Sifa za mume bora

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,910
6,704
Mwanaume ambaye anastahili kuwa mumeo. Nafanya hivi ikiwa ni msaada kwa wale ambao wamefikia hatua ya kuingia kwenye ndoa lakini bado wanashindwa kutambua yupi ni sahihi na yupi si sahihi kuitwa mume. Tufahamu kwamba si kila mwanaume unayekutana naye na ukampenda anafaa kuwa mumeo. Wengine wana mapungufu makubwa ambayo bila kuyabaini na ukaingia kichwakichwa, utakutana na matatizo makubwa. Kwa maana hiyo basi, sifa hizi sita ambazo nitazizungumzia leo endapo utaziona kwa huyo ambaye macho yako yameganda kwake, fanya maamuzi sahihi ya kumkubalia.

Anakupenda kwa maana ya kukupenda

Unapoingia kwenye maisha ya ndoa, unatarajia kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwenza wako. Wapo wanaume ambao wanaonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na demu flani bomba au kuonja tu penzi kisha kuanza visa ili muachane.Kwa nini ni vizuri kumpata mwanaume mwenye mapenzi ya dhati? Hii inatokana na ukweli kwamba kinyume na hivyo, maisha yatakuwa ya migogoro kila siku. Atakufanyia mambo ya kukuumiza kwa kukusaliti bila kujali maumivu utakayopata. Hii yote ni kwa sababu hana mapenzi ya kweli na wewe. Ndiyo maana unashauriwa kwamba, kabla hata ya kumuonjesha penzi kisha kufanya maamuzi ya kumruhusu aende kwa wazazi wako ili mfunge pingu za maisha, ni vyema ukawa na uthibitisho kwamba anakupenda kwa moyo mmoja.

Awe anaota mafanikio

Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanawake. Wengi hawapendi kabisa kuolewa na mwanaume ambaye hana kazi. Mwanaume anatakiwa kuwa dereva katika safari ya kusaka mafanikio, sasa kama atakuwa ni mtu wa kukaa kijiweni, kupiga mizinga, mvivu asiyependa kujishughulisha kwa namna yoyote, huyu hafai kupewa nafasi ya kuitwa mume.

lle dhana ya kukubali kuolewa na mwanaume yoyote ili mradi upate heshima ya kwamba umeolewa, imepitwa na wakati. Mwanaune sahihi ni yule mwenye malengo maishani, anayefikiria nini cha kufanya kwa ajili ya maendeleo yake, mkewe na watoto wao. Wa shida na raha Wapo wanaume ambao siyo wavumilivu kabisa katika maisha.

Tunajua maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha. Kwa mfano, unaweza kuingia kwenye maisha ya ndoa lakini kwa bahati mbaya ukawa huna kizazi, mwanaume mwenye mapenzi ya kweli na wewe anatakiwa kukuvumilia na kuwa upande wako.

Yule ambaye atakuwa anaungana na dada zake kukushambulia kwa kutozaa, hafai kuvwa na wewe kwani yapo mengi yanayoweza kutokea yanayohitaji kuvumiliana. Kimsingi uvumilivu kwa mwanaume utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali.

Wa shida na raha

Wapo wanaume ambao siyo wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha. Kwa mfano, unaweza kuingia kwenye maisha ya ndoa lakini kwa bahati mbaya ukawa huna kizazi, mwanaume mwenye mapenzi ya kweli na wewe anatakiwa kukuvumilia na kuwa upande wako.

Yule ambaye atakuwa anaungana na dada zake kukushambulia kwa kutozaa, hafai kuwa na wewe kwani yapo mengi yanayoweza kutokea yanayohitaji kuvumiliana. Kimsingi uvumilivu kwa mwanaume utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanaume mwenye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.

Anayejua thamani ya mke

Wapo wanaume ambao hawajui thamani ya mke na ukiwachunguza utabaini hawafai kuwa waume za watu. Mume sahihi ni yule anayejua kwamba mke ni kitu cha faraja kwenye maisha yake. Yule anayeamini kwamba, bila mke maisha yake hayawezi kuwa yamekamilika. Wapo ambao wanaamini hata bila wanawake wanaweza kuwa na maisha mazuri. Mwanaume mwenye dhana hii, ukimpa nafasi kwenye moyo wako na ukaingia naye kwenye maisha ya ndoa, lazima atakuwa mguu ndani, mguu nje. Hataona hatari kukupa talaka hata kwa jambo dogo tu ambalo mnaweza kuongea na mkalimaliza.

Ndiyo maana nikasema, mwanaume sahihi wa kumpa nafasi ya kuwa mumeo ni yule anayejua thamani ya mke, anayeweza kuvumilia yote akijua mke ndiye anayekamilisha maisha yake.
85.jpg
 
Hahaha wanaume wa ku google hao ongeza bandle utawapata ktk youtube pia Kwenye tamthilia za kifilipino
 
Mwanaume ambaye anastahili kuwa mumeo. Nafanya hivi ikiwa ni msaada kwa wale ambao wamefikia hatua ya kuingia kwenye ndoa lakini bado wanashindwa kutambua yupi ni sahihi na yupi si sahihi kuitwa mume. Tufahamu kwamba si kila mwanaume unayekutana naye na ukampenda anafaa
Nakupenda sana Mume wangu. Nakupenda, Nakupenda na Ninakupenda Tena. Sio kwa sababu wewe ni Malaika, Hapana. Nimegundua kuwa nipo na Mwanamume Bora na Sahihi😅

Nitaendelea Kukuheshimu Mume Wangu. Popote ulipo😘🥰😍💋😋
 
Mnapenda kuthaminiwa wakati thamani zenyewe mnazivunja hata kabla ya kuingia ndoani #mimi ni muumini wa jokajeusi
 
IMG_20211129_095118.jpg

Kwa fasta fasta hapa yupi anaweza akawa mume bora. 1. Mayweather 2.Just Sul
 
Back
Top Bottom