Tahadhari abiria wa mabasi ya Happy Nation

Tahadhari abiria wa mabasi ya Happy Nation

Pole sana mkuu....asante kwa kutujuza hilo sitayapanda hayo magari wala kuwasikiliza nikifika stand....hao dawa ni kuwatangaza kila kona...
 
Ndio tabia yao.wameianzisha karibia miaka sasa.
 
hivi zile happy nation balotel (mtoto mtukutu) na sauti ya manka zipo wapi?
 
Nilipata shida kama yako kwa princess muro, watu wa mabasi ni wahuni sana. Pole sana mkuu.
 
pole sana, next time chukua kitu cha new force.
 
hapo lazima madumu ya maji yawepo kwenye buti, yani poleni sana uwa inakera na safari ndefu kama hiyo. Mungu awasaidie mfike salama, maana na hiyo njia.
 
Me gari yangu New force 2 kama naenda songea au mbeya tunduma
 
Kampuni ya Happy Nation imeamua kwa makusudi kutumia mbinu chafu kutengeneza pesa toka kwa abiria kwa kuwakatia tiketi kwa bei ya luxury na kisha kuwapandisha abiria kwenye mabasi machakavu ya kampuni zingine ya bei rahisi huku happy nation wakila cha juu. Uchafu huu hufanyika huku uongozi wa kituo cha mabasi ubungo ukiwa unajua bila kuchukua hatua yoyote. Uhuni huu hufanyika hasa kwa safari za Dar - Mbeya ambapo abiria hukatiwa tiketi kwa sh.45, 000/ kisha hupakiwa kwenye mabasi mabovu ambayo pengine yasingepata abiria hata kwa 20, 000/- huku uongozi wa kampuni ya happy nation ukijifanya ni dharura imetokea kumbe ni biashara haramu. Ndugu zangu kuweni makini na kampuni hii ili muepuke usumbufu ulionikuta.

Mkuu nakupongeza kwa kuwa mvumilivu.Ningekuwa ni mimi safari ingekuwa basi manaake ningekekuwa nimeshang'oa mtu jino fasta!
 
Mkuu nakupongeza kwa kuwa mvumilivu.Ningekuwa ni mimi safari ingekuwa basi manaake ningekekuwa nimeshang'oa mtu jino fasta!

Duh mkuu ningeng'oa mtu jino ningekuwa urafiki saa hii
 
Back
Top Bottom