Tafakuri ya swallat adhuhuri: Naomba Mnisaidie kuyajua Majina ya watoto wa Adam kutoka kwenye quran

Mangi Meno

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2024
Posts
356
Reaction score
1,069

Jioni hii wakati natafakari na kuiskma quran kuna kitu kimenichanganya kidogo na kunipa ukakasi ndio maana nimekuja mbele yenu mnapenda majibu.

Vifungu vingi vinasema kuhusi uumbaji mzuri wa Allah kwa namna alivyomuumba Adam mfano:

1. (kumbuka) Mola wako alipowaambia Malaika, “Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo mkavu unaotoa sauti, wenye kutokana na matope meusi yaliyovunda.”“Basi nitakapomkamilisha na kumpulizia roho inayotokana na Mimi, basi mumuangukie kwa kumtii.” (15:28-29)

2. (Kumbuka) Mola wako alipowaambia Malaika: Hakika mimi nitaumbwa mtu kwa udongo. Na nitakapomkamilisha na kumpulizia roho inayotokana na mimi basi msujudieni (kama ishara ya kumheshimu). (38:71-72).

3. Hadhi ya Adam(a.s) na Kizazi Chake
Kabla ya Adam(a.s) kuumbwa, Allah(s.w) aliwafahamisha Malaika kuwa atamleta Khalifa (kiongozi) katika ardhi atakayesimamisha Ufalme wa Allah(s.w) (Dola ya kiislamu) kwa kufuata mwongozo wake Allah(s.w). Mazungumzo baina ya Allah(s.w) na Malaika wake juu ya ukhalifa wa Adam(a.s) na kizazi chake tunayapata katika aya zifuatazo:

4. (Wakumbushe watu khabari hii): Wakati Mola wako alipowambia Malaika: “Mimi nitaleta Khalifa katika ardhi.”
Wakasema (Malaika): “Utaweka humo watakaofanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutukuza kwa sifa zako na kukutaja kwa utakatifu wako?” Akasema (Mwenyezi Mungu): “Hakika Mimi nayajua msiyoyajua.”(2:30)

Na (Mwenyezi Mungu) akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema (kuwaambia Malaika): “Niambieni majina ya vitu hivi ikiwa mnasema kweli (kuwa nyinyi ndio wajuzi wa mambo).”(2:31)
Wakasema (Malaika): “Utakatifu ni wako! Hatuna ilimu isipokuwa ile uliyotufundisha; bila shaka wewe ndiye Mjuzi na ndiye Mwenye hikima.” (2:32).

Akasema (Mwenyezi Mungu): “Ewe Adam! Waambie majina yake.” Alipowaambia majina yake alisema (Mwenyezi Mungu) “Sikukwambieni kwamba mimi najua siri za mbinguni na za ardhi; tena najua mnayoyadhihirisha na mliyokuwa mn
“Enyi mlioamini! Je! Nikujulisheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iumizayo?(61:10)

Lakini nimekosa vifungu katika quran vinavyotaja majina ya watoto wa Adam zaidi ya hapa “Na wasomee khabari za watoto wawili wa Adam kwa kweli, walipotoa sadaka, ikakubaliwa ya mmoja wao na ya mwingine haikukubaliwa Akasema (yule asiyekubaliwa sadaka yake): “Nitakuua”. Akasema (yule aliyeahidiwa kuuawa): “Mwenyezi Mungu huwapokea wamchao tu”. “Kama utanyoosha mkono wako kwangu kuniua, mimi sitanyoosha mkono wangu kukuuwa. Hakika mimi ninamuogopa Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu .

Kwa kukosa kutaja watoto wa Adam, kumenifanya nihisi kama tumepigwa au quran imechakachuliwa. Nakuja mbele tenu wana JF, naomba kifungu kinachotaja majina ya watoto wa Adam.
1753712047279.jpg
 
Nyie jamaa huwa mnachekesha

Ukitaka challenge kaa chini kwanza usome vya kutosha ndiyo uje na hoja mezani
La sivyo ukiachana na kuonekana vituko kwa wenye elimu pia mnapotezea watu muda
 
Acha blah blah. Lete andiko we maamuma.
 
View attachment 3421786
Wahi hospital
 
halafu kumbe ibilis hakuwa ameambiwa kabla hta hii issue ya kumsujudia adam kabla ya wenzie malaika,ila alivyogoma akapewa adhabu.
 
Unaambiwa ukisoma Quraan soma na hadithi ya mtume hapo utaipata majina ya watoto wa adamu maana kuna aya zingine hazikufunguka na utaipata kwenye hadithi ya mtume
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom