Tafiti: Wanawake wanaamini ruksa mume kumpiga mkewe

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,303
Utafiti uliofanyika mwaka jana unaonyesha kuwa asilimia 54 ya wanawake wa Tanzania wanaamini kuwa mume anayo haki ya kumpiga mkewe. Asilimia 38 tuu ya wanaume wanaamini hivyo. Uhalali wa mume kumpiga mke unaaminiwa na wanawake na wanaume wa Kitanzania kama ifuatavyo kwa asilimia (%):

1. Kama mke akiunguza chakula - wanawake -17.7%, wanaume - 5.4%
2. Kama mke akigombana na mume wake - wanawake - 38.5%, wanaume -22.5%
3. Kama mke akitoka bila kumjulisha mumewe - wanawake - 40.3%, wanaume -24.6%
4. Kama mke akitelekeza watoto - wanawake - 40.3%, wanaume - 24.6%
5. Kama mke akikataa kufanya tendo la ndoa - wanawake - 31.1%, wanaume - 13.8%
6. Wale wote wanaoamini yote hapo juu - wanawake - 54.1%, wanaume -34.4%

Findings nyingine zinatisha hasa zile zinazolenga kwenye physical and sexual violence.
Source: The Demographic and Health Survey for Tanzania 2010: http://www.measuredhs.com/pubs/pdf/FR243/FR243.pdf
 
Hayo maswala ya kumpiga mke yamepitwa na wakati...kama vipi nyumba igeuzwe ulingo wapigane kabisa badala ya mmoja kumpiga mwenzake!!!
 
duhhhhhhhhhh


nilikuwa sijui wanaume tuna haki nyingi hiviii

wakati wa kuanza kuzitumia sasa lol
 
Utafiti wa kubuni, kila kona upo bwana. Hao waliofanya utafiti wametia chumvi au pengine wanapenda kupiga wake zao na wanajitetea kwa kusingizia sisi wenyewe wanawake wanalikubali sawa la kupigwa na mume kwa kosa kiduchu. Au walifanya utafiti kwenye makabila yanayopenda kupigwa.

Kama mke anaunguza mtoto moto au anasaliti ndoa yake kiudharau na kinyama, hapo naweza kukubali mke apigwe kuinyosha akili ya yake iliopinda. sio kaunguza ugali, kofi, katia chumvi nyingi ktk ubwabwa, gumi, duh. Sizani kama kuna mwanamke atakae weza kuishi maisha hayo
 
Hao wanawake wengi ni wa umri gani haswa?!Asili?!Elimu?!Historia za kifamilia??!
Ni kuanzia miaka 18 hadi 35, ni kaskazini mwa Tanzania jirani na Kenya pale ziwa Victoria, darasa la saba tu kwani kuna tatizo gani?, ni jamii ya wafugaji na wavuvi wenye maisha ya kawaida teh teh teeeh!
 
Ni kuanzia miaka 18 hadi 35, ni kaskazini mwa Tanzania jirani na Kenya pale ziwa Victoria, darasa la saba tu kwani kuna tatizo gani?, ni jamii ya wafugaji na wavuvi wenye maisha ya kawaida teh teh teeeh!
Kaskazini mashariki au magharibi?!Naomba unichoree na ramani kabisa maana tangu nifanye mtihani wa maarifa ya jamii darasa la saba sikuwahi kurudia kuangalia ramani ya nchi hii!!

Darasa la saba nalo la shule za kata au zile akademi za wazungu weusi!!?
 
Lizzy vp mbona unaniangusha! ni jirani na Kenya, pale ziwa victoria ebo!
 
Hahhahaha....hiyo ntasoma bwana ila hii inaonyesha sio hata imepikwa bali imechemshwa!!

Haya ngoja nikumegee kidogo, ila ile 10% ni yangu mwenyewe.

Jumla ya wanawake 10,139 na wanaume 2,527 men wenye umri kati ya miaka 15 na 49 walihojiwa.
Wanawake 6 kati ya 10 wameolewa and wanaume 5 kati ya 10 wameoa.
Asilima 5 ya wanawake na 4 ya wanaume wanaishi pamoja lakini hawajaoana rasmi.
Asilimia 25 ya wanawake ana 41 ya wanaume hawajaolewa/kuoa.
Asilimia 12 ya wanawake na 7 ya wanaume wametengana, wameachana au wamefiwa na waume/wake zao.
Wanaume walioa wana umri mkubwa kuliko wanawake waliolewa.
Asilimia 29 ya wanawake na 27 ya wanaume wanaishi mijini
Asilimia 97 ya waliohojiwa wanatoka Tanzania Bara.
Asilimia 9 ya wanawake na 8 ya wanaume wanaishi Dar Es Salaam.
Asilimia 8 ya wanawake na 11 ya wanaume wanaishi Mwanza.
Asilimia 8 ya wanawake na 7 ya wanaume wanaishi Shinyanga.
Nusu ya waliohojiwa wamemaliza elimu ya msingi.
Asilimia 15 ya wanawake na 23 ya wanaume wamemaliza elimu ya sekondari

Umegundua kitu hapo?
 
Anipige aone!!! Nitamvizia akirudi kwenye mapombe yake, nitamshughulikia na hatanisahau!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom