Tafakari ya Mwanakijiji leo...


katika kiwango changu kidogo cha usomaji wa mambo ya utawala bora na utawala wa demokrasia ckuwahi pata kukutana na kitu ushawishi kama sehemu au kanuni moja wapo ya utawala bora, kiongozi bora. Je nipate kuyaamini toka kwako kua ushawishi ni ni sehemu ya kiongozi bora?? Na unahisi dunia yote ya sasa itasadiki vivyo?
 
vitabu vitakatifu vinatueleza ya kua yatupasa kukwepa vishawishi, hapa we unaliongeleaje baina na kiongozi na waongozwaji?

kuna tofauti kati ya vishawishi (temptations) na ushawishi (persuasion).
 

we jamaa usituchoshe, wilson mandela ndio nani? cdm ina kila aina ya watu kwakweli.
km kweli mbona mlomtaja kama kinara hamjamfukuza?
 

Nadhani bado watu awjamuelewa MMK, anasema uongozi bora sifa yake kuu ni ushawishi, hapa anamaanisha hata kama katiba inavunjwa,na mtu akionywa na bado akaendelea kuivunja aendelee kushawishiwa asipewe adhabu..hii ni popote sababu anasema katika moja ya post zake hajakilenga tuu chama!(Hata jeshini) anamaanisha ili uongozi bora uwe bora na usio na tatizo pasiwe na vitisho,kikwara,kutegeana, kunyemeleana..uongozi msingi wake ni ushawishi!.. Labda wale mliosoma political science mtuambie .
 

kama ndivyo ulivyoelewa hakuna msaada kwako.
 

Ila hamna sehemu tunaonesha mwl Nyerere akiwashawishi wanaovunja maadili katika chama au serikalini akiwaomba na kuwashawishi waache..alifuata principles, ukiwa umekamatwa na tuhuma tu za rushwa wakati wa nyerere kabla tu haijathibitika you was supposed to step down, ikithibitika mahakamani adhabu hawakuiachia mahakama,ilikua ni kifungo na viboko wakati wa kuingia na kutoka..

Nyerere anasisitiza "hatukua na mchezo".. Ukimsikiliza zaid hotuba za nyerere anasifu uingereza wanavyoheshimu principles kwa kutolea mfano yule waziri alietembea na mama mmoja wa barabarani....unasema ujazungumzia somo zima la uongozi lakini kiini chake ni "ushawishi"..

Ningeomba go and read this book " leviathan" utaikuta social contract ya Thomas Hobbs (father of liberal thoughts)..pima anachosema na ulichosema.. Anaifaahamu hiyo democracy zaidi yako yet anasema human lazma tuset contract ambayo ndio msingi utakaotuongoza na kiongozi kusimamia hii misingi tuliyokubaliana ndio uongozi bora.
 

hizo semina zake niliingia mbili tu nkaona hana jipya sikuingia tenaaaa.
 

Tofauti kubwa ya mwanadamu ni uwezo wake wa kutumia akili yake kufikiri kuliko kufikiriwa na wengine. Mapendekezo yanayotolewa na wengine tunatakiwa tuyapime na kuona kwa kiasi gani tunakubaliana nayo. Nyerere kwa mfano aliweza kusikiliza mambo mengi lakini hakuwa na papara ya maamuzi. Unaposema kufuata kanuni na sheria hilo halina shaka hata kidogo lakini ni uongozi mbaya kufuata tu "the letter of the law" na siyo "the spirit of the law". Kanuni na Sheria zimewekwa ili kusaidia pale ambapo njia za ushawishi zinaposhindikana.

Mtu anapoharibu huweza kuhojiwa, kupewa ushauri na kusahihishwa na wakati mwingine kuonywa hii yote ni sehemu ya ushawishi. Unapoamua kusema huyu mtu hafai kabisa na unaamua kumtupa nje ni kwa sababu njia nyingine zote za ushawishi zimeshindikana. Kumbe ushawishi huo huo unaweza kabisa kuwemo ndani ya hiyo contract na kiongozi mzuri ni yule anayejua ni wakati gani wa kutumia nini na kwa vipi. Binafsi sioni tofauti ya kile ambacho ninakisema na ambacho wengine wamewahi kukisema.
 
Sishindwi. Hivi mkuu kipimo cha ushawishi ni nini? Nani apime? Hapa hakuna subjectivity! Na kama ipo atakae judge nae hatakuwa na muono subjective MM? Unataka tusome tu ulichoandika, tukariri kama kasuku Mm?
 
kama ndivyo ulivyoelewa hakuna msaada kwako.

Mkuu,

Wewe umekuwa Mwl wangu sana na kwa muda mrefu sasa.mawazo yako yanajenga sana lakini wakati mwingine huibua mjadala usiotoa suluhisho na hapa ndio ninapoona wakati mwingine unaweka kikwazo bila kujua kwenye jasho lako mwenyewe kukomboa Watanzania.

Mfano mdogo nukuu hii iliyoibua mjadala unadhani kama ungeiandika kwa namna ya kumgusa vizuri kila muhusika(kama unavyosema) Zitto angepata nguvu ya kuinukuu?

Nakuhakikishia nukuu yako haikujitosheleza kugusa vizuri pande zote kulingana na mfuatano wa matukio.

Niliwahi kusema humu watu wenye ushawishi kama wewe wakati mwingine tena muhimu huwa hampo wazi kwenye issues zinazohitaji karipio la wazi la kila mtu hasa linapogusa wapinzani.

Unaweza kutuona tuna akili ndogo kushindwa kuelewa kusudio lako lakini itakuwa yale yale ya wewe kushindwa kutushawishi!

ulipotumia neno kufukuzana huku pakiwa na vijana waliofukuzwa uelewekaje?

Umewasaidiaje hao vijana waliofukuzwa zaidi ya kama kuwaambia mmeonewa?
 

Unaakili sana! Very true!
 
Mwanakijiji acha unafiki. Sasa ulitaka BAVICHA wakae na hao panya kama CCM wanavyokumbatia mafisadi na kuwagharimu mara waendapo kwa wananchi.

Mm nadhani CDM wanaonyesha ukomavu ktk uongozi kimaadili. Huwezi kuanika utumbo wako kwa kukashifu viongozi then uachwe eti ushawishie kujirudi.

Na ukweli wameusema wenyewe kusaliti chama na kuanzisha chama kingine ili kuhujumu chama. Kama CCM waliwavumilia akina NAPE, SITA na wengine CDM ni tofauti. Najua huwezi kuonyesha direct impact kwa mwananchi lkn impact ni kubwa kwa chama mbele ya jamii.

Maake kinaweza kufa kwa kuvumilia upuuzi wa watu wachache wanaofadhiliwa na Chama adui wa Watanzania yaani CCM IS BIG SPONSER ON THAT ISSUE. Sasa CCM wawachukue hao masalia ili wawatumie kwenye vyama vingine lkn kwa CDM, big NO!!
 
Well said

QUOTE=Kiungani;5401735]Natafakari na nazidi kuelewa nini maana ya TANU/AFRO SHIRAZ/CCM kushindwa kwa HOJA kwa kuwatimua Mtemvu, Fundikira, Msangi, Hanga, Maalim Seif, Jumbe, Babu, n.k.

Huko kulikuwa ni kushindwa kwa hoja kwa uongozi wa Mwalimu JKN. Uongozi siyo vitisho wala mikwara.

Vile vile natafakari na kuelewa kukubalika na kutoshindwa kwa hoja kwa Mwenyekiti JMK kwa kutowavua magamba mapacha watatu: Lowassa, Rostam na Chenge na mafisadi kedekede ndani ya CCM, pamoja na wale waliopata nafasi zao kwa rushwa za uchaguzi.

Huu ndiyo uongozi uliokubuhu na usiyo na vitisho wala mikwara. Hakuna mambo kama vile kupeana siku 90 kwa magamba kujivua au wale walioshinda NEC kwa rushwa "kushughulikiwa" ndani ya miezi 6. Uongozi siyo vitisho wala mikwara.

Mwanakajiji, with all due respect, nashindwa kukuelewa na hii tafakuri yako. Is it not the case of what is good for the goose?

Pia kama mwana-CCM nitategemea kuwa chochote CDM, TLP au NCCR inachofanya kujidhoofisha ni baraka kwa CCM kwani kuvuja kwa pakacha.............!!!!

Sijawahi kuona bondia anamuongezea lishe bora mpinzani wake ili pambano liwe zuri.[/QUOTE]
 
Nimekuja spidi nilipoona kichwa cha habari nikadhani ni hoja ya rafiki yangu Mzee Mwanakijiji. Kumbe . . . . hata hivyo hongera kwa kunikamata!
 
Last edited by a moderator:

Mtazamo,

Ni vizuri kuelewa kuwa hilo unalosema nalo limo ndani ya nilichosema lakini sicho pekee nilichosema au kumaanisha. Suala la BAVICHA kwa kweli ni suala dogo sana ukiliangalia. Halikutakiwa kufika lilipofika na kama kungekuwa na uongozi wenye kushawishi lisingefikia watu kufukuzana. Sasa hivi inaonekana kuwa mtu akipata mwiba kwa vile unauma sana basi anaamua kukata mguu. Well.. umetatua tatizo lakini kweli umetatua?

Lakini hoja yangu ni kubwa zaidi. Nimeandika nikifiria majibu ya serikali dhidi ya walioandamana kule Mtwara na jinsi serikali hadi Ikulu ilivyokuwa juu kiasi cha kuwafanya wananchi wa Mtwara waanze kuwa na hofu. Tusipoangalia umwagikaji mkubwa wa damu unaweza ukatokea Mtwara kwenye suala hili hili. UOngozi ni ushawishi lakini watu wasio na ushawishi wa hoja mara nyingi huamua kutumia nguvu. Sasa ushawishi wa nguvu unatatizo moja kubwa - ili uzidi kushawishi zaidi inabidi utumie nguvu zaidi.
 
Sitaki kuamini kwamba you are the only one here who can think kidogo broad whatever wider as you've just pointed OUT. Re-think MMK na usitukune watu.

Hoja kwa Hoja. Hesabu maneno yako. Jua wengine pia watayahesabu

Take that from me.
 

Hebu ngoja niangalie kwa upande mmoja hivi kukashifu viongozi limekuwa kosa kubwa hivyo? Really? Kweli mwanachama kuwasema vibaya viongozi wake ni sababu tosha ya kumvua uanachama? Are you guys serious? Sijui hata kama mnaelewa implication ya mnachokitetea.

Ndio maana utaona sijachangia kabisa hoja hizi za sijui kiongozi gani anasemwa sijui nani anamuita nani nini; ni upuuzi hata kuchangia. Tunataka viongozi wanaopendwa tu wasio semwa, wasiokashfiwa, wasiojaribu kuoneshwa duni mbele ya wananchi? Tunataka demokrasia au nini?


sawa kama kuna sababu ya kuwavua watu uanachama ni hii peke yake. Lakini uthibitisho ni lazima uwe impeccable.
Maake kinaweza kufa kwa kuvumilia upuuzi wa watu wachache wanaofadhiliwa na Chama adui wa Watanzania yaani CCM IS BIG SPONSER ON THAT ISSUE. Sasa CCM wawachukue hao masalia ili wawatumie kwenye vyama vingine lkn kwa CDM, big NO!![/QUOTE]
 



Sisi unaotuita wajinga wa kufikiri, Nataka nikuhakikishie hatusomi thread tukaishia hapo, we take it kidogo to next level of thinking.
1. Kauli/Thread hii imeandikwa na nani?
2. Thread hii imeandikwa wakati gani?
3. Thread hii imeandikwa katika mazingira gani?
4. Thread hii inamlenga nani? (For this matter OK as you've Just said MTWARA,Uongozi wa Vyama, BAVICHA)
Baada ya hapo sisi 'wajinga' ndio Analysist.

Despite all. I still respect you MMK
 

Mkuu unaweza kushawishi kwa kujiamini pale tu kitu unachosimamia ni dhamira safi.Wananchi wana madai ya msingi na serikali inajua ni ya msingi lakini yaliyo nje ya mpango wao wenye maslahi tusiyoyajua.

Huwezi kushawishi u.puuzi zaidi ya kutumia nguvu hasa ukijua hula ya unao waongoza ni Watanzania! Hawa si wakuwaimbia nyimbo za falsafa ni kusema kwa kauli moja inatosha inabidi wasikilize umma kwa nguvu.

By the way mkuu,serikali imeshindwa kutushawishi, sawa.lakini huoni na sisi tumeshindwa kuwashawishi vile vile?

Hapa tukubaliane pande zote tumefeli na kuhatarisha muelekeo wa Taifa! Basi walau tusake muafaka!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…