Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Moja ya vitu vigumu sana ambavyo napambana navyo na pengine labda sio mimi peke yangu na watu wengine ni subira.
Wote tuna matarajio na matamanio ambayo tungependa tuyakamilishe. Matarajio haya na matamanio haya sio ya karibu; ni vitu vilivyo mbali.
Tunahitaji kufanya kazi kuyafikia. Na wakati mwingine kunakuwepo na vikwazo kuyafikia hayo matarajio yetu na matamanio yetu. Na wakati mwingine tunapungukiwa imani ya kwamba huenda yale ambayo yako kwenye akili zetu hayatokuja kutokea dhahiri machoni kwetu. Imani yetu inapungua mara kwa mara. Lakini kila wakati tuna tumaini na tumaini letu ndio imekuwa mwongozo wetu.
KWAKUWA bila matumaini binadamu hawezi kuishi. Kila wakati tuna tumaini kesho itakuwa bora kuliko jana na tunafanya kazi kufikia malengo yetu. Kwasababu sisi kama binadamu tunawajibika kuacha dunia bora kuliko ambayo tumeipokea kwa watu waliotutangulia.
Sisi binadaamu ni kama wafanya kazi wa kukodi tunafanya kazi kwa bidii na kuacha kila kitu tulichokipata kwa kufanya kazi kwetu kwa watu wengine, baada ya kufa.
Kuna watu wanaacha vikubwa na wengine wanaacha vidogo kulingana na juhudi zao. Lakini wote wanakufa , waliofanya kazi sana na wale waliofanya kazi kidogo.
Tunakufa tunaacha watoto wetu kama tumebahatika kupata , nao wanahangaika vile vile , kama sisi na kuondoka duniani.
Duniani tunapita na juhudi zetu zote ni kama wafanyakazi wa kukodi. Tunajenga nyumba hatuishi milele. Tunajenga miji hatuji kuikalia sisi badala yake wanakuja wengine. Kwakujua hili lazima tutambue kitu kimoja kuna nguvu iliyopo juu ya yote haya.
Huwezi kujua kama mtoto wako atakuwa na tabia sawa na wewe, na ataziangalia mali zako kwa umakini. Utajiri wote uliojikusanyia kwa maisha yako yote anaweza kuutapanya na kuuharibu. Anaweza asiwe na nidhamu na busara kama zako.
Tunaweza kujenga miji ikawa mizuri sana kwa busara kubwa na umakini. Watu wa miji hiyo wakaishi kwa amani na upendo. Wakawa wenye juhudi na maarifa. Lakini kizazi kimoja sio sawa na kizazi kingine. Tabia za binadamu hubadilika. Kile kilichojengwa kwa busara na maarifa huenda kikaharibika na kupotea kabisa. Hakuna kinachodumu.
Tunahitaji roho ya subira kujua na kufahamu mambo.
Ukitaka kujua baadae ya taifa lolote lile lazima ujue tabia za watu wa mataifa hayo kwa kipindi hiko. Tabia za watu zinaeleza kila kitu. Tabia haifichi kitu. Maendeleo yetu yanategemea tabia zetu.
Tunapotoka nje na kuangalia dunia tunaona nini? Miti, ndege, majani, ardhi kubwa. Na angani nyota, mwezi na jua. Binadamu ni sehemu ndogo ya kitu kikubwa kinachoitwa dunia. Maisha yake yote yanategemea ardhi. Tunatembea kwenye ardhi hii. Tunachunga mifugo kwenye ardhi hii. Tunalima kwenye ardhi hii kwaajili ya maisha yetu ya kila siku. Na tunapozaa watoto wetu wanaishi kwenye ardhi hii. Tunachangia ardhi hii na wanyama na hata wadudu. Kuna mambo tunapaswa kutambua na kufikiri. Na kitu kimojawapo ni uwepo wa Mungu. Asili ya dunia yetu tuliyopo na uumbaji.
Ni bora kwetu kufikiri mwisho wetu utakuwaje. Kwasababu maisha yetu ya duniani ni mafupi. Juhudi zetu zote za kupata vitu vile ambavyo tunahitaji katika maisha yetu zina faida tutakapojitambua. Juhudi za mikono yetu zitakuwa na faida pale tutakapojitambua. Na mali tutakazopata kwa juhudu zetu zitatufariji pale tu tutakapojitambua. Tutakapojijua sisi ni kina nani na nafasi yetu ni ipi. Tutakapotumia utajiri wetu vyema na kuupata katika njia zinazostahili.
Na subira ni kila kitu. Tunaweza kutumaini kile kitu tunachotumaini kisije kwa haraka. Tukakata tamaa, tukaacha kufuatlia ndoto zetu. Lakini kama tukitia juhudi na tusipokata tamaa yale yote tunayotumaini yatakuja kukamilika. Dunia tunayoiona haikuumbwa kwa vitu ambavyo ni dhahiri. Tusitafute njia za mkato ambazo zitakazotupelekea kujeruhi binadamu wengine.