Wakati wa kampeni Mh Pombe alipiga pushapu, wakati mwingine alicheza kiduku akiwaambia wananchi hasa wale wanyonge mimi nitafanya kazi usiku na mchana na nitatengeneza serikali rafiki kwa wanyonge akasema "HAPA KAZI TU" Wananchi wanyonge wasioijua michezo ya wanasiasa wakapiga makofi na kushangilia hadi kuombwa wanyamaze!
Nawauliza wanyonge vipi serikali hii ni rafiki kwetu?
Hebu nenda mabibo na kariakoo au nenda soko kuu Arusha au pale Kilombero kaulize bei ya kitu chochote alafu uje uniambie unaona nini mbele?
Majambazi wakivamia watu siku hizi wanakauli mbiu moja tu "HAPA KAZI TU" ndo maana nauliza kauli hii hasa ina maana gani?
Waziri mmoja akasema hata kama unavibali nyumba itabomolewa tu "Hapa kazi tu" akasema eti mimi raiya nikamshitaki yule aliyenipa vibali! Very interesting:🙁 yaani afisa wa serikali mwenye mamlaka na aliyepewa dhamana na serikali na wakampa mihuri ya serikali ili afanye maamuzi leo eti mimi raiya nimwajibishe!
Swali la mwisho kwa leo::hivi hii kauli ya "HAPA KAZI TU" inamuhusu kila anayeenda kinyume au ikifika maeneo Ofisi za CCM Lumumba, majengo ya wahindi upanga, ofisi za DART na KEBY´S HOTEL itageuka na kuwa HAPA PITA TU?