Orketeemi
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 4,918
- 12,124
MTAZAMO WANGU KUHUSIANA NA WIMBO WA IM SORRY JK.
________________________________
Kufuatia msanii Nick Mbishi kuitwa BASATA kwa kile kinachoelezwa kwamba kuhojiwa kutokana na nyimbo yake ya Im sorry JK kumekuwa na malumbano ya hoja hususani kuhusiana na kwamba je ni kweli tunamkumbuka na kumtaka radhi JK?
Kuna baadhi ya wadau wa CCM wanahoji kwamba JK Yule yule aliyeitwa dhaifu kila mahala Leo hii were sorry for him. JK yule yule tuliyesema anawachekea mafisadi?
Ukweli ulio wazi ni kwamba si Nikki Mbishi bali wengi tu tunasema Were sorry JK, hii haimaanishi kwamba JK hakuwa dhaifu la hasha wala haimaanishi kwamba JK hakuwa mpole Kwa mafisadi.
Tunasema I'm sorry JK kutokana na huyu tuliyenaye kutojua maana hasa ya kubadilishana uongozi. Yeye anachoona na kukumbuka ni udhaifu wa JK tu lakin hafaham kwamba unapochukua uongozi kutoka Kwa aliyepita ni jukumu lako kuwa makini sana ili usirudie makosa ya aliyepita lakini umakini wa ziada unahitajika ili usiharibu yale mazuri ambayo mtangulizi wako alikuwa akiyafanya.
JK kama binadam yeyote hakuwa amekamilika lakini Kwa bahati nzuri alikuwa na mengi mazuri na ndio maana zaidi ya kuitwa dhaifu na mpole hakuwahi kupigiwa kelele kuhusu demokrasia, hakulaumiwa kuhusu ukosefu wa ajira, JK hakukemewa kuhusu Ukurupukaji katika utamkaji na utendaji. Kuna maeneo mengi JK alikuwa smart.
Tulitegemea wewe tunayekuchagua sasa kutokuwa dhaifu kama JK lakini pia kutoharibu yale mazuri aliyokuwa anayafanya JK. Katika hili hata yeye JK alipokuwa kwenye hafla moja pale UDSM alizungumza.
Inakuweje wewe uwe busy kudhibiti makosa ya JK na kuharibu kila alichokifanya JK kana kwamba hukuona lolote zuri kutoka Kwa JK?
Unatufanyia maigizo juu ya maisha yetu na bado hutaki tuseme? Kwa kawaida ukifanya maigizo utaishia kuigiza na hautafanikiwa kukamilisha unachohitajika kukifanya.
JK alikuwa dhaifu lakini alikuwa kiongozi mzuri ,tulitegemea wewe hautokuwa dhaifu bali kiongozi mzuri zaidi lakini umekuwa si dhaifu ila cha kusikitisha umekuwa kiongozi mbaya kabisa.