Tafakuri: Haya Majiko ya Gesi wanayogawa Wabunge kila kona yanatoka wapi?

Master Legendary

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
550
786
Wanajamvi sijui kama na nyie mnaona au ni mimi tu,nimekuwa nikifuatilia kwa muda sasa naona Wabunge wanagawa sana Majiko ya Gesi majimboni mwao.

Ninachojiuliza ni kwamba wanaigana au wanakubaliana kuwa ndiyo zawadi nzuri au kuna maelekezo au kuna sehemu wamepata majiko hayo kwa fadhila au ni nini kinaendelea.

Kuna mmoja nimesikia amegawa majiko hayo na vitu vingine vyenye thamani ya Milioni 230, najiuliza Wabunge wanalalamika mishahara na posho ndogo haya mapato yanatoka wapi?

Tujenge utamaduni wa kujiulizauliza jamani siyo vibaya tunaweza kuona kitu,tahadhari na uoga ni vitu viwili tofauti kwenye kichaka chenye nyoka.
 
Tanzania ndio nchi pekee pesa za kampeni na uchaguzi zinatolewa mapema ,tena bila ya ukakasi ila mtumishi anadai stahiki zake anapigwa kalenda .
 
Wanajamvi sijui kama na nyie mnaona au ni mimi tu,nimekuwa nikifuatilia kwa muda sasa naona Wabunge wanagawa sana Majiko ya Gesi majimboni mwao...
Mambo madogo mkuu, kuna watu wameiba mabilion wanatafuta pa kuziweka na sisi wa tz tulivyo wajinga tunashangilia pewa majiko , we are stupid as Tanzanian, remember 24
 
Back
Top Bottom