Tulia Ackson aendelea kukanyaga kanuni kumlimda bosi ya mumewe, akidi ya wabunge haijatimia kupitisha bajeti ya nishati

Samson Kwayu

Member
Jun 9, 2022
18
90
Spika wabunge la Tanzania ana kibarua kigumu sana kunusuru na kuhalalisha bajeti ya wizara ya nishati baada ya kulazimika kutoa ufafanuzi leo kuwa ni wabunge 193 tu waliohudhuria majadiliano na kikanuni ni sawa.

Hiyo inafuatia mining'ono iliyokuwepo ndani ya ukumbi wa bunge juu ya uhalali wa kisheria na kikanuni wa bunge kuendelea kujadili bajeti hiyo huku kukiwa wa idadi ndogo sana ya wabunge.

Kwa kifupi ni kuwa mbali na wabunge wengi kupewa rushwa ili kuipitisha bajeti hiyo , wamesusa kuwa sehemu ya uchafu na historia ya giza ambayo itakuja kuwajeruhi kwenye uchaguzi wa 2025 kwa kuwa sehemu ya majadiliano ya bajeti iliyojaa hadithi na mambo ya kufikirika kuliko uhalisia.

Watanzania wanataka umeme na hawataki porojo na hadithi za QR codes. Watanzania wanataka wajue waziri January Makamba anapewa na nani ruhusa ya kukwapua mabilioni ya fedha za watanzania kama ambavyo CAG ameaibisha kwenye ripoti yake.

Hii ndiyo wizara ambayo bajeti yake imejadiliwa na wabunge wachache sana kuliko wizara zote na tunaarifiwa sasa kuwa viongozi wa juu wa CCM ndani ya bunge wanapigia simu wabunge wao na kuwalazimisha kuwepo ndani ya bunge jioni wakati wa kupitisha bajeti. Sasa kama kwenye majadiliano hawakuwepo jioni mnataka wapitishe nini? Mnawalazimisha kwa maslahi ya nani?

Haitasaidia sana kwa sababu tumefanikiwa kuwashtaki wabunge waliokubali kuwa sehemu ya uchafu wa hii wizara kwa wananchi na tutakuwa mstari wa mbele kuwakumbusha watanzania 2025.

Kanuni zinaheshimiwa lakini kitendo cha wabunge wetu 200 kususia mjadala wa wizara ya nishati ni salamu tosha kuwa bajeti hii itapita kwa sababu za kikanuni huku kimsingi ni bajeti ya kinadharia tu na imekosa uungwaji mkono kama ilivyokuwa bajeti ya wizara ya ardhi.
 
Sukuma gang nawauliza swali. Mnadhani akili na uwezo wa Makamba jr utadhoofishwa na chuki zenu dhidi yenu?? Makamba Jr ni mtu smart kuliko viongozi wa kisiasa wote kwa sasa.

Fanyeni figisu, fanyeni ujinga wenu lkn ndiyo kwanza mnazidi kumpa umaarufu.
 
Back
Top Bottom