Kisusi Mohammed
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 563
- 468
Assalaamu alaykum, hongereni kwa swaum. Hili zoezi la vitambulisho vya taifa sijalifatilia kwa undani, ila kwa mtazamo wa jumla linaonekana kuwa na nia njema na wananchi wa Tanzania. Kinachonipa tabu katika zoezi hili ni kuhusu mchakato wa utoaji taarifa kwa wananchi, uandikishaji, vitendea kazi vya zoezi, rasilimali watu na uwezo wao na kubwa zaidi ni vigezo vya mwananchi muandikishwaji. Kwa mfano: Mimi sikubahatika kupitiwa na wale vilaza waliokuwa wanaandikisha watu nyumba kwa nyumba, nilipokwenda ofc za serikali ya mtaa wakaniambia kuwa, kwa waliokosa kuandikishwa mtaani wataandikishwa tar. 28, 29 na 30. Waende na vivuli vya viambatanisho (kadi ya mpiga kura au leseni ya udereva au cheti cha kuhitimu shule). Kwa bahati leo asubuhi nikawa mtu wa kwanza kufika kituo cha kuandikisha nikiwa na vivuli vya viambatanishi vyote walivyohitaji, nilipofika kwa muandikishaji ananiambia sina barua ya kunitambulisha toka kwa mjumbe wangu! Nimeshindwa kuelewa kwa nini hawakuorodhesha kigezo hicho cha barua ya utambulisho ya mjumbe toka zamani kwny matangazo yao ya vipeperushi?! Kwa kweli imenikera, na kwa upuuzi huo, nimeahidi kuwa, sihitaji tena hicho kitambulisho chao kwa sbb hata taifa lenyewe limeshauzwa na kutaifishwa na walafi wachache wenye madaraka, ndio maana hata zabuni yenyewe ya hivi vitambulisho wamepeana kishemeji ili waendelee kutumaliza kabisa. Imeniuma sana.