Tafadhali nichagulie Wimbo mzuri wa Kusikiliza ili nishushe Hasira zangu za Draw ya Kizembe ya Ndola nchini Zambia 16 Sept, 2023

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,727
109,294
Najitahidi kushusha Hasira za tokea Jana Jumamosi Saa 12 Jioni na hadi Usiku huu wa Saa 4 leo Jumapili bado tu hazijapungua kwa Draw ya Simba SC huko Jijini Ndola nchini Zambia.

Ukiwa ni Wimbo wa Kikongo ( Rhumba au Sebene ) nitafurahi zaidi kwani ndizo Nyimbo ambazo huwa nikiwa Nimekwazwa nikizisikiliza tu Hasira hupungua kama pia siyo Kuisha kabisa japo kwa Sisi Watu kutoka Mkoani Mara ( Musoma ) automatically tukizaliwa tu huwa tayari tuna Akiba ya Hasira ( Jazba ) ya 25% na hi haitoki au haipungui ng'o hata kwa Maombi ya Papa Mtakatifu wa Katoliki, Mtume Mwamposa Kawe Tanganyika Packers wala Kuhani Mwacha na Kimara Temboni yake.

Wachezaji wa Simba SC mmetukera!!
 
Back
Top Bottom