Ndugu zangu,
Kwa mujibu wa takwimu za Kisayansi, mwaka 1950 nchi yetu ilikuwa na idadi ya Watanzania wapatao milioni saba. Takwimu hizo zinabainisha, ifikapo mwaka 2050, nchi yetu itakuwa na Watanzania wapatao milioni mia moja. Hii leo, idadi ya Watanzania inakadiriwa kuwa milioni arobaini na nane.
Nini tafsiri yake?
Tukianza na Krismas inayokuja mbele yetu, tunaona, kuwa mwaka 1950 kulikuwa na idadi ya Watanzania milioni saba tu waliosheherekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Na hata sherehe nyingine za kidini zilisheherekewa na idadi hiyo ya Watanzania. Krismas ya mwaka huu itasherehekewa na Watanzania wapatao milioni arobaini na nane.
Maana kubwa ya taarifa hizo za kisayansi ni ukweli, kuwa, wakati huko nyuma ilisemwa, kuwa ili tuendelee tunahitaji vitu vinne; ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora, tunapaswa sasa kutafakari upya.
Kwamba tulidhani kuwa ardhi tunayo ya kutosha, hapana, huko tunakokwenda ardhi yetu itakuwa ndogo sana kwa idadi kubwa ya Watanzania watakaoongezeka. Hivyo basi, moja ya tishio la nchi yetu kuendelea ni kukua kwa kasi kwa idadi ya watu bila kuwa na uwiano wa mipango thabiti ya kuhakikisha kuna udhibiti wa rasilimali za nchi na kuwaandaa watu wanaoongezeka kwenye misingi bora ya elimu na uhakika wa huduma muhimu kama vile afya.
Kwamba kikubwa kinachohitajika kukabiliana na changamoto za kuongezeka kwa idadi ya Watanzania miaka 50 ijayo ni kuwa na siasa safi na uongozi bora. Na hakika, siasa za hovyo hovyo huzaa uongozi wa hovyo hovyo, na uongozi wa hovyo hovyo ndio utakaopelekea Watanzania milioni mia moja watakaoishi miaka 50 ijayo waione nchi yao kuwa ni mahali pagumu zaidi pa kuishi.
Inahusu kuwa na siasa safi na uongozi bora utakaokuwa na uwezo wa kufanya maamuzi magumu ya kuhakikisha rasilimali za nchi hii ikiwamo ardhi zinalindwa. Kwamba zinalindwa kwa ari ya kizalendo ili Watanzania wa kesho na kesho kutwa wapate hakika ya uhai wao na maisha yenye staha kwenye nchi waliyozaliwa. Inahusu kuwa na mipango madhubuti ya baadae. Kuingalia Tanzania kwanza na si majina ya watu, na vyama vyao vya siasa ambavyo kimsingi ni vya kupita tu.
Na ili tuelewe hatari ya huko tunakokwenda, tuna lazima, na hasa kwa viongozi wetu, kuwa na uelewa wa hali halisi ya sasa kwa maisha ya Watanzania walio wengi.
Tunakwenda Wapi?
Hili ni swali muhimu la kujiuliza kwa kila mmoja wetu.
Na hili mwanadamu ujue ulipo sasa na unakokwenda, ni vema ukajua ulikotoka.
Tuwe wakweli kwa nchi yetu. Njia ya tulikotoka na tulivyokuwa tukienenda kuutafuta mustakabali haikuwa yenyewe. Kama taifa tulikuwa tunaelekea kubaya.
Rais huyu tuliye naye sasa ameamua kufungua makabati na sio tu kutuonyesha mizoga yenye kunuka, bali, yeye mwenyewe kaingia mstari wa mbele kuitoa na kusafisha makabati, kwa mikono yake.
Uchumi ule wa nchi na anasa iliyombatana nayo kwa wachache ulikuwa ni sawa na 'Uchumi wa maputo ya mapovu'. Ni dhahiri ungefika mahali yangepasuka na kutuacha na bumbuazi kama taifa. Si ajabu yangetufika kama ya nchi ile ya Estland iliyofilisika mpaka watu walishindwa kutoa fedha zao kwenye ATM. Yangeweza kutufika kama ya Ugiriki kwa nchi kufilisika na bahati nzuri kwao waliokolewa na ' Wajomba zao'- Jumuiya ya Ulaya. Sisi kama taifa, na katika dunia tunayoishi sasa hatuna ' Wajomba'.
Hatupaswi tena kuruhusu hali ya kuogelea kwenye ' Uchumi wa Mapovu'. Mwisho wa siku mapovu hukatika tu. Tutalazimika kuyaogelea maji halisi ya kiuchumi yenye kina kirefu na cha hatari.
Huyu Rais tuliye naye sasa ametambua ukweli, kuwa katika haya ayafanyayo kwa taifa, kuna watakaompenda na kumchukia. Kilicho cha dhahiri ni kuwa, kwa vile rushwa na ufisadi ilikuwa kero namba moja kwa Watanzania, na kwa kuwa Rais ameamua kupambana na rushwa na ufisadi kwa nguvu zote. Na kwa kuwa ameonyesha kwa vitendo kuwa kwenye Tanzania ya sasa hakuna anayeogopewa kwa jina na cheo chake, au kwa chama chake, hata kama ni anachotoka Rais mwenyewe. Basi, kwa hayo machache kati ya mengine mengi aliyoyafanya ndani ya mwaka mmoja tu, Watanzania walio wengi wanamwona Rais aliyemama upande wao.
Maana, Wananchi wanakerwa na viongozi wanaojiona "Mabwana Wakubwa". Kwa Rais, sio tu anapaswa kujipembua kutoka kundi la viongozi wa staili hiyo, bali, Rais ana wajibu wa kuondokana na viongozi wa aina hiyo. Watanzania wanaona akifanya hilo la mwisho. Maana, ni yeye waliyemchafgua na kumpa dhamana ya mwisho ya kuteua na kuwatengua madarakani viongozi kama hao.
Kikubwa kilichokosekana na kinachorudi sasa ni nidhamu, hivyo, kuzingatia maadili, kwa viongozi na raia.
Nani anamwelewa Magufuli?
Jibu, wenye kumwelewa wanaongezeka kwa idadi, lakini, ukweli unabaki, kama Krismas ya mwaka 1950 ilisheherekewa na Watanzania milioni saba, na ya mwaka huu itasheherekewa na Watanzania milioni 48, basi, Krismasi ya mwaka 2050 itasheherekewa na Watanzania milioni mia moja.
Na kwa haya anayoyafanya Magufuli wa leo, hatujui wa kesho atakuwaje, kama ataendelea hivi hivi, yumkini Watanzania wa mwaka 2050, ambao ni watoto na wajukuu zetu, wataelewa zaidi alichofanya Magufuli kwa taifa na watakuwa na kikubwa cha kusheherekea
Naam, kila kizazi na jukumu lake; hii ni tafakuri jadidi. Nakaribisha mjadala..
Maggid Mjengwa,
0754 678 252/ 0688 37 36 52