Tahadhari abiria wa mabasi ya Happy Nation

Tahadhari abiria wa mabasi ya Happy Nation

frakitosho

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2012
Posts
802
Reaction score
256
Kampuni ya Happy Nation imeamua kwa makusudi kutumia mbinu chafu kutengeneza pesa toka kwa abiria kwa kuwakatia tiketi kwa bei ya luxury na kisha kuwapandisha abiria kwenye mabasi machakavu ya kampuni zingine ya bei rahisi huku happy nation wakila cha juu.

Uchafu huu hufanyika huku uongozi wa kituo cha mabasi Ubungo ukiwa unajua bila kuchukua hatua yoyote. Uhuni huu hufanyika hasa kwa safari za Dar - Mbeya ambapo abiria hukatiwa tiketi kwa sh.45, 000/ kisha hupakiwa kwenye mabasi mabovu ambayo pengine yasingepata abiria hata kwa 20, 000/-

Huku uongozi wa kampuni ya happy nation ukijifanya ni dharura imetokea kumbe ni biashara haramu. Ndugu zangu kuweni makini na kampuni hii ili muepuke usumbufu ulionikuta.
 
Kifupi ndugu zangu jihadharini na.
HAPPY NATION
PRINCESS MURO
ama utallala njiani au utalipa cha juu kwa huduma mbovu.
 
Haya mabasi muda sana liniacha kupanda ukitoka lazima uchane nguo pia na simba mtoto ni vxuma tupu niliwai chana tshirt yangu mpya tena ilikuwa mara ya kwanza kuivaa
 
Hata mi nshawah kufanyiwa huu mchezo,nilikata ticket mpka tunduma nulivofika mbeya wakanifaurisha kwenye costa mbovu,dah nusura niue mtu maana roho yangu iliumia kwelkweli
 
Mkuu unajua hawa jamaa mi nlikuwa siwaelewi kabisa...mana kuna siku kweli nlikata tiketi....asubuhi nafika ubungo gari walonidirect la ovyo kweli yani...hawa jamaa wahuni kweli,wana gari lao wanalita HAI,kumbe huwa haiendi mby pambafu sana watu hawa,ngoja tuwaexpose everywhere.....
 
Wameniharibia sana siku yangu ndio maana nikaona nisikae kimya niwajulishe nanyi wanajf wenzangu muwaepuke kama ukoma
 
Hata mi nshawah kufanyiwa huu mchezo,nilikata ticket mpka tunduma nulivofika mbeya wakanifaurisha kwenye costa mbovu,dah nusura niue mtu maana roho yangu iliumia kwelkweli

Pole sana ndugu yangu.
 
Wameniharibia sana siku yangu ndio maana nikaona nisikae kimya niwajulishe nanyi wanajf wenzangu muwaepuke kama ukoma

Mkuu ndo upo kwenye safari nn,duh pole sana unaweza ukatamani uwanyonge,afu hao makonda na dereva wanajikuta wastarabu kweli yani....mkuu don't panic
 
Naona abiria karibu wote wanalalama. Hii kampuni balaa
 
Haya mabasi muda sana liniacha kupanda ukitoka lazima uchane nguo pia na simba mtoto ni vxuma tupu niliwai chana tshirt yangu mpya tena ilikuwa mara ya kwanza kuivaa

Pole sana kiongozi
 
Na hapo hata ukienda polisi hawachukuliwi hatua, mko wapi labda Sumatra wanaweza kufuatilia skendo hii maana nao wanaona hizi thread. Elezea mko wapi
 
Nami ishanitokea, nilikata tiketi ya Happy Nation asubuhi nikapandishwa Hai express
 
Mkuu ndo upo kwenye safari nn,duh pole sana unaweza ukatamani uwanyonge,afu hao makonda na dereva wanajikuta wastarabu kweli yani....mkuu don't panic

Ndio niko safarini ndugu yangu nashukuru kwa kunipa moyo.
 
Na hapo hata ukienda polisi hawachukuliwi hatua, mko wapi labda Sumatra wanaweza kufuatilia skendo hii maana nao wanaona hizi thread. Elezea mko wapi

Tumepandishwa kwenye mkweche wa Hai express seat chafu kwelikweli. Tunakaribia mlandizi
 
Tumepandishwa kwenye mkweche wa Hai express seat chafu kwelikweli. Tunakaribia mlandizi

Gari lenyewe siti zimebanana kweli cjui ni 3 by 3....iyo siti karibia na dereva ndo usiombe....ovyo kwanza ina heat kinoma
 
Back
Top Bottom