Halfcaste
JF-Expert Member
- Nov 28, 2010
- 972
- 215
Nimesikia na nimepitia maoni ya watu wengi kuhusu Mh.Rais JPM kuhusu kupunguza Wizara hadi 15. Lakini wengi wetu hatuelewi kuwa hata Wizara ukiipa jina sijui Tume au Idara au Agency bado gharama za uendeshaji ni zile zile, watumishi ni walewale na gharama za uwekezaji katika Kitengo hicho ni hizo hizo.
Mfano, Unaunganisha Wizara ya Maji, Kilimo, Mifugo na Biashara. Hapa hujapunguza Wizara umepunguza Mawaziri tu, Tena utaongeza Wakurugenzi na Makatibu Wakuu waweze kumsaidia Waziri. Gharama za uendeshaji wa kila Idara sijui Kitengo utakavoita wewe zipo palepale.
Narudia siyo rahisi kupunguza Wizara labda idadi ya Mawaziri.
Nakaribisha michango bila mahaba na mihemko ya kisiasa.