Tafakari yangu juu ya kauli za Freeman Mbowe.

Tafakari yangu juu ya kauli za Freeman Mbowe.

Huoni kuwa kuahidi kuachana na siasa ni kutoa nafasi kwa wengine kuendeleza pale alipoishia? Yeye kujitangazia uenyekiti kabla ya uchaguzi huoni kama ni kauli inayoonyesha kuwa amekikubali kuwa bado ana uwezo na imani ya kuendelea kuaminiwa na wanachadema kutokana na kazi aloifanya ndani ya chadema?

Tunataka uchaguzi wa kidemokrasia ndugu Ngowi, hatutaki kuingia kwenye uchaguzi huku mshindi akiwa tayari anjulikana.
Tusitake kuwa kama CCM ambao mshindi huwa anajulikana kabla ya kura.
 
Tunataka uchaguzi wa kidemokrasia ndugu Ngowi, hatutaki kuingia kwenye uchaguzi huku mshindi akiwa tayari anjulikana.
Tusitake kuwa kama CCM ambao mshindi huwa anajulikana kabla ya kura.

soma aya ya mwisho ya tafakari yangu
 
kwakuwa elimu yake ni ndogo.kwakuwa amekuwa m/kiti kwa muda mrefu.kwa kuwa anajua wanachama wanataka mabadiliko na kwa kuwa mabadiliko ndani ya vyama yanahitaji vijana zaidi na kwakuwa kauli zake zinaonesha kuwa anajua nini kinatakiwa ajiuzuru
 
We ulimaliza lini elimu yako kwenye kile chuo cha kata?

kwakuwa elimu yake ni ndogo.kwakuwa amekuwa m/kiti kwa muda mrefu.kwa kuwa anajua wanachama wanataka mabadiliko na kwa kuwa mabadiliko ndani ya vyama yanahitaji vijana zaidi na kwakuwa kauli zake zinaonesha kuwa anajua nini kinatakiwa ajiuzuru
 
Mbowe ni mtu hatari sana. Wala hamaanishi anachokisema. Mtakuja niamini muda ukifika. Time will tell.

Wewe utakuwa Juliana, manake unavyomsakama Mbowe utafikiri ulitaka akunanii akakataa
 
Mwenyekiti wa chadema huteuliwa na Mtei. Uchaguzi huwa ni magumashi tu ku rubber stamp maamuzi ya Mtei...
 
Mbowe ni mtu hatari sana. Wala hamaanishi anachokisema. Mtakuja niamini muda ukifika. Time will tell.

una macho ya ajabu! hiyo hatari unaiona peke yako si uwashirikishe polisi, au ndio mambo ya cd ya mipango ya mauaji (by Mwigulu Nchemba)
 
Last edited by a moderator:
Ngowile, nadhani tafakari yako ni makini hata mimi namfananisha mwenyekiti na mtu aliyeamua kujiachia toka ghorofani kuwahi burungutu la fedha lilopo ardhini, kwamba akipona ameshatajirika akifa haina shida kuliko kuishi maskini
 
Mwenyekiti wa chadema huteuliwa na Mtei. Uchaguzi huwa ni magumashi tu ku rubber stamp maamuzi ya Mtei...

CHADEMA ni zaidi ya mzee mtei na mbowe.Kama wewe sio mropokaji unaweza kuthibitisha kauli yako?
 
CHADEMA ni zaidi ya mzee mtei na mbowe.Kama wewe sio mropokaji unaweza kuthibitisha kauli yako?

Hiyo ni nadharia. Unajua kauli ya Mtei kuwa hawezi kumruhusu a man from nowhere awe mwenyekiti aliambiwa nani?
 
kwakuwa elimu yake ni ndogo.kwakuwa amekuwa m/kiti kwa muda mrefu.kwa kuwa anajua wanachama wanataka mabadiliko na kwa kuwa mabadiliko ndani ya vyama yanahitaji vijana zaidi na kwakuwa kauli zake zinaonesha kuwa anajua nini kinatakiwa ajiuzuru

Ajiuzuku kwa lipi my web??
 
Last edited by a moderator:
kwakuwa elimu yake ni ndogo.kwakuwa amekuwa m/kiti kwa muda mrefu.kwa kuwa anajua wanachama wanataka mabadiliko na kwa kuwa mabadiliko ndani ya vyama yanahitaji vijana zaidi na kwakuwa kauli zake zinaonesha kuwa anajua nini kinatakiwa ajiuzuru
(1)Wenye elimu C ndo hawa wanaozamisha TAIFA???(2)Amekaa ndio nini?Sema ametumikia na sio CHAMA bali ni TAIFA na watanzania kwa ujumla,ni katika wachache waliojitolea kuzuia jahazi letu lisizame kwa takriban miaka ishirini sasa ilhal waliosoma ndio wanakazana kuvuta TANZANIA yetu na kuizamisha jehanam utadhani wao wako nje.(3)Watu wanahitaji mabadiliko ya kweli sio maskhara kama mistari yako na mabadiliko hayachagui kijana au mzee,mtu aweza kuwa kijana lakini akawa amezeeka kiakili.(AKILI IMECHAKAA)Hivyo hoja sio kijana au mzee hoja ni MTU SAHIHI MWENYE FIKRA SAHIHI NA DHAMIRA YA DHATI YA MABADILIKO YA KWELI.Vijana wangapi wanapata nafasi MUHIMU(nyeti) kuweza kusaidia mabadiliko lakini wanafanya usanii na maisha yetu ex.Nape.(4)Kauli ya KAMANDA inaonyesha anajua amefanya nini,anafanya nini na anakusudia kufanya nini kwa CHAMA na TAIFA KWA UJUMLA BILA KUSAHAU ANAJUA UMMA UNAMJUA NA UNAMHITAJI KULIKO WAKATI WOWOTE KATIKA HARAKATI ZA KUMKOMBOA MTU MWEUSI KIFKRA,KIELIMU NA KIUCHUMI.
 
Mi naunga mkono hizi kauli za Mbowe! Nadhani ni njia ya uhamasishaji anayoitumiwa, na sidhani kama anabaka demokrasia yoyote. Unahitaji kuwapa wafuasi wako matumaini kwa kuwa mtu wa matumaini, hata kama kuwa optimistic.

Nadhani Mbowe anatumia psychological offensive techniques zaidi, kuwa frustrate ccm na serikali yake, lakini pia kuwa empower wale wenye mioyo mepesi kama wewe. Mwaume na hasa hasa kamanda kama Mbowe ni lazima awe na moyo mgumu au roho ngumu kabisa ikiwezekana. Kupambana na ccm siyo kazi rahisi, hasa ukiwa upinzani. Hala hakuna watu wagumu na rahisi duniani kuwashwishi kama watz. Yaani inabidi uwagonge vichwa vyao kilasiku mpaka kiwaingie akilini, waamke.

Mi nadhani for the time being, ni strategy nzuri, ila nashauri iwe inabadilika time after time. Na usiwe na wasiwasi kuhusu what will happen in the future, mbona ni kazi rahisi tu, watu au wanachama wanaweza kumwomba aendelee kuwa kiongozi katika nyanja zozote zile na nina uhakika Mbowe hawezi kukataa. Hii itakuwa inatosha kufutia mbali viapo vyote.

Kwa hiyo hakuna kinacho haribika hapa.
 
Habari wana JF

Ni wasaa mwingine tena ninapata kuweka mawazo ni fikra zangu hapa jamvini ili sote tujadili na kutafakari kwa pamoja kwa ustawi wa fikra zetu na Taifa kwa ujumla.

Leo nitajikita kwenye kauli mbili alizozitoa mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA Mh.Freeman Mbowe ambaye mimi hpenda kumwita simba wa vita.Kauli ya kwanza ni ile aliyoitoa mkoani Mtwara ya kwamba atajiuzuli siasa endapo CHADEMA haitashika dola katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.Kauli ya pili ni hii ya hivi karibuni kuwa atajiuzulu kuongoza CHADEMA ikiwa uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 utapelekea idadi ya wabunge wa CHADEMA kipungua.

Kabla ya kueleza tafsiri yangu juu ya kauli hizi mbili napenda kuweka wazi kuwa mimi ni mfuasi na ni mtu ninayemwamini sana Freeman Mbowe na kipekee nampongeza kwa kazi kubwa aliyoifanya kuifikisha CHADEMA hapo ilipo hivi sasa.Kwa uongozi wake napata ujasiri wa kusema kusema kuwa ni mwendawazimu pekee ndiye atakaeweza kuudharau ama kukashifu uongozi wake katika kipindi chote alichokuwa mwenyekiti wa chama.Sina maana kwamba hastahili kusolewa popote bali uongozi wake kwa ujumla unastahili kupongezwa.

Nirudi kwenye hoja ya msingi juu ya kauli zake mbili nilizoziainisha mwanzoni mwa tafakari hii.Kwa ujumla kauli zote mbili zinanipa picha kuwa Mbowe anaamini kuwa CHADEMA ipo tayari kushika dola.Na pengine kauli hizi zinanipa picha kuwa mbowe tayari ameshaonyesha uwezo wake wote katika kukijenga chama na hivyo kama malengo yake hayatatimia basi yupo tayari kuachia wengine kwani hatakuwa na jipya tena.Sura nyingine ninayoiona kauli hizi ni kukata tamaa mapema pale ambapo malengo hayatimii kitu ambacho ni hatari sana kwa wanamapinduzi ama kwa wanaoongoza mabadiliko.Nataka nimkumbushe mwenyekiti wangu kuwa njia sahihi ya kutatua tatizo sio kulikimbia tatizo bali ni kukabiliana nalo hadi mwisho wake.Steve Biko alipata kusema ni heri kuishi muda mfupi duniani jina lako likabaki linaishi kwa wema duniani kuliko kuishi miaka mingi ukatoweka kama mzoga duniani.Kipekee ninatamani kumuoma mbowe kwenye siasa za nchi hii mpaka pale tutakapotangaza ukombozi wa taifa letu sote na sio wengine kubaki nyuma.

Kwa upande wa kauli ya pili ya kuacha kuongoza chadema endapo idadi ya wabunge itapungua.Japo hakusema kuiongoza CHADEMA katika ngazi gani ila akili yangu kwa tafsiri ya haraka imebaki kwenye uenyekiti.Kama ni hivyo kauli hii inanipa picha kuwa mbowe bado anautaka uwenyekiti katika uchaguzi wa ndani wa mwaka huu.Kama hayo ndiyo malengo yake mimi binafsi namuunga mkono ila ninachoomba ni uchaguzi kufanyika katika misingi ya democrasia na uwazi.

Karibu tutafakari pamoja.

By. Nicholaus Ngowi( mtoto wa seremala)[/QUOTE Mtoto wa seremala Mbowe alipokuwa mtwara hakusema kama Chadema itashindwa kushika dola alichosema ni kama watashindwa kuweka mbunge katika jimbo la Masasi 2015, atajiuzulu nimetoa hiyo kumbu kumbu kwa faida ya wengine juu ya kauli ya kujiuzulu ikiwa mazingira hayo yatajitokeza.
 
Kama mtu ni well learned na uko makini huwezi toa kauli za hivyo wakati hujafanya utafiti wowote utakaokupelekea kuamini hivyo. Kwa siasa Muda bado ni mwingi na lolote laweza kutokea. Ni sawa na mtoto anaposema haya mahindi yasipoiva najinyoka, wakati mahindi yanategemea mvua na yeye hana control nayo. Kiddish

Rudi darasani nas ujifunze siasa, ndipo utakapoelewa maneno haya ni ya kawaida saana kwa wanasiasa!
 
thubutu mbowe aachie uongozi? awapi, nani kakuambia? labda ruzuku isiwepo, na tena ukizingatia jamaa ni kutoka kale kakabila kanako muamrisha mungu onyesha sehemu hela ilipo (moshi).
 
Back
Top Bottom