Tafakuri ya kina ya No Reforms, No Election

Tafakuri ya kina ya No Reforms, No Election

its_ruzel

New Member
Joined
Sep 5, 2025
Posts
1
Reaction score
1
Habari watanzania

Bila kupoteza muda ningependa niende moja kwa moja kwenye mada ninayotaka kuongolea.

Kila mmoja nadhani atakubaliana nami kwamba swala la NO REFORMS NO ELECTION limeibua hisia tofauti akilini mwa watu,

Kiuhalisia mjadala wa NO REFORMS NO ELECTION si jambo dogo kwa kuwa ni mjadala unaogusa uhalali wa demokrasia, Mustakabali wa Taifa na maisha ya mwananchi mmoja mmoja.

Hapa nimekusanya baadhi ya maswali ya msingi ambayo kila mmoja wetu anapaswa kujiuliza na kuyatafakari kwa kina:

1. Ni nani atakaeleta hizo reforms?

... Je, mageuzi tunayoyazungumzia yatakuja kutoka kwa wananchi wenyewe, viongozi wa siasa, au shinikizo la kimataifa? Mara nyingi historia hutuambia kuwa hakuna mtu anayeleta reforms kama zawadi; bali hutokana na msukumo wa wananchi na mshikamano wa kitaifa. Lakini je, sisi kama taifa tuko tayari kulibeba jukumu hilo?

2. Je tunadhani kwamba sisi watanzania tuna huo ujasiri wa kuingia barabarani hiyo october 29??

Ujasiri wa kudai haki mara nyingi huonekana kuwa hatua kubwa za wananchi. Lakini ukweli ni kwamba utamaduni wa Tanzania huonesha kuwa tuna nidhamu ya uwoga na kutokuwa na kauli ya pamoja kama wananchi katika masuala makubwa kama hayo yagusayo hatima ya nchi yetu kwa kisingizio kwamba Tz kuna amani..!!. Swali ni je, tunayo ile nguvu ya pamoja na mshikamano wa kweli wa kuonyesha ujasiri huo bila kuogopa madhara?

3. Je ni nani atakaekuwa kiongozi wa hayo maandano au coordinator wa ku shawishi na kuunganisha watu waandamane??
...
Je tunawategemea wanaharakati waendeshao shughuli zao nje ya nchi kama kina Mange na kina Polepole wawe ma coordinator ilhali wahapo hata nchini au kina lissu waliopo kifungoni???
Harakati kubwa hazifanikiwi bila viongozi thabiti. Tanzania ina viongozi wa siasa, wanaharakati na sauti za kijamii, lakini nani atakayechukua jukumu la kuunganisha watu kwa lengo moja? Je, ni kiongozi wa chama, ni mwanaharakati, au ni kizazi cha vijana kinachoinuka?

4. Je kwa mda uliobaki huu tunadhani unatosha kwa kufanya reforms???.. Au uchaguzi upelekwe mbele ndo reforms ziweze kufanyika?

Mageuzi makubwa kisheria na kikatiba mara nyingi yanahitaji muda mrefu na majadiliano ya kina. Hivi muda uliopo kabla ya uchaguzi unatosha kweli? Ikiwa la, je, tupo tayari kuona uchaguzi ukiahirishwa kwa ajili ya reforms?

Au uchaguzi upelekwe mbele ndo reforms ziweze kufanyika?
Kama ndio, swali linakuja, je wenye mamlaka watakubali uchaguzi uharishwe kwa ajili ya hayo mabadiliko bila hofu ya kupoteza uhalali wao?

5. What if kama uchaguzi ukafanyika na serikali iliyopo ikaendelea kuwepo????.. Je hatutoitambua na kivipi!?

Hii ni changamoto kubwa. Serikali ikitangazwa kwa mujibu wa katiba, hata kama watu hawajakubaliana nayo, inapata uhalali kisheria. Swali ni, je, kama baadhi ya wananchi hawataki kuitambua, hiyo itatafsiriwa vipi kivitendo?

6. Je kama watanzania wameamua kuyasusa masanduku ya kura hyo October 29, je tunadhani ndo itaondoa uhalali wa ccm kushinda. Je tunadhani idadi ya kura ndo itakuwa ndogo sana, ikiwa watu hawatojitokeza siku ya tukio????

7. Je tunaamini kuwa baada ya CCM kupewa ridhaa kwa miaka mi5 ijayo ndo wataleta mageuzi hayo tunayoyataka hivi sasa au bora mageuzi????

Siku zote chama tawala mara nyingi hubadilika kutokana na shinikizo kubwa, si kwa hiari. Je, tunayo imani kwamba kwa kipindi kipya cha miaka mitano CCM (CCM mtandao) itaamua kubadilika kwa faida ya wananchi?

8. Je ni ipi njia sahihi tutakoweza kuitumia ili kuikomboa nchi yetu ???

Maandamano si njia pekee. Kuna njia za kielimu, kidiplomasia, shinikizo la kiraia, na mshikamano wa vyama vya siasa. Swali ni je, tunayo mikakati ya muda mfupi na muda mrefu ya kuunganisha nguvu hizi zote kwa pamoja?

9. Hivi tunadhani kama ikitokea mf: Urais wa Tz amemshinda mgombea wa chama X.

Je mwenyekiti wa tume ataweza kumtangaza kwa haki???? Au atashinikizwa ( na wasiojulikana) ili aya ditch matokeo halali?

Je, mwenyekiti ataweza kuishinda nguvu ya shinikizo ili kuilinda sauti ya wananchi???.. (refer: Previous GE in kenya)


10. Je inawezekana Tz ikarudi mikononi wa wananchi na wazalendo kwa amani kabisa bila kumwaga damu?

11. Je tunaamini kweli kuwa mabadiliko ya kweli yanaweza kufanywa na viongozi waliopo madarakani?

Na je historia inatuonesha hivyo kweli?

Kwa kawaida, walio kwenye madaraka mara nyingi hupinga mabadiliko yanayoweza kupunguza nguvu zao. Je, tunaamini kweli kuwa mabadiliko ya kweli yataanzishwa na wale walionufaika na mfumo huu?

12. Je tuna uhakika kwamba mabadiliko tunayoyataka hayatageuzwa kuwa silaha za kisiasa na kuchochea mgawanyiko zaidi badala ya mshikamano?

✍🏽Hayo ni maswali ya kutafakari ambayo yatupasa kila mmoja wetu ajiulize na atafakari kwa kina.



TUNA SAFARI NDEFU SANA LAKINI MAISHA LAZIMA YAENDELEE 🙏🙏


Ahsanteni.
 
Siku ya huo uchaguzi wengi tutabakia majumbani kwetu kwa sababu hatutapoteza muda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom