Tahadhali kuu katika xmas

Tahadhali kuu katika xmas

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,141
Reaction score
951
Wakuu Mimi na Familia yangu tunawatakia Xmas njema pamoja na familia zetu.

Ila mchukue tahadhali kuu katika kipindi chote cha Sherehe, mjihadhari na ajali na matukio mengine yanayoweza kuficha ikiwemo pombe na ngono zembe. Kamwe msimwamini mtu, eti kama wameshindwa kudhibiti ubora wa kondom na wale wa TFDA wakashindwa kudhibiti ARV na kusababisha wale ambao walitumia Kondom feki wakapata maambukizi, Je, matukio mengine makubwa ikiwemo kuzuia wananchi wasikatane vichwa na kunyofoana viungo kwa ajili ya biashara za kishirikina wataweza ??

Hii ndo Bongo wakuu, jambazi anakupora 150M, unaomba msaada wa Polisi, wanakuja kukusaidia, lakini wakiokoa zigo la hela wanagawana pasupasu na mhanga wa tukio anaachwa solemba.....nini kifuatacho??


...MLINZI MKUBWA WA MAISHA YAKO NA MAISHA YA MWENZIO NI WEWE MWENYEWE.....





May the good times and treasures of the present
become the golden memories of tomorrow.
Wishing you lots of love, joy and happiness.
Merry Christmas!
​
 
Ur wrong,Mungu asipoulinda mji aulindae afanya kazi bure


Mkuu hiyo ya Zaburi ya 127 yakupaswa uielewe tafsiri, pasipo kujongea mbele za Bwana kwa kushika maandiko hakuna atakae kulinda. Ni wewe mwenyewe wapasa kujilinda kwa kumwomba Mwenyeenzi Mungu akupe ulinzi. Zingatia kuchukua tahadhari kwa kila jambo ujilinde kwa neno pia:

Zaburi 127

1 Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.
2 Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi.
3 Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, Uzao wa tumbo ni thawabu.
4 Kama mishale mkononi mwa shujaa, Ndivyo walivyo wana wa ujanani.
5 Heri mtu yule Aliyelijaza podo lake hivyo. Naam, hawataona aibu Wanaposema na adui langoni.
 
Wengine watasoma tahadhari yako baada ya kumaliza hangovers za chrismas sijui kama kuna tamaa kwa hao!
 
Back
Top Bottom