tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,854
- 1,145
Mwisho wa siku hutulazimishi tuamini kwamba kila mtizamo wako ulivyo basi ndio uko sahihi, ni wewe ndio ulikuwa mpiga debe mkubwa wa CCJ kwenye Media matokeo yake chama kikafa kabla hakijasajiliwa, kuna muda tuache tutumie uwezo wetu wa kufikiri na usidhani unaweza kufikiri kwa niaba yetu, hell no.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/380596-tafakari-ya-mwanakijiji-leo.html
Mbona hiyo nukuu tumeambiwa ni ya Mzee Mwanakijiji wewe unasema ya Zitto? Mods which is which?
Mbona hiyo nukuu haipo kwenye facebook ya Zitto? hebu rudi tena kwenye account ya Zitto ujiridhishe, mimi nimeangalia hamna kitu kama hicho yeye anaongelea katiba mpya kwenye post zake za leo.soma vizuri nilichoandika unalia nini kwa mods?
Zitto kanukuu hiyo kutoka kwa mwanakijiji akaiandika kinafiki kwenye fb page yake, what does it mean?
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/380596-tafakari-ya-mwanakijiji-leo.html
Mbona hiyo nukuu tumeambiwa ni ya Mzee Mwanakijiji wewe unasema ya Zitto? Mods which is which?
Chadema hakuna uongozi ....viongozi wa chadema upeo wa kutatua migogoro ni kufukuzana tu......inatia shaka
Uongozi ni ushawishi. Uongozi siyo kutegeana, kutegeshana, kunyemeleana na kufukuzana. Na uongozi siyo vitisho au mikwara. Kiongozi anayeishi kwa vitisho ni kiongozi aliyeshindwa hoja. Hili ni kweli kwa vyama vile vile; chama kinachoishi kwa vitisho kimeshindwa hoja. Tafakari
- Ndio maana nilisema Zitto, Mwanakijiji na Dr. Kitila ndio wanaofaa kugombea Urais Chadema, hii ya leo inaitwa kumkoma nyani giladi!!
le mutuz
MMK umeweka mpaka wa uongozi sehemu ambayo siyo. Jaribu kusoma taasisi mbali mbali zenye nidham uone inajengwaje. Anza na jeshi ( sio lazima iwe Tz)
Uongozi ni kusimamia sheria na taratibu zilizopo. Uongozi ni mambo mengi.
Kazi pia ya kiongozi ni kumpeleka punda kunywa maji. Swala la kunywa ni juu ya punda.
Jifunze kwa Wilson Mandela na mke wake wa kwanza Winnie ujue athari za usaliti.
Na CCM nani na nani wanafaa kugombea Urais?
Usisome zaidi ya nilivyoandika; unaweza kuapply kwenye lolote vile.
Kwani nimeandika somo zima la uongozi? of course uongozi ni zaidi ya haya lakini kiini hasa cha uongozi ni ushawishi siyo sheria wala taratibu. Ni uwezo wa kushawishi watu kuona wasichokiona, kukubali ambalo walikuwa hawakikubali au hawataki kukikubali na kutenda yale ambayo vinginevyo wangekuwa wanasita kuyafanya. Huwezi kuwa na kiongozi ambaye anakimbilia 'taratibu na sheria' kwa vile kashindwa kushawishi.
Kitu kimoja ambacho Nyerere alikuwa mbali sana kuliko viongozi wetu wengi wa sasa ni kuwa aliweza kushawishi (kama alishawishi kwa mazuri au la hilo jingine). Kiongozi ni lazima ajifunze kushawishi. Na hili ni kweli zaidi kwenye utawala wa demokrasia.