Tafakuri: Mungu, Adam, Hawa vs Shetani, Hawa, Adam

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,998
142,025
Mungu alimpa maagizo Adam kwamba matunda ya miti Yote aweza kula isipokuwa tunda la mti wa katikati na kwamba siku atakapoyala atakufa hakika

Shetani alimwambia Hawa siku mtakayokula matunda ya mti wa katikati mtafumbuliwa macho nanyi mtakuwa kama Mungu mkijua mema na mabaya

Hawa akamshawishi Adam wakala tunda na kujikuta wako uchi

Tafakari ni wapi Uzembe ulifanyika tukaanguka dhambini

Je, leo hii Nguvu ya sauti ya Hawa kwa Adam ni ile ile?

Sabato njema!
 
Kama ikiwezekana Mungu na shetani wakae pamoja wamalize tofauti zao ,Kwanza kipindi kile Mungu anakutana na shetani ,shetani akasema anazurula ,Mungu akasema unamuona mwanangu yusufu ,Mungu akasema nenda kamjaribu ,mbona hawakumalizana ,au hawajamaa Ni marafiki nin ,isijekuwa tunachezewa movie wakuu....sisi tunahangaika kwa ujinga waliofanya wengine
 
Back
Top Bottom