Hahhahaha....hiyo ntasoma bwana ila hii inaonyesha sio hata imepikwa bali imechemshwa!!
Haya ngoja nikumegee kidogo, ila ile 10% ni yangu mwenyewe.
Jumla ya wanawake 10,139 na wanaume 2,527 men wenye umri kati ya miaka 15 na 49 walihojiwa.
Wanawake 6 kati ya 10 wameolewa and wanaume 5 kati ya 10 wameoa.
Asilima 5 ya wanawake na 4 ya wanaume wanaishi pamoja lakini hawajaoana rasmi.
Asilimia 25 ya wanawake ana 41 ya wanaume hawajaolewa/kuoa.
Asilimia 12 ya wanawake na 7 ya wanaume wametengana, wameachana au wamefiwa na waume/wake zao.
Wanaume walioa wana umri mkubwa kuliko wanawake waliolewa.
Asilimia 29 ya wanawake na 27 ya wanaume wanaishi mijini
Asilimia 97 ya waliohojiwa wanatoka Tanzania Bara.
Asilimia 9 ya wanawake na 8 ya wanaume wanaishi Dar Es Salaam.
Asilimia 8 ya wanawake na 11 ya wanaume wanaishi Mwanza.
Asilimia 8 ya wanawake na 7 ya wanaume wanaishi Shinyanga.
Nusu ya waliohojiwa wamemaliza elimu ya msingi.
Asilimia 15 ya wanawake na 23 ya wanaume wamemaliza elimu ya sekondari
Umegundua kitu hapo?