Tahadhali: Kumbukeni kuna maisha baada ya chuo

bhachu

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
6,704
2,000
Kwani na wewe ushawahi kutoa kipochi manyoya unapo omba kazi eti?
 
perfect Combo

Member
Sep 4, 2016
37
125
Ukimaliza form six na kubahatika kupata chuo utafurahi saaana, Wengi kipindi cha kuomba Nafasi za vyuoni hudanganyana kuwa kozi hii mshahara wake si chini ya million .... MTU huyu akifika chuo kipindi chote cha maisha ya chuo anakuwa na irrelevant dreams baada ya kumaliza chuo...

Kimbembe ni pale unapomaliza chuo.... Guys maisha ni magumu saaaaaana kama ni fresh graduates ... Naomben msome kitabu cha rich dad, poor dad kitawajenga sana kifikra kuhusu elimu na ajira na kutokuwa na ndoto za kuajiriwa tu
ndo zao hizi..mtu anasoma Bcom BANKING anawaza kupiga hela..mtu anasoma PEroleum anawaza kupiga hela..ngoja amalize chuo sasa.....
 
perfect Combo

Member
Sep 4, 2016
37
125
Kwani na wewe ushawahi kutoa kipochi manyoya unapo omba kazi eti?
noo sijawahi...ila nasikitika saiv inbox yangu kumejaa PM za wanaume wanafikiri nina njaa....MEN ARE STUPID..sijawah kuona watu wanapenda ngono kiasi hiki...mie nimeandika hii thread kuelemisha,,people are thinking am seeking for employment
 
kukutia

Member
Sep 26, 2016
24
45
Habari wana JF wote mnaosubira kwenda chuo....

wakati tunapofanya application za kwenda chuo hasa kwa wale wanaosoma course ambazo hazina ajira ya moja kwa moja . Nitajaribu kuoredhesha baadhi ya course ambazo ajira zake ni ngumu.

1.Non education courses
2.Engineering karibu zote kwa sasa ajira yake ni ngumu (NAJUA MTABISHA)
3.education zote ya arts japo sina uhakika sana

TAHADHALI.

kama hauna direction kabisa na unatoka familia duni kuwa makini katika kuchagua course ya kwenda kusoma DEGREE...kuna watu wanaamini kuwa DEGREE yoyote ina ajira lakini amin nakuambia mtaani kuna mengi sana na elimu kubwa ndiyo iko mtaani ,,kipindi unapoenda chuoni unaweza kujiona kuwa ndiyo umefauru maisha MAISHA BAADA YA CHUO UNAWEZA KUJIFUKIA SHIMONI...

Kuna watu mtaani wamesoma computer engenering tena wamesomea INDIA lakin hawana kazi mpaka sasa na mbaya zaidi wamesomeshwa na serikali...kuna watu wamesoma petroleum ,,wengine wamesoma biomedical lakin wapo mtaani....kuna wengine wanakurupuka kuchagua course mpya eti wakijua kuwa ajira ni uhakika lakini kinachotokea baada ya chuo tumwachie MUNGU tu...na kuna wengine wanajipa moyo eti hii course inatolewa na vyuo viwili tu TZ nzima....

Najua kuna wengine mtapata sana sapu na kuna wengine hamtapata sapu ...baada ya chuo nawakaribisha mtaani na elimu ya huku ni zaidi ya huko chuoni mnakoenda ..tunapokuwa chuoni huwa na ndoto nyingi sana ila tunaporudi mtaani maisha hubadilika....

Unaweza kupagawa ..mtaani watakusema sana eti vyeti vyako vibovu....una apply kazi mpaka unachoka kampuni nyingi zinahitaji watu wenye uzoefu..RUSHWA ya ngono...wasichana wenzangu ndiyo uwa wanaachia,,,,wanavua nguo ili wapate kazi....ELIMU kubwa ya maisha ipo huku mtaani..imewakuta wengi wenye degree,,diploma na hata cheti..waungwana husema nawmachia MUNGU.....

Upo chuoni unawaza kumiliki ALTEZA lakin baada ya chuo unaishia kutembea na bahasha miaka mitano hujapata kazi..

WENGINE wanatuaminisha kujiajiri lakn amini nakuambia kujiajiri kwa TZ hii ni ngumu sana....

ALL THE BEST WADOGO ZANGU....KUWENI MAKINI...

poleni sana kwa wale mtakaodisco.....lazima wapo wa kudisco hivyo kuweni makini huko chuoni..........mtaa una elimu kubwa malecture ni wanajamii wenzako......
Umenena vyema
 
NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,895
2,000
Namkumbuka Lecturer wangu wakati nasoma Chuo tena kwa heshima namtaja jina lake anaitwa VENANCE SHILLINGI alituambia kuwa, sasa mnamaliza masomo yenu mnarudi nyumbani, huko hakuna boom tena, mtabadilisha bahasha za kubebea vyeti vyenu maana zitafika mahali zinachafuka, na mbaya zaidi hapa Chuoni naamini karibia wote mnasabuni za kuogea na kufulia, lakini sasa mnakwenda nyumbani, kitakachotokea ni kwamba sabuni ya kipande ya kufulia ndio hiyo hiyo utakayoogea. Nawaomba mkiwa huko mtulie, msichanganyikiwe. Kila la Kheri. Alivyomaliza kutuambia hayo maneno akasema haya "sasa nawapa hizi notes mkasome zitawasaidia zinahusu "interview"

Ahsante Mwalimu VENANCE SHILLINGI barikiwa popote ulipo baba
 
aliona mbali sana...vijana wengi tunafikiria maisha ya chuo kuliko maisha baada ya chuo
 
Jitu Refu

JF-Expert Member
Sep 9, 2016
827
1,000
Ajira zisizokuwa na longolongo:-
1.ualimu primary na sekondary kwa science
2.upolisi
3.afya lakini nursing kwa certificate inasumbua kidogo ila huwez kosa pa kujishikiza
 
SODOKA

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,664
2,000
ha haaaaaa....namsubira sodoka accoment hapa
he heee nipo ....mie naona vijana wengi tunapofauru vizuri tunafikiria maisha ya chuo zaidi kuliko maisha baada ya chuo....a well quoted view ..Perfect Combo umenikuna kumoyo..
 
SODOKA

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,664
2,000
Ajira zisizokuwa na longolongo:-
1.ualimu primary na sekondary kwa science
2.upolisi
3.afya lakini nursing kwa certificate inasumbua kidogo ila huwez kosa pa kujishikiza
upolisi ndo WAPO smart zaid ..yaan unatoka chuo unapelekwa na bus kituoni kuanza kazi Mara moja
 
ney kush

JF-Expert Member
Feb 16, 2012
1,313
2,000
noo sijawahi...ila nasikitika saiv inbox yangu kumejaa PM za wanaume wanafikiri nina njaa....MEN ARE STUPID..sijawah kuona watu wanapenda ngono kiasi hiki...mie nimeandika hii thread kuelemisha,,people are thinking am seeking for employment
ugumu dada sio stupidity
 
Senior Boss

JF-Expert Member
Aug 19, 2011
3,309
2,000
Life la kitaa bana lisikie tu.

Baada ya kumaliza masomo na kuingia in the employment world.....i was still a young man nd not too experienced with the whole life struggle in general.

Ila few years working i met two people both corporate clients....these people changed my life nd thinking big tym. Yan hangin wit them kulinifanya kuzinduka usingizini na nikaanza kuwa mjanja mjanja .

Hela nyingi zipo humu humu mtaani tuliza akili and hang around the right people. Usikae na mtu mjinga.

Its like everyone wants to go to university and wants to work in TRA, Banks, Government et al nd still more are enrolling each year and thats kynda funny/crazy.
 
perfect Combo

Member
Sep 4, 2016
37
125
Life la kitaa bana lisikie tu.

Baada ya kumaliza masomo na kuingia in the employment world.....i was still a young man nd not too experienced with the whole life struggle in general.

Ila few years working i met two people both corporate clients....these people changed my life nd thinking big tym. Yan hangin wit them kulinifanya kuzinduka usingizini na nikaanza kuwa mjanja mjanja .

Asikuambie mtu hela nyingi zipo humu humu mtaani tuliza akili and hang around the right people.
yeah,,,,respect all classes of people
 
Adolf Hitler Jr

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
343
250
Tatizo letu/lenu vijana wa sasa tumekariri maisha . Tunasoma bila kuangalia mazingira yetu na jinsi nchi yetu ilivyobadilika. kusoma kwa kufikiria kuajiliwa ni vibaya kwa kozi yoyote ile (ntaelezea baaadaye ). kwa nchi yetu ilivyosasa naona nchi yetu, viongozi wetu walifanya jambo la busara kwa mtazamo wangu la kufanya nchi yetu iwe na wasomi wengi ndo maana zikaibuka hizi BRN n.k ilimradi watu wengi waweze pata nafasi ya kufika vyuoni . sasa wewe kama kijana unashindwa kutambua hali halisi ya nchi yako ya kwamba hivi sasa wasomi ni wengi nchini kwetu kama ilivyo nchi nyingine mf; Nigeria hata majirani zetu Kenya. Hivi sasa hali imebadilika vijana wa makamo yangu 20's na n.k fatilia hizi nchi nilizokutolea mfano uone wenzetu walivyotuacha mbali katika kuchangamkia fursa nyingine zilizo ndani ya field walizosoma na hata ambazo hawajazisomoa iwe ni ndani ya nchi ama nje ya nchi , ni wakati wa vijana kubadilika na kutafuta fursa kwa nguvu sio kuishia kulaumu (msomi kukaa kulaumu mda wote ni kujiabisha) Waacheni wanasiasa wafanye kazi ya kulaumu - THEY ARE PAID TO DO SO . FURSA ZIPO NYINGI XANA !!!!!!!!!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom