Habari wana JF
Ni wasaa mwingine tena ninapata kuweka mawazo ni fikra zangu hapa jamvini ili sote tujadili na kutafakari kwa pamoja kwa ustawi wa fikra zetu na Taifa kwa ujumla.
Leo nitajikita kwenye kauli mbili alizozitoa mwenyekiti wa chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA Mh.Freeman Mbowe ambaye mimi hpenda kumwita simba wa vita.Kauli ya kwanza ni ile aliyoitoa mkoani Mtwara ya kwamba atajiuzuli siasa endapo CHADEMA haitashika dola katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.Kauli ya pili ni hii ya hivi karibuni kuwa atajiuzulu kuongoza CHADEMA ikiwa uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 utapelekea idadi ya wabunge wa CHADEMA kipungua.
Kabla ya kueleza tafsiri yangu juu ya kauli hizi mbili napenda kuweka wazi kuwa mimi ni mfuasi na ni mtu ninayemwamini sana Freeman Mbowe na kipekee nampongeza kwa kazi kubwa aliyoifanya kuifikisha CHADEMA hapo ilipo hivi sasa.Kwa uongozi wake napata ujasiri wa kusema kusema kuwa ni mwendawazimu pekee ndiye atakaeweza kuudharau ama kukashifu uongozi wake katika kipindi chote alichokuwa mwenyekiti wa chama.Sina maana kwamba hastahili kusolewa popote bali uongozi wake kwa ujumla unastahili kupongezwa.
Nirudi kwenye hoja ya msingi juu ya kauli zake mbili nilizoziainisha mwanzoni mwa tafakari hii.Kwa ujumla kauli zote mbili zinanipa picha kuwa Mbowe anaamini kuwa CHADEMA ipo tayari kushika dola.Na pengine kauli hizi zinanipa picha kuwa mbowe tayari ameshaonyesha uwezo wake wote katika kukijenga chama na hivyo kama malengo yake hayatatimia basi yupo tayari kuachia wengine kwani hatakuwa na jipya tena.Sura nyingine ninayoiona kauli hizi ni kukata tamaa mapema pale ambapo malengo hayatimii kitu ambacho ni hatari sana kwa wanamapinduzi ama kwa wanaoongoza mabadiliko.Nataka nimkumbushe mwenyekiti wangu kuwa njia sahihi ya kutatua tatizo sio kulikimbia tatizo bali ni kukabiliana nalo hadi mwisho wake.Steve Biko alipata kusema ni heri kuishi muda mfupi duniani jina lako likabaki linaishi kwa wema duniani kuliko kuishi miaka mingi ukatoweka kama mzoga duniani.Kipekee ninatamani kumuoma mbowe kwenye siasa za nchi hii mpaka pale tutakapotangaza ukombozi wa taifa letu sote na sio wengine kubaki nyuma.
Kwa upande wa kauli ya pili ya kuacha kuongoza chadema endapo idadi ya wabunge itapungua.Japo hakusema kuiongoza CHADEMA katika ngazi gani ila akili yangu kwa tafsiri ya haraka imebaki kwenye uenyekiti.Kama ni hivyo kauli hii inanipa picha kuwa mbowe bado anautaka uwenyekiti katika uchaguzi wa ndani wa mwaka huu.Kama hayo ndiyo malengo yake mimi binafsi namuunga mkono ila ninachoomba ni uchaguzi kufanyika katika misingi ya democrasia na uwazi.
Karibu tutafakari pamoja.
By. Nicholaus Ngowi( mtoto wa seremala)