Tahadhali: Kumbukeni kuna maisha baada ya chuo

Tahadhali: Kumbukeni kuna maisha baada ya chuo

Tatizo letu/lenu vijana wa sasa tumekariri maisha . Tunasoma bila kuangalia mazingira yetu na jinsi nchi yetu ilivyobadilika. kusoma kwa kufikiria kuajiliwa ni vibaya kwa kozi yoyote ile (ntaelezea baaadaye ). kwa nchi yetu ilivyosasa naona nchi yetu, viongozi wetu walifanya jambo la busara kwa mtazamo wangu la kufanya nchi yetu iwe na wasomi wengi ndo maana zikaibuka hizi BRN n.k ilimradi watu wengi waweze pata nafasi ya kufika vyuoni . sasa wewe kama kijana unashindwa kutambua hali halisi ya nchi yako ya kwamba hivi sasa wasomi ni wengi nchini kwetu kama ilivyo nchi nyingine mf; Nigeria hata majirani zetu Kenya. Hivi sasa hali imebadilika vijana wa makamo yangu 20's na n.k fatilia hizi nchi nilizokutolea mfano uone wenzetu walivyotuacha mbali katika kuchangamkia fursa nyingine zilizo ndani ya field walizosoma na hata ambazo hawajazisomoa iwe ni ndani ya nchi ama nje ya nchi , ni wakati wa vijana kubadilika na kutafuta fursa kwa nguvu sio kuishia kulaumu (msomi kukaa kulaumu mda wote ni kujiabisha) Waacheni wanasiasa wafanye kazi ya kulaumu - THEY ARE PAID TO DO SO . FURSA ZIPO NYINGI XANA !!!!!!!!!!!
yaan nature ya fikra zetu ni kuajiriwa hata wewe umeandika tu haya maneno umebezi kisiasa zaidi....ukigusia kujiajiri lazima utasema kufuga kuku
 
Mimi sio mwanasiasa ila nchi yetu ilivyo kila kitu kinahusiana na siasa. Though it's my hope itabadilika
 
Kwa hali ilivyo heshima itarudi kwa mwali hasa wa sayansi! UDSM wamechukuwa wanaochukua ualimu wa sayansi kuanzia pointi 13.5 hadi 6 mwisho! Kwa waalimu wa sanaa wamechukua kuanzia pointi 13.5 hadi 9 mwisho! Huu ni ufaulu mkubwa sana!
Enzi za kusema wanaofeli ndo wanakwenda ualimu zimekoma kwa kasi!
 
Halafu wimbo wa kujiajiri ni rahisi kuuimba lakini kuucheza ni shughuli!!!!
 
Just emagine umesoma BAED utajiajiri kwa lipi litakalokuingizia kipato kutokana na elimu uliyopata!!
Usimlaumu mtu huyu anapolalamika kuajiriwa ilihali hana hata sehemu ya kuweka bond achukue mkopo wa kujiajiri
 
Kujiajiri Tz ni rahisi sana maana Tz ni nchi Ambaye bado ina unexploited opportunities nying sana. Tatizo ubishoo ndyo unawasumbua vijana wa Tz.
Hivi Mkuu wewe umejiajiri au umeajiriwa?
Usijekuwa kama yule Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa aliyetumbiliwa na baba Jesca akawa anaomba huruma ya mkuuwa nchi wakati yeye alikuwa akiwahubiria vijana wajiajiri.
So msiwe mnawapa watu matumani amabayo hata wewe ungeshauriwa ungekiri kuwa huu ni ushauri hewa.
 
Maneno yako ni mazur kwan yanakumbusha maisha baada ya chuo, ni vyema sasa kusoma huku ukijua nikimaliza naenda mtaani kupambana na kitaa, kitaa sio kubaya ila itategemea unakujaje kitaani, ishu za kufanya kutumia elimu yako zipo na zile usizo tumia elimu yako nazo zipo, mi nilipo maliza chuo nilianza kuwa kondakta wa daladala kama sio jasir wa maisha huwez nikapanda cheo nikawa dereva wa roli, mpaka nilipo ajiriwa, ila huku kitaa usije na Yale mawazo yako kuwa utapata kazi kwa haraka hivyo kama si mchakarikaji.
 
Siku zote mtu ukisoma kwa malengo fulani kwa level ya degree na kuwa vizuri kwenye degree uliyo somea huwezi jutia, lazima ipo siku tu utafaidika na ulicho somea "Kuteseka ni kwa muda tu".
 
Back
Top Bottom