote hasa kwenye JACKPOT sio mchezo ndio maana wanaobashiri wanaweza kuwa 100000 lakini asipatikane hata mmoja, kwenye hii michezo hakuna cha odd ndogo wala kubwa wengi wanalia na faida inaend kwa yule aliyetengeneza mfumo huo ila nyie mnaliwa tu.

Ukija kwenye biashara zenye sura ya upatu kama forever na nyinginezo nazo hamna jipya chini ya jua, ninauzoefu nayo na nimeifanya simaanishi ni biashara mbaya bali uwezo wa kufanikiwa ni mdogo sana wala hatipaswi kudanganyana. Ni vema mtu unapomhamasisha ajue kwamba biashara hiyo ni nzuri ila pia ni ngumu sana kwa mfano unapewa bidhaa/virutubisho uuzie watu ili wanunue na kwa sababu utawaaminisha kwamba zitawasaidia halafu wao wananunua na haziwasaidii au unamuunganisha mtu kuingia kwenye biashara hiyo kwa zaidi ya Tsh210, 000/= Za kianzio ambapo akishaingia anawaza tu kuwa tajiri bila kujua kwamba wakati mwingine hata bidhaa alizopewa kwa kuanza nazo wakati mwingine hata hazipati wateja! Mwishowe unavunja urafiki naye na kuwa maadui,.

Ni heri sisi tubadilike na tujue biashara zinazoendelea mitandaoni zinamaliza na kukausha fedha tunazozitafuta kwa nguvu na jasho letu na hizo fedha zikiteketea huko tunabakia hatuna wa kumlaumu zaidi ya kuumia mioyoni mwetu tu.

Nawaomba ndugu zangu tufanye kazi kwa bidii na tuwe wabunifu kwa kutengeneza vyanzo sahihi vya fedha na usihadaike na kudanganywa kuingia kwenye biashara ya mtandaoni bila kuwa na elimu ya kutosha kwani huko unaweza kuishia kulia tu.

ASANTENI SANA.
 
Vizuri sana mdogo wangu kwa kujitambua mapema
jambo jema ni kwamba umepata maono mapema hiyo no faida nzuri sana

TANZANIA ukiwa mtu wa kujituma na kutochagua biashara kwa kutofuata mkumbo ni rahisi sana kupata mafanikio

kikubwa ufahamu fika uwezi ukaweka ela ndogo mtaji ukataka kupata faida kubwa utafeli sana au utaishia kuwa taperi km si kutaperiwa

mtoto wa mkulima mtaji ni nguvu zake mwenyewe na kwakuwa MUNGU amekujalia AFYA NJEMA NGUVU na UTIMAMU WA AKILI tumia vema fursa hizo muhimu kufikia mafanikio kabla havijapungua uwezo au kupotea kabisa
 
Vizuri sana mdogo wangu kwa kujitambua mapema
jambo jema ni kwamba umepata maono mapema hiyo no faida nzuri sana

TANZANIA ukiwa mtu wa kujituma na kutochagua biashara kwa kutofuata mkumbo ni rahisi sana kupata mafanikio

kikubwa ufahamu fika uwezi ukaweka ela ndogo mtaji ukataka kupata faida kubwa utafeli sana au utaishia kuwa taperi

mtoto wa mkulima mtaji ni nguvu zake mwenyewe na kwakuwa MUNGU amekujalia AFYA NJEMA NGUVU na UTIMAMU WA AKILI tumia vema fursa hizo muhimu kufikia mafanikio kabla havijapotea au kupungua
Asante sana Kaka yangu
 
Pamoja na hayo wahanga wakubwa ni vijana pamoja na wazee hasa wataafu ambao hudanganywa kwamba wataongezea pension yao lakini kinachofuatwa ni kulizwa tu.
 
Mkuu forex wengi mliivamia kwa kutokuijua!

Siri moja inabidi ujue forex ni biashara ya wenye hela ( Full Pocketers Bussiness) ... Kama wewe una hela ya kudunduliza lazima ujue ni namna gani utaweza kusustain.

Siri nyingine nakuibia forex huwezi kuimaster kwa kufundishwa. Narudia Tena forex huijui kwa kufundishwa. Forex utaielewa kwa wewe kujifunza na kuwa creative Hadi utakapoona Matokeo chanya. Najua hunielew ila kaa chini utafakari. mengi mnayofundishwa kuhusu forex ni asilimia chache Sana ndio uhalisia.

Uhalisia wa forex unatafutwa na wewe binafsi.

Funzo: katika fursa yoyote iwe kilimo , ufugaji , forex n.k ... Usiingie au kufanya kwa kusikia habari kwa watu. Kuna watu walivamia kilimo na kupoteza Zaid ya mamilion.

Taarifa sahihi huzipati kwa kusikia juu juu. Spend muda kutafuta taarifa kwa Jambo lolote unalotaka kufanya .

Asante.
 
Nakumbuka kuna mdogo angu flan hv yupo IFM pale ndo alikuwa kila wiki tukionana mara Forex mara Bitcoin bas nikamuangalia na kumsikiliza mwisho nikamwambia bro mi MWENYEKITI WA BARAZA LA WAZEE hayo mambo yenu vijana mi siamini kabisa hivyo vitu. Even though I am around early 20's hii ni kama warning sign kwangu

Nikamuona hayuko Pleased na jibu langu bas nikamwambia kama wewe unaamin Take risk then gain advantage! Ila usisahau Shortcut is a wrong cut!
Bas akachukua Take risk then gain advantage! But haikujibu iliyotoa majibu ilikuwa Shortcut is a wrong cut!

So sad kila nikikumbuka alipoteza kama tsh 500k na maisha ya chuo yalivyo nilimhurumia kweli nikamsaidia nusu hasara 250k tokea siku hiyo ameomba kad ya kujiunga na BARAZA LA WAZEE TZ
 
Mtoa mada ##JURUDYIZA##

Wapendwa hakuna jipya chini ya jua asilimia kubwa ni ubatili mtupu.

Kwa sasa watu wengi wanajikita kutafuta utajiri wa haraka bila kujua harakaharaka haina baraka Na ujue tu kwamba Sayansi na teknolojia kwetu Afrika bado inanufaisha wachache tena nao wananufaika kwa kuhadaa wengi wasiojua au wale wanaokurupuka kufanya maamuzi.

Biashara za mtandao kwa sasa zimewaliza wengi wanaotamani kufanikiwa zaidi kwa kutumia njia za mkato na biashara hizo ni hadaa sana na wao wanao zihubiri asilimia kubwa hawajanufaika bali nao ni walaibu tu wakiamini ipo siku watatoka tu mwishowe huwa hawasimulii tena hasara wanazozipata.

Ndugu zangu mimi ni mhanga mkubwa, nimefanya biashara mbalimbali japo si zote ila nakupa mfano wa chache nilizo na uzoefu.

Kwa ukweli wangu naamini mtaunga mkono kama kweli ninyi ni wakweli na uhalisia ni kwamba kwenye biashara za mtandao mifumo yake ni migumu kukutajilisha na huwezi kupata utajiri kiurahisi. Mfano wa biashara hizo ni kama zifuatazo:-

Forex na mfano wa hizo, hapa najua wapo wengi wanatamani kufanya biashara hizo na baadhi yao wanajigamba wana mafanikio makubwa, Du hapana nasema hapana! Naamini kabisa kati ya watu 100 wanaofanikiwa ni watu 3 hadi 5 na huo ni mtazamo wangu tu ila najua hata watu hao ni wengi sana na hii inaniuma sana.

Kwenye mfumo huo wa FX wanaofanikiwa naamini kabisa ni wale walioutengeneza mfumo huo wa biashara ukianzia na mifumo yao ya kufanyia biashara iwe MT4 au MT5 kute huko ni sehemu ya kuteketezea fedha.

Kwa mfano mtu anaweza kuweka USD 200 lakini ndani ya dakika 20 akawa amepata hasara ya hela yote sasa hiyo ni biashara kweli! Hapana mtamaliza hela zenu bure ni bora hiyo USD 200 zaidi ya TSH 400,000/= ukafanyia biashara nyingine au huu ni uongo? Hata biashara ya nyanya huwezi kupata hasara hiyo yote kwa mpigo ni biashara kweli hiyo au balaa!

Mimi naamini kabisa hakuna biashara ya kukupatia faida kwa mkato na ukawa tajiri zaidi ya kujituma na kuwa mbunifu katika biashara ndogo unayoanza nayo wewe mwenyewe kuliko hizi zinazohamasishwa na vijana.

Wengine wamegeukia kubashiri michezo mbalimbali kwa kuangalia dau linalowekwa, ndugu yangu nako huko usithubutu utamaliza pesa zako tu, kupatia timu zote hasa kwenye JACKPOT sio mchezo ndio maana wanaobashiri wanaweza kuwa 100000 lakini asipatikane hata mmoja, kwenye hii michezo hakuna cha odd ndogo wala kubwa wengi wanalia na faida inaend kwa yule aliyetengeneza mfumo huo ila nyie mnaliwa tu.

Ukija kwenye biashara zenye sura ya upatu kama forever na nyinginezo nazo hamna jipya chini ya jua, ninauzoefu nayo na nimeifanya simaanishi ni biashara mbaya bali uwezo wa kufanikiwa ni mdogo sana wala hatipaswi kudanganyana. Ni vema mtu unapomhamasisha ajue kwamba biashara hiyo ni nzuri ila pia ni ngumu sana kwa mfano unapewa bidhaa/virutubisho uuzie watu ili wanunue na kwa sababu utawaaminisha kwamba zitawasaidia halafu wao wananunua na haziwasaidii au unamuunganisha mtu kuingia kwenye biashara hiyo kwa zaidi ya Tsh210, 000/= Za kianzio ambapo akishaingia anawaza tu kuwa tajiri bila kujua kwamba wakati mwingine hata bidhaa alizopewa kwa kuanza nazo wakati mwingine hata hazipati wateja! Mwishowe unavunja urafiki naye na kuwa maadui,.

Ni heri sisi tubadilike na tujue biashara zinazoendelea mitandaoni zinamaliza na kukausha fedha tunazozitafuta kwa nguvu na jasho letu na hizo fedha zikiteketea huko tunabakia hatuna wa kumlaumu zaidi ya kuumia mioyoni mwetu tu.

Nawaomba ndugu zangu tufanye kazi kwa bidii na tuwe wabunifu kwa kutengeneza vyanzo sahihi vya fedha na usihadaike na kudanganywa kuingia kwenye biashara ya mtandaoni bila kuwa na elimu ya kutosha kwani huko unaweza kuishia kulia tu.

ASANTENI SANA.
Forex ni biashara ya matajiri ....
ww kapuku uliingia kufanya nini huko....
hata kwowladge huna....
unaweka dola 200 ndani ya dk tano umeliwa ww hujui.....
 
Unaliwa tu halafu unajifariji utapata mbeleni kumbe hujui kama hujui.
JamiiForums409639654.jpg

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Nakumbuka kuna mdogo angu flan hv yupo IFM pale ndo alikuwa kila wiki tukionana mara Forex mara Bitcoin bas nikamuangalia na kumsikiliza mwisho nikamwambia bro mi MWENYEKITI WA BARAZA LA WAZEE hayo mambo yenu vijana mi siamini kabisa hivyo vitu. Even though I am around early 20's hii ni kama warning sign kwangu

Nikamuona hayuko Pleased na jibu langu bas nikamwambia kama wewe unaamin Take risk then gain advantage! Ila usisahau Shortcut is a wrong cut!
Bas akachukua Take risk then gain advantage! But haikujibu iliyotoa majibu ilikuwa Shortcut is a wrong cut!

So sad kila nikikumbuka alipoteza kama tsh 500k na maisha ya chuo yalivyo nilimhurumia kweli nikamsaidia nusu hasara 250k tokea siku hiyo ameomba kad ya kujiunga na BARAZA LA WAZEE TZ
Kwa uhalisia hizi biashara zinaushawishi sana ila mwisho wa siku ni vilio, mimi nimejitahidi sana kuzifanya nikijua ni kuendana na teknolojia sijwahi pata faida yoyote zaidi ya hasara, hata walionihimiza na kunishawishi wengi wao hawana hamu na hizo biashara.
 
Mbali na kushiriki mimi naamini mada zinazotolewa si za kupuuza kwani ukizisoma utapata lolote la kukusaidia ndugu yangu hatushiriki ili kushinda tu bali hata kuelimishana.
 
Mkuu forex wengi mliivamia kwa kutokuijua!

Siri moja inabidi ujue forex ni biashara ya wenye hela ( Full Pocketers Bussiness) ... Kama wewe una hela ya kudunduliza lazima ujue ni namna gani utaweza kusustain.

Siri nyingine nakuibia forex huwezi kuimaster kwa kufundishwa. Narudia Tena forex huijui kwa kufundishwa. Forex utaielewa kwa wewe kujifunza na kuwa creative Hadi utakapoona Matokeo chanya. Najua hunielew ila kaa chini utafakari. mengi mnayofundishwa kuhusu forex ni asilimia chache Sana ndio uhalisia.

Uhalisia wa forex unatafutwa na wewe binafsi.

Funzo: katika fursa yoyote iwe kilimo , ufugaji , forex n.k ... Usiingie au kufanya kwa kusikia habari kwa watu. Kuna watu walivamia kilimo na kupoteza Zaid ya mamilion.

Taarifa sahihi huzipati kwa kusikia juu juu. Spend muda kutafuta taarifa kwa Jambo lolote unalotaka kufanya .

Asante.
Those who know don't speak and those who speak don't know.

Many can talk the talk but few can walk the walk when a real money is on line.
Forex hata mie namkatalia.
Ni ngumu Sana na ulichosema ni ukweli
We're created for short time survival or gratification.
 
Inawezekana ukawa sahihi lakini kujifunza biashara mpya wewe mwenyewe ni ngumu na inawezekana kati ya watu 100 wakatokea watu watatu wenye uwezo huo, shida sio elimu ya biashara watu wametumia hizi biashara kama njia mkato ya kufikia kilele cha mafanikio, na wengi wao wakishasimuliana hutumbukia moja kwa moja na hao ndio wengi tuliao ila wanaofanikiwa ni wachache tena shuhuda zao hazipo wazi, labda wewe kama ulishafanikiwa weka ushuhuda wako tukujue kwamba haupo level yetu.
 
Sikia ishu Iko Ivi wengi wanakimbilia kufundisha,kuuza kozi,kuuza signals,kuwakamata newbies,
Kufanya akaunti management Ila kiukweli hao wamechezea za uso mkuu.

Hii ishu ni legitimate Ila ni ngumu.
Is not easy but it's simple.
Sijafanikiwa so Sina shuhuda.
Ila ni ngumu mkuu sio suala la kitoto mpaka kufikia kileleni
 
Back
Top Bottom