Mwigulu yupo sahihi, kipato cha mtu kinapoongezeka na matamanio yanaongezeka

KwetuKwanza

Member
Mar 13, 2023
34
82
IMG-20240301-WA0020.jpg

“GDP ya Nchi sio namba ya Watumishi wa Umma ni namba za uzalishaji wa Nchi, hivyo zinapoongezeka ni uzalishaji unaotajwa, namba inatajwa kwenye Sensa kwa uwiano wa kilichozalishwa na uwiano wa Wananchi.

“Kipato cha mtu kinapoongezeka na matamanio yanaongezeka, hicho ndicho kinachosababisha maisha yawe magumu.

“Ugumu wa maisha ni kuanzia pale unapozaliwa ndio maana wanasema maisha ya mwanadamu siku zake ni chache tena zilizojaa tabu.”

Hiyo ni kauli ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba aliyoitoa Februari 29, 2024, ambapo kiuhalisia alikuwa sahihi, ndio maana hata binadamu awe tajiri mkubwa bado hawezi kuacha kutamani mambo makubwa zaidi ya aliyonayo.

Alichokisema Mwigulu bila shaka nimemaanisha uhalisia wa maisha yetu binadamu lakini inawezekana kwa imani za kisiasa au vyama sio wote wanaoweza kumuelewa au hata kama wamemuelewa hawawezi kukubali na kuweka wazi hadharani.

Unadhani katika ulimwengu huu wa digitali utaficha kitu gani na watu wasikijue? Watu wamekomaa kwa dhihaka na utani kuhusu mifano aliyoitoa Mwigulu kuwa kuna magari mengi mapya yaliyosajiliwa tofauti na ilivyokuwa miaka kadhaa nyuma, foleni za benki na hata michango ya harusi, hiyo yote ni mifano halisi na rahisi kuielewa.

Mifano hiyo inawezekana ikaonekana ni ya kuchekesha lakini huo ndio uhalisia, kuna mabadiliko mengi ya kimaendeleo kwa ngazi za watu au mtu mmojammoja lakini wapo ambao hawataki kukubali kwa sababu wanazozijua wao.

Kupitia hotuba yake ya Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023/2, Mwigulu alisema sekta ya benki nchini imeendelea kubaki imara, himilivu na yenye kutengeneza faida na kuwa Mikopo kwa sekta binafsi imeongezeka kufikia Sh Bilioni 28,702.95 kwa Mwaka ulioishia Aprili 2023 kutoka Sh Bilioni 23,422.5 hadi Aprili 2022 sawa na ongezeko la 22.5%

Mfano huo ni wazi kuna mamilioni ya watu wamenufaika na mikopo kwa kuwa mtu mmoja anapokopa kuna cheni kubwa nyuma yake ama inayomtegemea au inayoenda kunufaika na mikopo hiyo, wanaobea hilo hawalioni.

Mwigulu alieleza watoa huduma ndogo za fedha Daraja la Pili walikopeshwa mikopo yenye thamani ya Sh Bilioni 870 kwa wajasiriamali wadogo na wa kati nchini, hayo yote hawayaoni.

Mwigulu amesisitiza uwekezaji mkubwa unaoelekezwa kwenye shughuli za uzalishaji ndio unaoenda kupunguza pengo la walionacho na wasionacho, pia utatoa jawabu la kudumu kwenye maisha ya Watanzania.
 
Kwahiyo kipato cha mtanzania kimeongezeka. Hivi mnajua hiyo Harusi inakaa ni mchango wa miezi mi ngapi yaani hiyo 100000 anaivunjavunja miezi mingapi
 
Watanzania wanyonge wanaendelea kuumizwa na mikopo umiza mitaani huku kuna waziri anaagiza basi kumi kwa wakati mmoja
 
Kuna wajinga wanabisha 😁😁
 
Kwahiyo kipato cha mtanzania kimeongezeka. Hivi mnajua hiyo Harusi inakaa ni mchango wa miezi mi ngapi yaani hiyo 100000 anaivunjavunja miezi mingapi
Kwani Bar Huwa mnakusanya michango ya miezi mingapi?

Pili kwani kipato hakijaongezeka?
 
Kimeongezeka kwa akina nani na kwa kiasi gani. Huko nje Kuna zaidi ya 50% ya watu milioni 60 hawana kazi mzee. Kama utachujua kipato cha MO ukakigawa kwa watu wote hapo sawa kila mmoja atakuwa ameongeza kipato
 
Mil.60 ni raia wote wa Tzn Hadi Watoto Kwa hiyo hawana kazi? Acha kuropoka hovyo
 
“GDP ya Nchi sio namba ya Watumishi wa Umma ni namba za uzalishaji wa Nchi, hivyo zinapoongezeka ni uzalishaji unaotajwa, namba inatajwa kwenye Sensa kwa uwiano wa kilichozalishwa na uwiano wa Wananchi.

“Kipato cha mtu kinapoongezeka na matamanio yanaongezeka, hicho ndicho kinachosababisha maisha yawe magumu.

“Ugumu wa maisha ni kuanzia pale unapozaliwa ndio maana wanasema maisha ya mwanadamu siku zake ni chache tena zilizojaa tabu.”

Hiyo ni kauli ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba aliyoitoa Februari 29, 2024, ambapo kiuhalisia alikuwa sahihi, ndio maana hata binadamu awe tajiri mkubwa bado hawezi kuacha kutamani mambo makubwa zaidi ya aliyonayo.

Alichokisema Mwigulu bila shaka nimemaanisha uhalisia wa maisha yetu binadamu lakini inawezekana kwa imani za kisiasa au vyama sio wote wanaoweza kumuelewa au hata kama wamemuelewa hawawezi kukubali na kuweka wazi hadharani.

Unadhani katika ulimwengu huu wa digitali utaficha kitu gani na watu wasikijue? Watu wamekomaa kwa dhihaka na utani kuhusu mifano aliyoitoa Mwigulu kuwa kuna magari mengi mapya yaliyosajiliwa tofauti na ilivyokuwa miaka kadhaa nyuma, foleni za benki na hata michango ya harusi, hiyo yote ni mifano halisi na rahisi kuielewa.

Mifano hiyo inawezekana ikaonekana ni ya kuchekesha lakini huo ndio uhalisia, kuna mabadiliko mengi ya kimaendeleo kwa ngazi za watu au mtu mmojammoja lakini wapo ambao hawataki kukubali kwa sababu wanazozijua wao.

Kupitia hotuba yake ya Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023/2, Mwigulu alisema sekta ya benki nchini imeendelea kubaki imara, himilivu na yenye kutengeneza faida na kuwa Mikopo kwa sekta binafsi imeongezeka kufikia Sh Bilioni 28,702.95 kwa Mwaka ulioishia Aprili 2023 kutoka Sh Bilioni 23,422.5 hadi Aprili 2022 sawa na ongezeko la 22.5%

Mfano huo ni wazi kuna mamilioni ya watu wamenufaika na mikopo kwa kuwa mtu mmoja anapokopa kuna cheni kubwa nyuma yake ama inayomtegemea au inayoenda kunufaika na mikopo hiyo, wanaobea hilo hawalioni.

Mwigulu alieleza watoa huduma ndogo za fedha Daraja la Pili walikopeshwa mikopo yenye thamani ya Sh Bilioni 870 kwa wajasiriamali wadogo na wa kati nchini, hayo yote hawayaoni.

Mwigulu amesisitiza uwekezaji mkubwa unaoelekezwa kwenye shughuli za uzalishaji ndio unaoenda kupunguza pengo la walionacho na wasionacho, pia utatoa jawabu la kudumu kwenye maisha ya Watanzania.
Haya Njoo tuzungumzie GDP per capita na Purchasing power huku tukizungumzia pia Inflation..
Karibu
 
Back
Top Bottom