Tafsiri ya Maneno ya Kingereza- Fund

IshaLubuva

JF-Expert Member
Dec 4, 2008
250
11
Salamu wana JF.

Naafahamu neon fund humaanisha Fedha kwa Kiswahili, lakini kuna wakati huwa linamaanisha Mfuko au Fuko (hapa nashindwa kuelewa ni lipi neno muafaka maana kwa mfano IMF huwa kuna wakati inatafsiriwa kama Fuko la Fedha la Kimataifa lakini wakati mwingine inatafsiriwa kama Shirika la Fedha la Kimataifa, kipi ni kipi? tafadhal)

Aidha, naomba mwenye kufahamu tafsiri ya maneno yafuatayo:

Reserve Fund, accumulated fund.

asanteni kwa sasa.

IshaLubuva
 
Kwa kawaida kwenye lugha maneno yana tabia ya kuselelea. Neno "fund" peke yake haliwezi kuwa na maana ila linategemea limetanguliwa au limefuatiwa na neno gani. Kwa kumaanisha fuko inamaanisha fuko la kuwekea fedha, kwa hiyo utaona kwamba neno fund kwa maana ya fuko linatokana na asili ya neno hilo kuelezea fedha.
 
Back
Top Bottom