Hadithi.
Na. Musumi.
Siku moja Baba aliamua kuficha kitumbua cha Mtoto wake Baada ya kuficha Mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo.
Mtoto:analia sana kwa kupoteza kitumbua
Baba: anauliza! Mwanangu kwanini unalia!
Mtoto: Kitumbua changu kimepotea!
Baba😛ole Mwanangu kimeishapotea!
Mtoto: akaendelea kulia analia sana!
Baba: Mwanangu nyamaza ngoja nikakutafutie!
baada ya muda kidogo baba akaja na kitumbua.
Baba: mwanangu kitumbua hiki hapa nimekipata.
Mtoto: akafurahi sana na kumuuliza, baba umepata wapi kitumbua changu!
Baba: mama yako ndio alikuwa ameficha.
Mtoto alimchukia Mama kwasababu alikuwa anataka kumnyima chakula.
Ila Mama baada ya kusikia hivyo alikuwa hana uwezo wa kumwambia Mwanae kama sie yeye aliyekuwa ameficha kitumbua.
Kwasababu Mama anaona akisema anafahamu tabia ya Mmewe kwa ukali, hivyo anaweza sababisha Ndoa kuvunjika kisa kitumbua cha Mtoto.
Mama aliamua kunyamaza Kimya, Mtoto akaendelea kufurahi na kumshukuru Baba.
Je Baba alikuwa na lengo gani kuficha kitumbua??
Busara za Mama kunyamaza ziko sahihi?
Mtoto kumshukuru Baba wakati ndie Aliyefucha, yuko sahihi au kwa vile hajui?
Nakutakia Sikukuu Njema.