Tafadhali Wabunge wetu, ACHENI KULALAMIKIA bajeti timizeni wajibu wenu!

Serikali haina uwezo au nia ya kutekeleza mpango wa maendeleo, au imeshindwa kuutafasri katika bajeti yake.
 
Nape, mbona uko hapa chini ukichungulia bila ya kujibu kitu, au picha za Iringa zimekuogofya!

Nimewaambia anayetaka mjadala wa Iringa aanzishe thread yake, ntakuja huko hapa tunajadili role ya wabunge kwenye kujadili bajeti ya serikali......
 
Nnauye Jr Kijana aliyechanganyikiwa na M4C ya Chadema, Nnauye Jr ni Mropokaji kama Yule wa Ombaomba wa Kimataifa alipangishwa na NEC kule Magogoni kila kukicha kiguu na njia kwenda kutembeza kopo ili aongezee bajeti uchwara. Hebu tumieni akili Nnauye Jr na umwambie yule mteule wa NEC kule magogoni atumie akili pia msitumie masaburi.

Nnauye Jr bajeti hii inawalenga nyie Mafisadi sio Mlalahoi, Watumishi wetu wana haki ya kuja huku barabarani na kulalamika kwa kuwa katika Bunge la Mafisadi wanadharauliwa.

Come 2015 Nnauye Jr utangulie Segerea mwenyewe kama ulivyosema na usisahau kumwambia yule mteule wa NEC na Mafisadi wenzake wajijengee sehemu nzuri huko Segerea ndiko mtakapo malizia maisha yenu kwa ufisadi mliotufanyia. Pesa mnazo jijengeeni magereza yenu Mafisadi
 
Umenena vema mtoa hoja. Wabunge wamepewa nafasi kubws sana na ya muhimu katika kujadili bajeti, wana uwezo wa kuikataa, sasa wanapolalamika majukwaani ni kutokujua wajibu wao au ndo kujiosha kwa wananchi tu hafu wakifika bungeni wsnadai naunga mkono bajeti, nyuma ya pazis washachukua rushwa. Waache unafiki.
 
HIVI KWANINI WABUNGE WETU WANALALAMIKA JUU YA BAJETI BADALA YA KUTIMIZA WAJIBU WAO?! WANAMLALAMIKIA NANI?

Kimsingi bajeti inapopelekwa Bungeni na serikali inakwenda kwa ajili ya mjadala na marekebisho palipo na mapungufu NA SI KUPITISHWA KAMA WAJIBU TU, tunategemea mjadala wenye lengo la kuboresha bajeti iliyowasilishwa bungeni kwa faida ya wananchi.

Sasa haya malalamiko ya baadhi ya wabunge barabarani, mara "niko tayari kufukuzwa"!! Nani anamfukuza nani?! Nani anayetishia uhuru, haki na wajibu wa kikatiba wa wabunge wetu mpaka wanalalamika barabarani?!!

Nashauri wabunge timizeni wajibu wenu, jadilini na kuishauri serikali ndani ya bunge juu ya maboresho ya bajeti iliyoletwa kwenu! Kulalamika barabarani kunaonyesha ama baadhi hawajui wajibu na haki zao kikatiba, au kuna watu wanatafuta umaarufu binafsi. Hivi kila mmoja akilalamika na nyie tuliowapa dhamana ya kuisimamia na kuishauri serikali maana yake nini? Nyie mlalamike na wananchi walalamike kuna sababu gani ya nyie kupewa dhamana hii kubwa mliopewa!!

With due respect TIMIZENI WAJIBU WENU BUNGENI NA SI BARABARANI KULALAMIKA KUTWA KUCHWA!
With due respect haya ndiyo mtatizo ya hawa wabunge wa chama chetu kufikiria kwa kutumia masaburi yao badala ya mbongo zao
 
Wabunge wanatuangusha sana kwa hili. Wamekuwa wanafiki zaidi kuliko maslahi ya wananchi.Rushwa inachukua nafasi kubwa katika kupitisha bajeti kuanzia ngazi ya halmshauri kwenye kamati hadi wizara hadi huko bungeni kwenyewe. Sina imani na mbunge yoyote yule naacha tu fate ichukue mkondo wake.
 
Jamani wabunge wanaosema wako sahihi kabisa na mimi nawapongeza, kikatiba bunge ndio chombo kikuu cha maamuzi nchini na ndicho chenye dhamana ya kusimamia na kushauri serikali. Lakini kwa mda mrefu kimepokonywa madaraka haya na serikali imejiweka juu ya bunge na kupuuza serikali. Hivyo kunahitajika uhamasishaji wa jamii ili ifike wakati sote tutambue kazi ya bunge si kulalamika tu bali wanarungu wasilolitumia la kuishauri serikali na inapokaidi wanawajibisha.

Tunaposema madaraka yarudi kwa wananchi, maana yake ni bunge kurudishiwa mamlaka yake na hawa ndio wawakilishi wetu. Kama ni kampuni inayoitwa tanzania wabunge ndio bodi.

Tutambue bunge si mali ya vyama vya siasa bali ni muhimili wa utawala unaowakilisha wananchi ila vyama vya siasa vimepora chombo hiki na kukifanya mali yao.

Chama cha siasa ni dhamana ya kuingilia bungeni tu hivyo mbunge anayesema nitasimamia hoja za wananchi bila kujali chama changu kinapenda au hakpendi huyo ndio mbunge anayestahili kukaa bungeni, anayebeba hoja za chama aende kituo cha demokrasia humo ni siasa.

Kuna haja ya kuondoa kambi kwenye chombo chetu hiki ili kisimamie vizuri serikali na kuishauri.

Tukumbuke hii ni bajeti ya nchi si ya vyama hivyo wananchi tuwapongeze wabunge wanaoanza kutambua wajibu wa bungni ni nini? Bunge ni chombo cha nani? Chama au wananchi? Je bunge linasimamia serikali kama chombo hiki kinavyotakiwa kufanya kwa kugawanyika ki vyama.

Vyombo vya habari wasiturudishe nyuma kwa kuwaita wabunge wanaojimbua waasi.

Vyama jijengeni kwa kutoa kauli za kupongeza wabunge wanaokuwa na misimamo ya kutetea wananchi hadharani. Anayetetea wananchi hahitaji kukaa kimya eti atajadili bungeni bali awafahamishe waliomtuma nini msimamo wake
 
Nimewaambia anayetaka mjadala wa Iringa aanzishe thread yake, ntakuja huko hapa tunajadili role ya wabunge kwenye kujadili bajeti ya serikali......

Nakubaliana na wewe, ila inaelekea pamoja na kuwa na semina elekezi za mara kwa mara, Wabunge wa chama chako hawajui ROLE yao kwenye kujadili bajeti ya serikali yao ndiyo maana wanalilia barabarani!
 
Jamani wabunge wanaosema wako sahihi kabisa na mimi nawapongeza, kikatiba bunge ndio chombo kikuu cha maamuzi nchini na ndicho chenye dhamana ya kusimamia na kushauri serikali. Lakini kwa mda mrefu kimepokonywa madaraka haya na serikali imejiweka juu ya bunge na kupuuza madaraka ya bunge. Hivyo kunahitajika uhamasishaji wa jamii ili ifike wakati sote tutambue kazi ya bunge si kulalamika tu bali wanarungu wasilolitumia la kuishauri serikali na inapokaidi wanawajibisha. Huwezi kusema kurudisha madaraka kwa wananchi ni mikutano ya vijiji kama wengi tunavyoshauri. Bali bunge ndio muhimili wa wananchi.

Tunaposema madaraka yarudi kwa wananchi, maana yake ni bunge kurudishiwa mamlaka yake na hawa ndio wawakilishi wetu. Kama ni kampuni inayoitwa tanzania wabunge ndio bodi.

Tutambue bunge si mali ya vyama vya siasa bali ni muhimili wa utawala unaowakilisha wananchi ila vyama vya siasa vimepora chombo hiki na kukifanya mali yao.

Chama cha siasa ni dhamana ya kuingilia bungeni tu hivyo mbunge anayesema nitasimamia hoja za wananchi bila kujali chama changu kinapenda au hakpendi huyo ndio mbunge anayestahili kukaa bungeni, anayebeba hoja za chama aende kituo cha demokrasia humo ni siasa.

Kuna haja ya kuondoa kambi kwenye chombo chetu hiki ili kisimamie vizuri serikali na kuishauri.

Tukumbuke hii ni bajeti ya nchi si ya vyama hivyo wananchi tuwapongeze wabunge wanaoanza kutambua wajibu wa bungni ni nini? Bunge ni chombo cha nani? Chama au wananchi? Je bunge linasimamia serikali kama chombo hiki kinavyotakiwa kufanya kwa kugawanyika ki vyama.

Vyombo vya habari wasiturudishe nyuma kwa kuwaita wabunge wanaojitambua kuwa waasi.

Vyama jijengeni kwa kutoa kauli za kupongeza wabunge wanaokuwa na misimamo ya kutetea wananchi hadharani. Anayetetea wananchi hahitaji kukaa kimya eti atajadili bungeni bali awafahamishe waliomtuma nini msimamo wake
 
Ni aibu ilioje kwa mwanasiasa na wapambe waliolipwa kuteka soko na kuzuia barabara ili kuhutubia. Nape mnatumia nguvu kujenga chuki dhidi ya chama cha mapinduzi na serikali yake.
 
Ni Barabara hipi hiyo na ya kuelekea wapi wabunge wetu ambao wako tayari kwa lolote? Ni barabara ipi hiyo ambayo watu wanasimama kusikiliza kilio cha ukombozi wa mtu waliyemtuma kuwakomboa katika jehanamu ya CCM iliyokalia mirija yote ya Asali ya nchi yetu huku ikiinyonya na kubakiza makapi. Sasa ni barabara ya kuleta mambo bara-bara kwa kukataa ukondoo walio uenzitangu enzi za mkapa, utawala wa wasio sikia la mkuu.
 
Back
Top Bottom