Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote

Bemendazole

JF-Expert Member
Nov 14, 2020
2,361
5,879
Ndugu wana JF wenzangu, kulingana na andiko hilo linalopatikana kwenye kitabu kitakatifu cha Biblia,
Napenda kuchukua fursa hii kumuomba radhi mtu yeyote ambaye nitakuwa nimemkwaza kwa namna moja ama nyingine.

Awe mwanasiasa, kwenye chama na Serikali wale niliowahi kufanya nao kazi au kushirikiana nao kwa namna moja au nyingine au wale niliowahi kuwa nao kwenye mahusiano huko nyuma.

Zaidi zaidi kumuomba msamaha Mungu baba endapo kwa mawazo, kwa maneno au kwa vitendo nitakuwa nimemkosea.

Nasema hivi kwa kuwa nimegundua kuwa kuna baadhi ya vitu vyangu kwenye maisha ya kawaida haviendi sawa na pengine nadhani ni kwa vile siko sawa na baadhi ya watu au kundi fulani.

Naombeni mniwie radhi, yaliyopita yaishe na maisha yaendelee kama kawaida.

Ahsanteni wote kwa kuitikia wito huu.

Sitokuwepo hewani kwa kipindi kifupi nikijitahidi kuweka mambo yangu kwenye mstari. Yakisha kaa sawa, tutajumuika tena kwa amani na upendo.

Mimi mwenzenu, Bemendazole.
 
Back
Top Bottom