GE2025 Ole Sabaya: Kanisa la kweli halibishani na Serikali

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,713
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya amesema kuwa Kanisa la kweli la Bwana halibishani na Serikali kwakuwa Mamlaka ya Serikali yanatoka kwa Mungu hivyo amewaomba Viongozi na Waumin wa Makanisa mbalimbali kudumisha amani.

Upuuzi,wanufaika wa mfumo kandamizi lqzima wautetee ugali wao.
 
Dini inabeba waumini ambao ndio waamini wa vyama tofauti tofauti hivyo sioni dhambi siasa kusemwa kanisani
 
Bila shaka aliyetoa kauli hiyo atakuwa ni mwendawazimu anayemtumikia shetani.
 
Kanisa la kweli litakemea utekaji, mauaji na watu kupotezwa.
 
Serikali ni watu
na kanisa ni watu sio jengo
kwanza huyu alipaswa kuwa jela mpaka sasa
sijui alitokaje?!
 
..kwa hiyo serikali ya makaburu wa Afrika Kusini haikupaswa kupingwa na Makanisa?

..Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipata kuwaambia watawa wa Kikatoliki wa Mary Knoll kwamba Kanisa likinyamazia uovu linakuwa ni kama limeshiriki au kubariki uovu huo.
 
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, amewataka viongozi wa makanisa na waumini kutoingilia au kubishana na mamlaka za serikali, akisisitiza kwamba mamlaka za utawala zinatokana na Mungu, akisisitiza kuwa wanapaswa kudumisha amani na kujitokeza kupiga kura Oktoba 29, 2025.

Sabaya alitoa wito huo alipokuwa kwenye ibada ya kumsimika Mchungaji na Kiongozi wa West Meru iliyofanyika chini ya uongozi wa Askofu Mkuu wa FPCT Jimbo la Arusha. Katika hotuba yake, Sabaya alirejea mifano ya Biblia kuonesha kwamba mamlaka ya kisiasa ni sehemu ya mpangilio wa Mungu.

“Ipo saa Mungu hata kama wewe ni muovu hata kama ni mharibifu, saa yake ya kusema endelea kukaa kwenye hicho kiti mradi ipo, wewe mwache aendelee kukaa maana ni wa Bwana, hivyohivyo inatumika kwa Serikali, Kanisa la kweli la Mungu mtakatifu haijalishi sauli yupoje, haumpendi, unamuona Mama Samia anafaa hafai! Kanisa la kweli la Mungu halibishani na Serikali”, alieleza.

Alisema pia kuwa hata mtu mwenye makosa kwa mujibu wa wakati wake, Mungu ndiye mwenye mamlaka ya kumchagua ni lini ataondolewa au kubadilishwa, hivyo wachungaji na waumini wasiwe chanzo cha vurugu au kuvuruga utulivu.

Sabaya aliwataka waumini wasiwe mashirika ya siasa na badala yake waende kupiga kura, wakizingatia amani na utulivu kama wajibu wa kiraia na wa kidini.

Hao wenzetu ni waoga wa kufa hawezi kufanya lolote na hawana umoja kabisa maneno mengi sana, na wameharibu mapambano walivo ingiza udini ndani ya struggle ya dimokurasia hapo ndo basi, watulie hi miaka mitano kabisa.
 
Hahaha Sabaya? Kanisa gani analolizungumzia? Yaan mboni sijamsikia akikemea utekaji na uuaji au hio ndio mipango ya Mungu anaemzungumzia?
 
Back
Top Bottom